Jipatie Nakala yako: Uongozi wetu na Hatima ya Tanzania by Nyerere

FMES,
Najua umeshaondoka kwenye mjadala lakini kama ulifuatilia issues za Bongo hasa mwaka 1997 kila mara Mwalimu alipotembelea Watanzania alikuwa anazungumzia umuhimu wa NBC kubaki benki ya Watanzania. Ilifika wakati Mkapa alimfuata Butiama akamsihi, aache kuzungumzia suala la NBC, amwamini Mkapa. Mwalimu aliponyamaza Mkapa akageuka na kuwakabidhi Makaburu NBC. Hicho kitu kilimwuuma Mwalimu mpaka mauti ilipomfika. Inasemekana tayari Mkapa alishachukua hongo ya $300,000 kutoka kwa Makaburu. Hapa Mwalimu hana lawama hata kidogo. Kama mnaitakia Tanzania mema pambaneni na rushwa!
 

Mkuu shutuma kuwa Mkapa alichukua hongo ya dola laki 3 zinasikitisha. Lakini kama unajua madhara ya monopoly kwenye biashara unaweza kuona kuwa uamuzi wa Mkapa kuivinja NBC ulikuwa sahihi. Kusingekuwa na fair competition kwa benki nyingine, na huenda zisingetaka hata kuja kuwekeza hapa Tanzania kama NBC ingeendelea kuwa kubwa kama ilivyokuwa. Kwa upande fulani ulikuwa ni uamuzi sahihi, kwani kuvunjwa kwake hakujapunguza huduma za Benki Tanzania, japo kumepunguza umiliki wa Benki hizo Tanzania.

Matatizo yanayotokana na monopoly ya CCM kwenye siasa, yangekuwa ni hayo hayo kwenye sekta ya Benki kama NBC ingeendelea kuwa kama ilivyokuwa. Ili kuwe na fair competition kunatakiwa kuwe na level ground, na sio wengine wawe na head start.
 
Bongolander,
Hata tungeendelea kuwa na NBC benki za kigeni zingekuja tu. India waliruhusu benki za kigeni lakini wamebaki na benk yao, Bank of India. Kumbuka NBC ni benki pekee iliyokuwa na matawi katika sehemu zote za Tanzania hata vijijini, halafu kinachosikitisha zaidi ni bei tuliyoiuzia. Kaburu alitengeneza faida ya 200% katika kipindi cha miaka mitano tu. Hizo zingekuwa ni hela kwenye hazina yetu.
 
Mimi nafungua hakifunguki wajameni!!! Napata internet explorer error. Nisaidieni nifungueje au ndiyo kimeshapigwa pin tena hapa jamvini??
 
Hata mi nimejaribu kukifungua lakini haiwezekani 5 times.
Pengine mtusaidie zaidi
 
Sio baraza la mawaziri kwa ujumla wake ndio linaamua ubinafsishaji wa shirika kama NBC?

Kama mwenyekiti wa baraza la mawaziri kala hongo halafu kapigia chapuo kuuza kipande cha nchi na wajumbe wa kikao wamenyweshwa chai na chapati za Ikulu wakalala kikaoni hoja ikapita basi kosa la kuuza NBC si la Mkapa.
 

Mjadala huu umenipita kidogo!

Jasusi,
Putting it this way unafanya wengine wadhani kwamba Salim aonekane alikuwa anamuwekea Mkapa kauzibe. Mimi nadhani Salim alikuwa anatoa ushauri wake kwa Rais Mwinyi kwa nia jema kabisa kwa kuelewa tabia ya Mkapa maana wote walishakuwa kwenye international diplomatic circles. Kwa tabia na hulka ya Mkapa asingeliweza kuwa Waziri Mkuu mzuri kwa Mwinyi. Bila shaka Mkapa na mbwembwe zake angejaribu kum-outshine Rais wake hasa katika international fora.

Huenda basi ndio sababu ya Mkapa kuhakikisha anapindisha utaratibu wa kumpata mgombea wa CCM ili Salim asiweze kupita!! Alikuwa analipiza kisasi?
 

Lets be realistic. Waziri gani anayeteuliwa na Rais anaweza kupinga matakwa ya Rais aliyempa cheo? Rais akisema nataka jambo hili analiona ni jema na akatoa sababu zake zenye 'agenda' ya kificho nyuma yake, Waziri gani anaweza kumpinga? Wanachoweza kufanya ni kuchangia mawazo yao lakini mwisho wa yote hoja itapitishwa. Tunayaona hayo Bungeni, wabunge huzungumza hadi mapovu kuwatoka lakini mwisho wa siku wanasema wanapitisha hoja kwa asilimia 100, sembuse Baraza la Mawaziri lenye wateule wa mtoa hoja?
 
kitabu hakija patikana,kipo wapi,??/*&^% nashindwa kudownload hiyo link,au ndio kimefichwa tena online??
please,weka hicho kitabu katika google book,or or online server ktk pdf.

thanks
sorrry happo juuu for my *$*T%#$(%,
mzalendo
 

Kati ya maandishi yako mengi dhidi ya mwalimu katika jukwaa hili, haya uliyoandika hapa ndiyo ya maana na hitimisho sahihi. Sasa waweza kumwacha apumzike kwa amani. Tujadili walio hai sasa. Jambo la maana ni tutampataje Rais ambaye siyo mwizi wala fisadi na wala hacheki na kutumiwa nao?

