Jipatie jiko la gesi la kulipia kidogo kidogo kama luku kuanzia sh 1000

Mpaka picha ndio uamini?
Tafuta sehemu nzurnzuri upige picha nzuri. Hii itasaidia kutangaza bishara yako. Tekinolojia yako na ubunifu ni mzuri unaorahishisha maisha ya wengi.


Ongeza ubunifu wa kibiashara kuvutia wateja.

Vinginevyo hongera kwa kuja na wazo zuri km hilo la kubadili changamoto ya matumizi ya mkaa kwenda kuea gesi

Pamoja
 
Picha zipo nyingi sana ndugu
 

Attachments

  • 287309147_7639863612722529_4235309923810040881_n.jpg
    42.8 KB · Views: 22
  • 300792920_5513425345370132_6416045719178177298_n.jpg
    61 KB · Views: 21
  • download.jpg
    7.1 KB · Views: 22
  • jiko&mtungi.jpg
    27.6 KB · Views: 21
  • mgas2.png
    15.4 KB · Views: 19
  • sample5.png
    16 KB · Views: 17
  • tangazo.png
    67.9 KB · Views: 20
Wewe utakua dalali.

Mbona hii huduma mpaka Pwani bagamoyo ipo walishanipa vipeperushi vyao na mtaani kwangu wanapita sana na pikipiki lao la bluu la kuchaji. Toa taarifa kamili usaidie na wenginw na uisaidie kampuni yako.
 
Wewe utakua dalali.

Mbona hii huduma mpaka Pwani bagamoyo ipo walishanipa vipeperushi vyao na mtaani kwangu wanapita sana na pikipiki lao la bluu la kuchaji. Toa taarifa kamili usaidie na wenginw na uisaidie kampuni yako.
Ni kweli, baadhi ya maeneo ya mkoa wa Pwani imefika kama vile Bagamoy, Kibaha, Kwa Matheus na Mlandizi. Asante kwa kutuongezea
 
Wapi upo mkuu na ni kampuni gani.
 
Andron Mendes, Minaki boy, mtanzania mwenye asili ya mkoa wa Manyara, alianza na Kopagas, akishirikiana na Sabastian kutoka US.

Wakapambana na technology hiyo mpaka kufikia point ya kueleweka kwenye international innovation platform, na kuishawish kampuni mashuhuri inayojihusisha na biashara ya gas nchini uingereza iitwayo circle gas, wanaamua kuinunua technology hiyo kutoka kwa hawa wabia wawili (Andron n'a Sebastian) kwa donge nono la sh.billion 57.6 za kitanzania!

Andron anakuwa bilionea kijana kabisa katika ardhi ta Tanzania, akiwa na miaka 35 tu.

Mwezi Novemba, anapata janga la kumuua mlinzi wake wa godown la kuhifadhia gas kwa risasi, n'a kuutupa mwili wa mlinzi huyo huko kibaha...

Kesi inaendelea, tusubiri kuona nguvu ya pesa inavyonyinga haki za watu masikini...

Turudi, kwenye bei ya gas kupitia M-gas (Kopagas zamani), ni kweli kabisa kwamba huu ubunifu ni mzuri sana, lakini bei zake zipo juu mno, hufika mahali kg 1 ta gas huuzwa mpaka 5,000/= kwa mtu wa kipato kidogo atakimbia kuitumia, hii bado ni technology inayowarahisishia matajiri kutosumbuka sumbuka kununua gas mara kwa mara, na kusombelea mamitungi, otherwise masikini hawezi kumudu.

Ili iwe rafiki kwa wengi, serikali ione namna ya kumpunguzia kodi, ili na yeye auze kwa bei rafiki, itaokoa sana mazingira...


Sent from my Infinix X652 using JamiiForums mobile app
 
Kweli kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…