Jirani anaweza kukufanya uchukie nyumba yako

Jirani anaweza kukufanya uchukie nyumba yako

Jaribu kumnunua

Mimi mjomba Wangu anasali swala tano Ila jirani anauza pombe za kienyeji na kupiga kelele na walevi

Alichofanya alimnunua akamtoa .


Alikuwa Ana eneo dogo Sana miguu 20 Kwa 20 Ila alimpa million 20 na Nyumba yake ya Vyumba wiwili.
Kama uwezo unaruhusu unafanya hivyo. Kuvumilia kero ni ngumu sana.
 
Kama Mambo Mengi katika nchi yapo holela, barabara zimegeuzwa masoko, hakuna Njia za waenda Kwa miguu, full fujo!! Sasa unahisi huyo Jirani ni mwerevu kuliko uongozi wa tunayoyaona mabarabarani, haiwezekani ustaarabu huanza na uongozi kuja kwenye ngazi ya familia. Jua uongozi wa kiserekali ni taratibu na Sheria na Familia ni hekima na ustaarabu!! Nakushauri wewe endelea kujenga upendo na Jirani Yako, acha Visa!! Huko mabarabarani nako ni hovyo Kabisa
 
Kama kichwa cha habari kinavyoeleza z, unaweza kumpata jirani anafuga, inawezekana ikawa kuku, ng’ombe, bata nk.

Mifugo inatoa harufu inayoambatana na inzi, harufu inaweza kukukatisha hamu ya kula na unashindwa kupunga upepo nje ya nyumba yako kwa kero ya inzi pamoja na harufu.

Unapolalamika jirani hakuelewi kwakua ng’ombe wanampatia maziwa na yeye ndiye muuzaji wa maziwa mtaa..

Ukizingatia viwanja vyetu vya uswahilini hivi vya 20x20. Unawaza ningejua nitakutana na haya nisingenunua kiwanja hapa.

Kuku kwanza jogoo anakuamsha ile saa ya usingizi mzito na wala huna safari, kama unashighuli za kufanya unaweza kusema hii ndiyo alarm yako asubuhi.

Kuna jirani alikua anapika mama ntilie, mchana moshi wote unaingia sebuleni kwangu. Nilipomambia masikitiko yangu alianza kuniimbia nyimbo za vijembe. Ilibidi nipeleke malalamiko yangu kwa kiongozi wa mtaa. Baada ya kupata ujumbe kutoka serikali ya mtaa, amehamisha sehemu ya kupikia lakini sikuhizi hatusalimiani. Nimepata adui mpya.
Jirani ananiambia be humble
Be humble!!?? That's ridiculous am serious notorious baba hakutuachia mtaji wala urithi sasa huyo ni baba gani?
Humble au mtemi?
 
Ha ha ha haaaa hivi na tulio kwenye nyumba za kupanga nao tuna majirani? Any way mimi mpangaji mwenzangu alikuwa kero kwangu kama ndio jiran basi ndiye huyo huyo.
Picha linaanza ana miaka 31 na ana watoto watano. Kinachotokea huduma muhim kwa familia hatoi chai ikipikwa sukari inawekwa kiasi kwamba chai ikiwa inaingia tumboni ndio unajua kuwa ilikuwa na sukari.
Uji ukikorogwa ni marufuk kuweka sukari anatia chumvi.
Samaki akinunua bichwa lote lake pekee yake watoto watajua wenyewe na kwa kuwa ni msabato anapitia humo humo kuwanyima familia baadhi ya huduma.
Shughuli kwa majirani watot wake wte wanajua ratiba ya majirani kula ha ha haaa ukitenga tu timu ya watoto wanne hao hapo kasoro mkubwa tu ndio anajitambia maana mkubwa yupo drs la pili.
Kumbuka watoto ni malaika maana huwezi wanyima chakula ila kero na lawama zinarudi kwa mzazi hasa wa kiume ni Nyau saana yule mwamba
 
Back
Top Bottom