Plot4Sale Jipatie Shamba Vigwaza la ekari saba na nusu kwa Milioni 20

Plot4Sale Jipatie Shamba Vigwaza la ekari saba na nusu kwa Milioni 20

Asante sana mkuu kwa taarifa hii. Vipi kilimo cha alizeti hapo kinafaa?
Karibu sana mkuu. Ile ardhi ukiamua kulima alizeti au hata ufuta utalima na utavuna vizuri tu. Njoo ujionee mwenyewe mkuu
 
Ilo Apo liko mjini mjini,sehemu panajengeka,ukiitaji la kilimo ,lipo ,laki tatu kwa eka
Anaweza kulima na kujenga pia mkuu. Sasa akichukua eka saba zote atazitumia kujenga tu? Ukaribu wa shamba na mjini maana yake hata kusimamia shamba gharama ni ndogo maana hatapata tabu ya usafiri. Pale shambani kwangu ukitokea vigwaza mjini mpaka shambani pikipiki ni elfu 1500 hadi 2000. Hata unaweza kwenda shambani kwa mguu ukishuka kwenye daladala
 
Asante sana mkuu kwa taarifa hii. Vipi kilimo cha alizeti hapo kinafaa?
Pale unaweza kulima mihogo, alizeti, ufuta, mbaazi, viazi nk. Upande wa kufuga ndio babkubwa kabisa na uzuri ukitaka kupeleka mifugo yako kama mbuzi au ng'ombe mnadani hauingii gharama yoyote zaidi ya kuswaga mifugo yako mpaka mnadani maana mnada uko hapohapo Vigwaza. Unajaza mfuko wako unarudi mdogomdogo na furaha zako tele. Karibu ujipatie eneo mkuu..kumbuka mi ni mmiliki na siyo dalali hivyo ukija tutaelewana tu
 
Asante sana kwa ufafanuzi huu mkuu. Nitakucheki ngoja nijipange
 
Karibuni sana naendelea kuwakumbusha wale wanaohitaji shamba tuwasiliane tufanye hii biashara kwa bei nafuu kabisa.
 
Haya sasa weekend imewadia. Karibuni mje mjichukulie shamba kwa bei nafuu vigwaza. Shamba eka saba na nusu kwa milioni 20 tu. Ukitaka eka moja unapata pia. Karibuni sana
 
Karibuni mjipatie Shamba la eka saba na nusu kwa bei nafuu ya shilingi milioni 20. Shamba liko umbali wa kilomita tatu na nusu kutoka barabara ya lami ya Dar Morogoro. Shamba linafaa kwa ufugaji wa kuku, mbuzi, bata na mifugo mingine.

Huduma ya maji ya DAWASA imesogezwa karibu na shamba umbali wa mita 400. Shamba liko jirani na Chuo cha Mainjinia wa Ndege hivyo kwa baadae ni eneo zuri kwa kuwekeza katika ujenzi wa hosteli. Baadhi ya majirani wameshaanza ujenzi wa nyumba za kuishi na mabanda ya ufugaji. Karibuni sana tufanye biashara
 
Naendelea kuwakumbusha wanaJF karibuni mjipatie ardhi kwa bei nafuu. Unaweza kupata eka moja au zaidi. Ni wewe tu na kiasi ulichonacho hatuwezi kushindwana
 
Ukitaka eka moja au shamba lote au zaidi ya eka moja mimi nakukatia tu unaanza kufanya mambo yako. Wekeza sasa kwenye ardhi kwa bei nafuu.
 
Ukihitaji nifuate inbox tuyajenge nitakupatia punguzo la bei lengo tu ujipatie kipande cha ardhi kwa ajili ya maendeleo yako.
 
Naendelea kuwakumbusha wanaJF karibuni mjipatie ardhi kwa bei nafuu. Unaweza kupata eka moja au zaidi. Ni wewe tu na kiasi ulichonacho hatuwezi kushindwana
Mkuu nikiwa vizuri nitakuona japo nipate eka moja. Majuzi nimepita hapo Vigwaza nikiwa nimetoka mkoani nikakumbuka tangazo lako hili la shamba.
 
Mkuu nikiwa vizuri nitakuona japo nipate eka moja. Majuzi nimepita hapo Vigwaza nikiwa nimetoka mkoani nikakumbuka tangazo lako hili la shamba.
Karibu sana kiongozi. Nakufata inbox tuanze kujadiliana
 
Back
Top Bottom