Jirani nimemchoka na siwezi muambia

Jirani nimemchoka na siwezi muambia

Mwachiluwi

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2022
Posts
25,258
Reaction score
48,589
Habarini

Mimi bhana naishi sehemu fulani hapa Dar sio ushuani nakaa ubalozi wa Marekani pale

Sasa jirani yangu ni kero nikipika kuku anaomba, akisikia napika chochote kile anaomba

Leo nimetoka zangu mihangaiko nimenunua nyama choma na kitimoto nikamwambia muuzaji changanya si najua ni muislam hatumii

Ebwana kasikia nafungua mlango tu kaja kaka nani umebeba nini chakula na njaa hapa naomba nionje kidogo maana nimebandika maji ya ugali sasaiv nikamjibu ni kitimoto

Akasema kwa sauti napenda balaa ikabidi nimwambie njoo uchukue tukawa tunakula kwa pamoja nikajua atanibakishia mpaka mimi nikaona jau nikamwambia kamalize basi kwako.

Sipendi tabia ya kuombwa na kumwambia naogopa yaani nahisi atajisikia vibaya sijui nifanyeje
 
Ubalozi wa Marekani hapo Morocco nyumba gani hapa. Hapa maeneo ya Driven in ama huku Kawe Ukwamani?
 
Mzee jau atanichukia
Afie mbali kama anataka kula achangie japo kidogo. We umekuja na ktm yako tena ya mtu mmoja anaitafuna kama yake wakat hayupo kwenye hesabu. Ukwel siku zote unauma
 
Back
Top Bottom