Jipatie jiko la gesi la kulipia kidogo kidogo kama luku kuanzia sh 1000

Jipatie jiko la gesi la kulipia kidogo kidogo kama luku kuanzia sh 1000

Sendaro

Member
Joined
Apr 5, 2012
Posts
58
Reaction score
28
Hili ni zuri sana, haikulazimishi kulipia mtungi mzima kwa Sh 23000 au Sh 58000. Kwa Sh 1000 yako tuu (buku) unanunua sehemu ya gesi iliyo kwenye mtungi na kupikia. Achana na zile gesi ikiisha unatelekeza mtungi na kurudi kwenye mkaa au kulazimika kutibua bajeti yako uliyojiwekea.

Unalipia kwenye tigo pesa, airtel money au m pesa kama vile unavyolipia vitu vingine.

Kizuri zaidi unaweza kufuatilia matumizi yako kwa kutumia mita maalum yenye kadi janja. Ujanja sasa ni teknolojia, hii ni mkombozi wako.

Jiunge leo kwa Sh 40000 na upewe jiko la sahani mbili na mtungi wake sambamba na salio la gesi ya kuanzia la Sh 5000 bure.

Huduma hii ni kwa Dar es Salaam pekee na usafiri ni bure mpaka kwako.
Tupigie sasa +255 713 748 763
 
Na gasi ikiisha kwenye mtungi ni njia gan inatumika kuujaza ?
Asante kwa swali lako, bahati nzuri tuna mifumo ambayo inafuatilia matumizi yako yote ya jiko lako, gesi inapokaribia kuisha tunapata ishara maalum ya mteja wetu kukaribia kuishiwa gesi. fundi wetu atafika mpaka kwako na kukubadilishia mtungi bila gharama yoyore
 
Na kwenye hio gas ya 23k mnataka faida kifupi utakuta mtu ananunua gas ya elf 40 kwenye kamtungi kakijaa kanauzwa 23k

Ukipiga mahesabu unaona work done is equal to zero
Labda tuu uelewe, hakuna kampuni isiyotaka faida. Halafu unapaswa kujua kuwa kuna bei elekezi ya gesi kutoka serikalini ambayo kampuni zote hutumia, pili ni salama na ipo kwa ajili ya mtanzania zaidi. Mfumo uliopo kweye jiko la sahani moja ukiujua hutumii tena. hebu fikria unatoa sh 40000 unapewa jiko na mtungi bado unalalamika, au hatujazoea mambo haya
 
Napewa au mnanipa nitumie kwa muda
 
Attachments

  • 299612984_5772783312740997_6206092647108123619_n.jpg
    299612984_5772783312740997_6206092647108123619_n.jpg
    66.3 KB · Views: 41
Labda tuu uelewe, hakuna kampuni isiyotaka faida. Halafu unapaswa kujua kuwa kuna bei elekezi ya gesi kutoka serikalini ambayo kampuni zote hutumia, pili ni salama na ipo kwa ajili ya mtanzania zaidi. Mfumo uliopo kweye jiko la sahani moja ukiujua hutumii tena. hebu fikria unatoa sh 40000 unapewa jiko na mtungi bado unalalamika, au hatujazoea mambo haya
Hizo gesi zina mita ya kuonyesha umetumia kiasi gani ya ulicho nunua!?
 
Yan katika kitu sitomshauli mtu kutumia hili jiko la et unalipia kidogo kidogo yan ni uhuni mtupu unajikuta samani yake ni sawa na kununua mitungi hiyo miwili naongea hivi nishatuma nikaonaga huu ni ujinga hakuna kusave hapa nikapiga chini nikafunga langu mpaka sasa natumia na kweli natumia bila stress kabisa
 
Back
Top Bottom