Ila kanda ya ziwa inaongoza kwa wanaume kupiga wanawake zao....kuna sehemu nilihamia mzee ndani ya wiki wapangaji watatu wamewapiga wake zao na kuwafukuza kabisa....ila baada ya muda wakarudiana...
Kuna mmoja alikuwa ana mchapa mke wake kimya kimya,mwanamke akishindwa kuvumilia kichapo akaanza kulia niache niende kwetu,jamaa alifunga mlango kwa ndani anaendelea kumpa vitasa mkewe,sisi tunasikilizia tu mtifuano hahaaahaa ni raha kama mtu una bifu naye ukasikia anakula vitasa.
Basi mpangaji wa jirani na jamaa anayempiga mke wake akaamua kuingilia ugomvi,akamwambia jamaa anayetoa displine, oya tokeni mkapiganie nje msije kuuwana humu ndani tukapata kesi,mtoa vitasa anaendelendelea kutoa vitasa ....mke analia tu,mwisho wake jirani akatoka kwake akaenda mlangoni kwa jamaa akagonga mpango kwa nguvu...jamaa wa vitasa akapoa akafungua mlango akamwambia jirani yake haya chukua huyo mwanamka kama unataka ,walijibizana pale wakataka kupigana kabisa...mke akaondoka usiku ule ilikuwa kama saa sita,jamaa wakabaki wanarushiana maneno....
Ujumbe.
Wanaume tujizuie kuwapiga wake zetu sio ustaarabu hasa kwenye maisha ya nyumba za kupanga inamdhalilisha sana mwanamke,kama unaishi kwako afadhali kama hauwezi vumilia mchape fimbo kama mwanao umpendaye wanawake ni dhaifu sana inabidi kuishi nao huku tukielewa udhaifu wao....kuna wazazi wetu wametulea tumeona katika ndoa zao hawajawahi kupigana zaidi ya miaka 10,20,-30 hivyo kwenye ndoa uvumilivu ndio silaha yako mwanaume.