Hivi mi nashaa watu kama kina Ludovick Mwesiga wanaibuka wanakoibukia sasa kumsema vibaya Mwalimu, walikuwa wapi kipindi yupo hai na hasa baada ya kung'atuka? Nadhani wanatakiwa kunyamaza. Bora Mchungaji Mtikila alikuwa akimsema akiwa hai, kwa nini hawakutumia kipindi hicho cha uhai wake baada ya kustaafu?.
 
Mkuu naona umeandika kwa jazba kidogo na sababu inaeleweka.

Mwalimu aliipenda nchi yake na aliitumikia kwa moyo wake wote - hili halina mjadala. Lolote lile aliloamua kufanya akiwa Rais na hata baada ya kustaafu alikuwa akifanya hivyo kwa mapenzi makubwa aliyokuwanayo kwa nchi na wananchi kwa ujumla, hakuwa na agenda yoyote nyingine. Yale tunayoweza kuyaona kama ni makosa kwake yeye yalifanyika kwa nia njema kabisa.

 
Boramaisha,
I wasn't able to give you senks until now because I could not sign in. Good analysis.
 
Nafikiri wadau wengi hapa mnatakiwa kutumia Voltaire Principle katika kujadiliana na FMES: "I totally disagree with what you are saying, but I'll defend to death your right of saying it".

From the arguments between FMES and the rest, it looks like it is "not allowed" to provide the other side of the story, especially when discussing Nyerere. In any discussion where people resorts to name-calling, personallity attacks, instead of the issue at hand, that is a good sign of healthy discussion.

Surely we don't want "zidumu fikra" type of discussion, where everyone says "me too", do we?
 
Mlenge,
Mbona sijaona mtu kamnyima mwenziwe nafasi na haki ya kutoa maoni yake? Tumesikia maoni ya pande zote bila upande mmoja kutaka kulazimisha mwenzake kuwa upande wake ndio sahihi, au?
 

Baada ya kusoma hii comment yako Mkuu Mlenge, nimepitia tena hii thread kutoka mwanzo nione ni wapi name-calling, personality na attacks zimeelekezwa kwa FMES lakini sikufanikiwa. Nilichoona ni watu ambao wamesimama kidete kutetea kile wanachoamini ni cha kweli dhidi ya madai ya FMES. Wengine wetu kwenye huu mjadala tu watu wazima na mengi yanayoongelewa humu tumeyashuhudia na si kusimuliwa. Hatuna uhusiano wowote wa kindugu na Mwalimu Nyerere na hivyo tunasukumwa zaidi ya historia ambayo kwa namna moja ama nyingine sisi ni sehemu yake kwa sababu tulikuwapo. Bila shaka hatutakaa kimya wala hatutaona haya kumkosoa yeyote yule atakayejaribu ama kwa makusudi au kwa malengo yoyote yale kuupindisha ukweli.

Ninachoweza kusema ni kuwa haya madai hayangeweza kutolewa wakati Mwalimu yuko hai kwa sababu moja tu - hofu ya kuwakwaza wananchi walio wengi kuliko hofu ya kumkwaza Mwalimu. Wanaoyatoa hivi sasa waliwaogopa watanzania kuliko walivyomwogopa Mwalimu kwani kwa wakati huo madaraka yote yalikuwa mikononi mwao. Amini usiamini Mkuu, kila wakati Mwinyi alipokwaa kisiki, alitafuta ushauri Butiama licha ya wabaya wa Mwalimu kumshauri tofauti. Baadaye aliposalimu amri na kuanza kuwasikiliza, kama pale ndogo ndogo zilipoanza kupigwa ili aongezewe awamu ya tatu, alijikuta akishukiwa kama mwewe anavyomshukia kifaranga. Mwalimu alijali na kuheshimu utaratibu, ni hiyo ilimsukuma hadi kumshukia hata Sam Nujoma wa Namibia alipotaka kuchezea katiba ili aendelee kubaki madarakani -Katiba haibadilishwi kama shati !
 

Hakikuchapishwa nje si kwa sababu ya kutokuwapo printing facilities nchini mwetu wakati ule, zilikuwepo. Nadhani Oxford University Printing Press wamekuwepo nchini kwa muda mrefu, pia Government Printer's wangeliweza kuombwa na kukubali kuifanya kazi hiyo kwa ajili ya Mwalimu. Kwa vyovyote vile Mwalimu angelipenda zaidi kutumia facilities za nchini badala ya nchi za nje (Zimbabwe). Kilichapishwa nje kutokana na unyeti wa suala lenyewe. Kuchapisha nje ilikuwa ni kwa ajili ya kuhakikisha kwamba habari za kitabu hicho haziwezi ku-leak.

Kama wazo la kukipiga marufuku kitabu hicho lipo basi halijatangazwa rasmi. Naamini kitabu bado kipo ofisi za Taasisi ya Mwalimu Nyerere kwa yeyote anayetaka kukinunua. Hivi sasa wamehamia kwenye jengo refu lililopo mkabala na hospitali ya Dr. Khan. Bila shaka kinaweza kuuzwa kwenye Kongamano la Kumbukumbu ya Kuzaliwa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere linaloanza kesho tarehe 12/4/2010 Chuo Kikuu Dar es Salaam, Mlimani.
 
Toleo jipya.. liko mbioni.. likiwa na commentary. Naomba anayekumbuka mlolongo wa viongozi wote wakuu wahusika wa sakata la Tanganyika na OIC... anisaidie..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…