- Mwalimu hakupenda utawala unaoheshimu sheria, ndio maana mpaka leo Tanzania hatuheshimu sheria, alipenda utaratibu hapana kiongozi akiharibu hapa alihamishiwa pengine tabia ambayo tumeirithi mpaka leo,
Utaratibu wa kuhamisha kiongozi akiharibu kumpeleka kwingine ndio kuvunja sheria, ipi? Tusisahau kwamba wakati wa awamu ya kwanza kulikuwa na wasomi wachache wenye ujuzi wa kutosha kumuwezesha Rais kufukuza huyu na kumuweka yule badala yake. Nadhani alichokuwa akikifanya Mwalimu ni kujaribu pia kumpa nafasi kiongozi aliyeharibu pale, aweze kujirekebisha mahali pengine.
alimpa Mwinyi space hapana asingemchagulia Waziri Mkuu au kumwachia katibu wake mpaka msaidizi wake wa binafsi,
,
Mie naamini kwamba Mwalimu kwa tabia yake asingeliweza katu kumchagulia Mwinyi Waziri Mkuu. Naamini alichokifanya Mwalimu ni kumshauri Mwinyi kwamba fulani anaweza kukusaidia zaidi, period. Pia yawezekana Mwinyi mwenyewe ndiye aliyemuomba Mwalimu ushauri. Kuhusu Mwinyi kuachiwa Wasaidizi wa Mwalimu pia naona yalikuwa ni makubaliano yaliyokuwa na manufaa kwa Mwinyi. Ni wazi alihitaji kupata uzoefu wa nafasi aliyonayo.
Mambo ya kuiga wafanyavyo Wamarekani ama nchi zingine zilizoendelea bila kupima na kuwa huru kujiamulia yanayotufaa, yana madhara yake. Kwanza kwa utamaduni wetu sisi Waafrika ni kitendo cha uungwana zaidi ya kitu chochote kingine kwa Rais anayeingia madarakani kuomba ama kuachiwa wasaidizi kwa muda hadi azoee.
ndege zilikuwa haziishi Butiama watu wake hasa Mkapa wakienda kushitaki, kuna siku Apiyo anashuka na ndege Musoma, huku Mkapa anaondoka na ndege nyingine, Mwinyi akapiga marufuku hizo safari ndio Mwalimu sasa akarudi Msasani, akawa na safari ya Angola anataka ndege ya Rais, somehow Ikulu wakagoma kumpa ile ndege akaishia kwenda na ndege za kawaida, kwa mara ya kwanza Mwinyi anamvuta Simba sharubu!
Mambo kama haya yanarudisha nyuma maendeleo yetu. Mwalimu alikuwa ni kiongozi wa nchi yetu, Baba wa Taifa letu. Alikuwa na haki zote za kutaka kujua kinachoendelea nchini mwake na alikuwa na uwezo wa kumuomba kiongozi yoyote aende Butiama ama Msasani kumueleza kinaganaga kinachoendelea maana alikuwa na uchungu na nchi yake. Kama ni kweli Ikulu (Wasaidizi wa Mwinyi) waligoma kumpa Mwalimu ndege walikuwa wanafanya mambo ya kitoto sana na ya kumvunjia heshima Mwalimu. Tusimsingizie Rais Mwinyi, wala si yeye ambaye alikuwa anapanga ndege iende kumchukua Mwalimu au la. Ni wazi kwamba waliofanya kitendo hicho walikuwa wapambe nuksi tu ambao nadhani walifanya hivyo kwa 'ulevi' tu wa kuwa Ikulu.
- Mwinyi hakuomba ushauri kwa Mwalimu, ndio maana kina Mkapa na Apiyo walikuwa hawaishi kwenda kuchongea Butiama, kama Mwinyi angekwua anaomba ushauri wa Mwalimu basi hiki kitabu kisingeandikwa mengine ni common sense tu. mengine
Mimi nahisi kilichotokea ni kwamba Mwinyi alikuwa anashauriwa vibaya ya viongozi/wasaidizi wake wa karibu (kwa sababu za kibinafsi tu). Bila shaka wapo waliokuwa wanamwambia Mwinyi kwamba yeye ndiye Rais sasa kwa hiyo asimsikilize Mwalimu, Mwalimu wakati wake umekwisha, bla bla.
