Jipatie Nakala yako: Uongozi wetu na Hatima ya Tanzania by Nyerere

 
Wakuu,

Kabla ya kuteuliwa kuwa Waziri Mkuu akitokea ubalozini Uingereza, Jumanne alikuwa Mbunge wa Mtera anaeishi London, sio? Itakuaje?
 
FMES,
Butiku hakutaka kubaki Ikulu. Mwinyi alimwomba Mwalimu Butiku na Bi Wicken wabaki naye wamsaidie hasa katika ile miaka ya kwanza ya Ikulu. Bi Wicken alikataa akasema yeye utumishi wake ulikuwa kwa Mwalimu. Ikabidi Butiku akubali kubaki baada ya Mama Maria kusema kuwa Mwinyi asione kuwa sote tumemkimbia.Butiku alikaa na Mwinyi kwa miaka 2-3 hivi lakini baadaye Mwinyi akaweka Mzanzibari katika nafasi hiyo hiyo wakiwepo Private Secretary wawili.
Mwalimu alipoona hivyo akaomba Butiku apelekwe kuwa mkuu wa mkoa Mara ili amsaidie shughuli zake pale Musoma.
 
 

Mkuu Jasusi, heshima mbele. Mwalimu alikuwa mtu aliyejali sana utaratibu na hasa katika utendaji. Baada ya kung'atuka alijitahidi kwa uwezo wake kumpa Mwinyi breathing space, yaani kutomwingilia katika utendaji. Pamoja na msimamo huo, hii haikumwondolea haki kama Mtanzania kutoa maoni yake kwa maswala ya kitaifa kama azimio la Zanzibar. Alijitahidi kukaa kando kwa miaka ya mwanzoni lakini siku zilivyoendelea na mambo ya ajabu ajabu kufumka alijikuta hana jinsi na kukaa kimya alijua kungemsuta. Ni Mwinyi mwenyewe aliyeomba ushauri kwa Mwalimu mara kwa mara hasa pale ambapo alikuta anakwama. Hivyo hivyo na kwa Mkapa, Mwalimu hakuingilia hadi pale alipoanza kutoridhishwa na rasilimali za taifa zilipoanza kutapanywa ovyo. Njia aliyotumia sana ni kuwatonya kwanza na kama hilo halikufaulu aliwaita waandishi wa habari.
 

- Mkuu Jasusi, with all due respect, kama nilivyosema huko nyuma wewe ninakuaminia sana, now naomba kuuliza Obama kumuomba Karl Rove abaki amsaidie? Ungesema alimuomba Apiyo nisingepata wasi wasi kwamba ni kweli, lakini Rais mpya amuombe personal assistant wa anayeondoka, on a serious note unajua hii inaweza kwenda kwenye Guiness Record book kwa sababu haijawahi kutokea duniani, labda sisi Tanzania ndio tunakwua wa kwanza, kwa sababu Mwinyi alipokuwa Rais wa Zanzibar si alikuwa na msaidizi wake wa binafsi na alikuwa enough experience na Urais, I mean haijakaa sawa hii! Tumeona viongozi wadogo wakihama na wasaidizi wao, sijawahi kusikia wakiomba wa anayeondoka abaki!

- Halafu unaona ndugu yangu sasa unavyokubali kwamba Demokrasia yetu ni Mungu nisaidie, Mama Maria amesema Butiku abaki maana Mwinyi asijeona tumemkimbia is this how you govern a nation, Mwalimu alimuomba awe RC ili amasaidie shuguli zake binafsi na wakati tunayo bajeti kubwa sana kwa marais wastaafu na wasaidizi, I mean thnks for this info lakini zimeishia ksuema mengi zaidi kuhusu uongozi wetu Tanzania na tulikotokea,

Respect.


FMEs!
 
 
 
Jamani mnyonge mnyongeni, lakini haki yake mpeni. Nyerere alikuwa kiongozi wa tofauti kabisa na viongozi wetu wa leo ! Nyerere asingekubali hata siku moja kuwa mbunge katika bunge lililogubikwa na ufisadi, yeye alijali utaifa zaidi kuliko chama. Katika moja ya hotuba zake alizungumza kwa uchungu kuhusu benki ya NBC, na alitoa sababu za msingi kwa nini isiuzwe !

Tofauti na viongozi wengine wa leo ambao wanaogopa kumsema wakina Kikwete, Mwalimu alikuwa na audacity kuwaambia watu kile wanachotakiwa kusikia na sio kile tuu wanachotaka kusikia. Mwalimu ameandika vitabu vingi sana katika maisha yake, kwa nini hawa viongozi wengine wasiandike vyao ? Tupate hadithi ya upande wa pili .

