Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,761
- 216,011
Kama kichwa cha habari kinavyoeleza z, unaweza kumpata jirani anafuga, inawezekana ikawa kuku, ng’ombe, bata nk.
Mifugo inatoa harufu inayoambatana na inzi, harufu inaweza kukukatisha hamu ya kula na unashindwa kupunga upepo nje ya nyumba yako kwa kero ya inzi pamoja na harufu.
Unapolalamika jirani hakuelewi kwakua ng’ombe wanampatia maziwa na yeye ndiye muuzaji wa maziwa mtaa..
Ukizingatia viwanja vyetu vya uswahilini hivi vya 20x20. Unawaza ningejua nitakutana na haya nisingenunua kiwanja hapa.
Kuku kwanza jogoo anakuamsha ile saa ya usingizi mzito na wala huna safari, kama unashighuli za kufanya unaweza kusema hii ndiyo alarm yako asubuhi.
Kuna jirani alikua anapika mama ntilie, mchana moshi wote unaingia sebuleni kwangu. Nilipomwbia masikitiko yangu alianza kuniimbia nyimbo za vijembe. Ilibidi nipeleke malalamiko yangu kwa kiongozi wa mtaa. Baada ya kupata ujumbe kutoka serikali ya mtaa, amehamisha sehemu ya kupikia lakini sikuhizi hatusalimiani. Nimepata adui mpya.