- Kama Mkapa angekua anaomba ushauri basi asingeweza kuuza NBC kwa bei poa, sikumbuki mkutano wowote na wananchi ambako Mwalimu alilalamika kuhusu kuuzwa kwa NBC tena kwa hela ndogo sana, huku makaburu wakitaka sheria yetu ya ardhi ibadilishwe ikidhi matakwa yao, Mwalimu alikuwepo hakusema kitu, ingawa alilalama sana in private, lakini sio in the public sababu?
Power corrupts. Mkapa naye bila shaka alipata kiburi cha kudhani kwa kuwa yeye ni Rais hawezi kufuata ushauri wa Mwalimu. Watu wanaojali maslahi ya Taifa na kuliweka Taifa mbele hutafuta ushauri, huangalia kwanza maamuzi wanayofanya yatawasaidia/yatakuwa na madhara gani kwa wananchi. Labda Mkapa alijali zaidi faida atakazopata yeye kama kweli alipewa huo mulungula. Nahisi pia alikuwa anajitafutia sifa kwamba yeye naye anaweza kuiongoza nchi bila kufuata ushauri wa Mwalimu. Alijidanganya. matokeo tunayaona hadi leo.
-
Ninachojua ni kwamba Mwinyi alipoongeza bei ya Matrekta Mwalimu alilalama sana kule Mbeya, sasa inasababisha maswali mengi sana yasiyo na majibu, kwa mfano, ipi was the worst kuuza NBC kwa bei poa, au kumshambulia Amin mpaka ndani ya Uganda ili kumrudisha Obote, na Tanzania kulipa madeni ya silaha za ile vita mpaka leo, vita ambayo alishauriwa sana kwamba iishe baada ya kumtoa Amin kwenye mipaka yetu tu ili kutuokoa na madeni? Si tunalipa yale madeni mpaka ingawa Obote wala hakudumu na Uraisi uliotugharimu sana Tanzania mpaka hii leo, au?
What a comparison! Pia umechanganya issues mkuu. Sababu za kuingia ndani ya Uganda Mwalimu alizielezea wazi - kuwasaidia wananchi wa Uganda. Waganda waliomba Tanzania ifanye hivyo. Kumbuka Obote alidhulumiwa na kupokwa uongozi wa Uganda baada ya kazi aliyoifanya hadi Uganda ikawa nchi huru, so he deserved to have his country back. Kuna factors nyingi zilizosababisha Obote asimudu urais as you put it. Urais wa Obote sio uliotugharimu sana Tanzania. Kilichotugharimu ni kutetea nchi yetu dhidi ya nduli Idd Amin ambaye alianzisha vita dhidi ya Tanzania. Sidhani kwamba kuna Rais yeyote ambaye anaweza kukaa Ikulu kuendesha business as usual wakati kuna Rais kichaa anatishia usalama wa wananchi wa Tanzania!
On another issue, baadhi ya watu wamekuwa wakidai kwamba Mwalimu alikuwa anamchukia Mzee Malecela na ndio maana akaandika kitabu kumsakama. Argument hii ni hafifu. Kama kawaida yake Mwalimu alikuwa anaangalia maslahi ya taifa zaidi kuliko kitu kingine chochote. Nasikia Mzee Malecela na Mwalimu walikuwa marafiki (family friends). Kwa hiyo inadhihirisha ni kwa kiasi gani Mwalimu alikuwa anaweka maslahi ya taifa mbele kuliko kitu kingine chochote.
Kubwa zaidi, kwenye hiki controversial kitabu, Mwalimu wakati wote amezungumzia wajibu wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na si wajibu wa Mzee Malecela as a person. Angelitaka kumjadili Malecela as a person, bila shaka tungelisoma humo ule udaku usio na ukweli wowote kwamba Mzee Malecela alisilimishwa!
Respect!