Kumlaumu Nyerere kutokana na vile vinavyooendelea leo itakuwa ni kushindwa kuona mbali. Mwalimu alisema wazi pale Mbeya ni Rais wa aina gani tunaomhitaji, na watanzania wategemee nini kutoka kwake . Sasa kama Mzazi alifanya kazi yake , mtoto akaamua kudiverge from his/her parent directives: how are you then going to blame the parent?
 

- Ni kweli kabisa mkuu Mwalimu was the greatest, lakini usisahau kwamba alibariki Salmin kupora Urais kule visiwani, alikuwa ni bin-adam mwenye mengi mazuri na mapungufu, ambayo tunayalipia mpaka leo.

- Lakini haibadili ukweli kwamba hakwua mwizi wala fisadi, hilo hatukatai.

Respect.


FMEs!
 


With all due respect, sielewi kwa nini unapoteza muda mwingi kutetea watu ambao wanaweza kujitetea wenyewe - hawa watu bado wako hai . Kwa nini hawaandiki vitabu vyao, ili watu wajifunze kutoka kwenye mafanikio na kushindwa kwao ?
 

Kama tukiambiwa tuweke kwenye mizani hayo mengi mazuri na upande mwingine hayo yanayoitwa mapungufu ni upande gani utaelemea? Hakuna namna ya kukataa jinsi gani Mwalimu alivyojitolea kusimamisha taifa hili tulilonalo leo.Misingi iliwekwa na hatuwezi kumlaumu tu kwa kuwa misingi ile haikupelekea kusimamisha nyumba Imara, wajenzi walikua ni wengi na wengine walikua kama wale mafundi wa mtaani waibao cement na kupelekea nyumba kumomonyoka miezi michache tu baada ya ujenzi.
 
FMES,
Hii comparison ya Obama na Karl Rove haina mshiko. Kumbuka Mwinyi ni CCM na Mwalimu alikuwa CCM. Afadhali ungetoa mfano wa Al Gore kama angeshinda amwombe msaidizi wa Bill Clinton abaki White House kuendelea kumsaidia wakati wa transition, jambo ambalo hufanyika wakati wote mgombea rais wa chama kimoja anaposhinda na kumrithi mwenzake kutoka chama hicho hicho hapa Marekani.. Kumbuka Mwinyi hakuwa na "watu wake" mainland, na mimi nadhani kweli pale mwanzo alihitaji msaada wa watu watakaosaidia kum guide through the intricacies of the State House. Butiku hakuwa personal secretary wa Mwalimu alikuwa Private Secretary, a much higher title than personal secretary au assistance na alikuwa na Mwalimu Ikulu kuanzia mwaka 1965. Anyway, nilichokisema katika bandiko langu nakijua kuwa fact.
 
FMES,
Hii ya Mama Maria haina uhusiano wowote na demokrasia yetu. Mwalimu, nilivyomjua, hakutaka kumlazimisha Butiku abaki Ikulu. Katika mazungumzo yao pale Msasani Mama Maria alishauri tu siyo kwamba alikuwa anafanya maamuzi ya
Ikulu. Hiki kilikuwa kikao cha kifamilia, Mwalimu alishastaafu, na wala si policy session. Mwalimu aliomba Butiku "amsaidie" pale Mara baada ya kuona kuwa Mwinyi ana Private Secretraries wawili pale Ikulu. It was Mwalimu's way of getting Butiku out of the State House kwani hatujawahi kuwa na Private Secretaries wawili pale.Ni kama Mwalimu alikuwa anamwambia Mwinyi, nirudishie mtu wangu naona sasa humhitaji.
 

- Mkuu naona umeongeza maneno over your original post, ni kwamba kama kweli Mwalimu alikuwa na hiyo tabia unayoisema, basi angekemea kuuzwa kwa NBC, tabia hiyo ya Mwalimu ilikuwa siku zote inaangalia sura kwanza, ndio maana alimbariki Salmin kuiba urais, can you imagine Malecela ndiye angeiba urais, ingekuwaje?

- Viongozi wengine wasingeweza kuandika vitabu kuhusu tabia za Mwalimu isingewezekana it was simply impossible you know that, tumjadili Mwalimu kama bin-adam na sio kama Mungu, na tupeni nafasi na wengine tu-present the otherside kuliko kutaka kutulazimisha wote tuimbe wimbo mmoja, wa-Tanzania tujifunze kutengniasha mapenzi yetu wka Mwalimu na Mapnezi kwa taifa, inatakiwa kuwa vitu viwili tofauti.

Respect.


FMEs!
 
With all due respect, sielewi kwa nini unapoteza muda mwingi kutetea watu ambao wanaweza kujitetea wenyewe - hawa watu bado wako hai . Kwa nini hawaandiki vitabu vyao, ili watu wajifunze kutoka kwenye mafanikio na kushindwa kwao ?

- Vipi mkuu mbona kwenye hii htread umekua ukihangaika sana, hapa ni JF where we dare, demokrasia at work yaani kuangalia ishu pande zote mbili, hakuna tatizo mkuu tunajaribu kujadili kitabu na author wake Mwalimu, that is all! kama hampendi basi tutakaa pembeni muandike mnaofanana, au?

FMEs!
.
 

- Mkuu with all due respect, ni suala la kuchagua moja either Mwalimu alikwua na mapungufu au alikua hana, kumbe yeye akwia kiongozi wajenzi walikuwa wengi, lakini Malecela akwia Waziri Mkuu mjenzi aliwkau mmoja tu mpaka kuandikiwa kitabu chote hiki! Sawa sawa mkuu umesikika.

Respect.


FMEs!
 

- Mkuu Jausi, kisichokuwa na mshiko ni kushauri kwamba Private Secretary wa Rais mmoja kubaki kuendelea kuwa wa Rais mpya, it absolutely impossible na haijawahi kutokea ndio maana ninasema Tanzania tunahitaji kuingia kwenye Guiness Book for this act, kwa sababu sikuona Kumchaya akibaki kuwa Private Secretary wa Kikwete na hawa wote ni wa CCM, ila umesikika sana mkuu.

Respect.


FMEs!
 

- Haya jamani naomba ku-retire hapa, nafikiri nimejitahidi sana ku-present upande wa pili wa hiki kitabu, sioni jpya ila yale yale ya kawaida ya kumkingia Mwalimu kua sio bin-adam wa kawaida, ninawaruhusu wakuu wote mnaokubaliana kuendelea.

- Sitairudia tena hii thread.

Thanks.


FMEs!
 

Karibu wote tunafahamu kuwa Mwamlimu was human being, he was not a saint. That means he had weaknesses just like you and i. Lakini ukweli ni kwamba he believed in what he was doing, stood by it and strongly defended it. Completely the opposite of what we see today. Ubabaishaji na porojo nyingi kuliko utendaji.

Lakini ukianza kuwajudge kina Malecela kwa mujibu wa kitabu alichoandika Nyerere, am not sure kama itakuwa fair. Are we sure that Malecela was believing in Ujamaa na kujitegemea? or he was justing singing the song of the day? What if Malecela writes a book today, what will he say about Mwalimu and the reason why we as a country are corrupt and visionless. Or can we just ask him to publicly give his honest opinion of what is currently going on in Tanzania, tuone kama ni mnafiki au vipi. Tumeona madongo mengi anatupiwa na amekuwa mstaarabu sana kuwa low key, tofauti na wengine ambao wanatumia media kurusha jibes za ajabuajabu.

On the other side if he says mwalimu was wrong am sure i will be first to criticize him, simply because what mwalimu was thinking at that time was right at that epoch. Na sikubaliani na mwalimu kum-ridicule Malecela kwa "weakness" iliyoonekana during the serikali ya Tanganyika. Kulikuwa na sababu za msingi ambazo mpaka leo bado hazijawa addressed, PM yoyote kwa wakati ule kama si dikteta angesikiliza wanachotaka wabunge. Mengi aliyofanya Malecela wakati ule ni kutokana na hali ya wakati ule. By the way yeye hakuwa rais na wala hakuwa spika wa bunge.

Kuna watu wengi walikuwa wanafiki sana wakati wa mwalimu na wakaendelea hivyo wakati wa Mwinyi simple because waliokuwa wanaona aibu kuwa mwalimu atawalipua. At least MZee Malecela has remained himself, as far as i know. Ona Mzee Kingunge alifikia hata hatua ya kumkataa Mungu na kujiita mkomunisti, he "stood" by rules za chama, laws of the land, and was "discplined" man. Look at him today, after Mwalimu's death he has shown his true colours, anatetea ufisadi waziwazi, aliitisha hata press conference kusema kina Slaa waongo, na ukweli umeonekana kuwa yeye ndiye alikuwa anaongopa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…