Jirani yangu kapoteza ufahamu gafla chooni ila ni mzima

Jirani yangu kapoteza ufahamu gafla chooni ila ni mzima

Tajiri Tanzanite

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2016
Posts
2,536
Reaction score
4,621
Hapo vip!!

Binafsi nimeshindwa kumpa ushauri kuhusiana na tatizo hilo.

Kuna jirani yangu leo amekuja kunieleza jambo la ajabu sana nikashangaa

Hivi anadai ameingia chooni kukojoa usiku alivyomaliza mkoja gafla akapatwa na kizunguzungu na kupoteza ufahamu gafla akajikuta amepiga magoti akiwa anataka kutoka chooni.

Akaamka akatoka chooni ila akawaa ameshtuka sana na ajaumia wala hana maumivu yeyote na anaendelea na kazi zake kama kawaida.

Ananiomba ushauri juu ya hilo jambo kwasababu anakosa amani na anataka kuchukua hatua zaidi..
karibuni wataaam kwa ushauri.
 
Anatumia dawa za pressure? Kama anatumia hilo linaweza kutokea na ni hatari, wanashauriwa kukojoa wamekaa. Na hata kama hatumii hiyo huwa inatokea, inaitwa Postural Hypotension. Yaani pressure ya damu inashuka mtu anaposimama, hasa ghafla sababu damu hukimbilia miguuni. Hilo linafanya damu kwenye ubongo iwe ndogo na kuleta kizunguzungu.

Bahati mbaya watu wengi huwaza majini, mapepo na uchawi.
 
Anatumia dawa za pressure? Kama anatumia hiko linatokea na ni hatari, wanashauriwa kukojoa wamekaa. Na hata kama hatumii hiyo inatokea, inaitwa Postural Hypotension. Yaani pressure ya damu inashuka mtu anaposimama, hasa ghafla sababu damu hukimbilia miguuni. Hilo linafanya damu kwenye ubongo iwe ndogo na kuleta kizunguzungu.

Bahati mbaya watu wengi huwaza majini, mapepo na uchawi.
Orthostatic hypotension hutokea mara nyingi soon after kusimama, sasa kweli mpaka amefika chooni akafanya yaliyompeleka more than 30 sec. Sina uhakika kama inaapply hapo hii.
 
Anatumia dawa za pressure? Kama anatumia hiko linatokea na ni hatari, wanashauriwa kukojoa wamekaa. Na hata kama hatumii hiyo inatokea, inaitwa Postural Hypotension. Yaani pressure ya damu inashuka mtu anaposimama, hasa ghafla sababu damu hukimbilia miguuni. Hilo linafanya damu kwenye ubongo iwe ndogo na kuleta kizunguzungu.

Bahati mbaya watu wengi huwaza majini, mapepo na uchawi.
Amesema hana pressure,ugonjwa wa moyo wala kiuskari
 
Naomba ufafanuzi zaidi umeniweka kwenye bracket...
Tayari alishaandaliwa maradhi kwa ulimwengu wa roho wa giza na wakapanga sehemu kuwa ni chooni

Hapo yeye kuja kwenda chooni na kuanguka ilishapangwa...

Mambo ya ulimwengu wa roho yana process hupangwa na kutokea baadae...

Vivo hivyo maisha tunayoishi yanaanzia rohoni alafu ndo yanatokea...

Hivyo ni muhimu kuomba kwa YESU KRISTO kupata macho ya Rohoni na nguvu za rohoni na maana utayajua mambo yajayo...hata maadui na kuwashinda..

Pia kukumbuka ndoto unazoota maana ni moja ya macho ya kuona kama Yusufu aliota ndoto ikaja kutokea Mwanzo 37: 5-11
 
Ila kuna baadhi ya watu wanasema huwa mtu akianguka chooni akipona ni bahati sana wengi wanapata stroke,kupooza upande,kupinda mdomo au kufa kabisa ila haya yanampata pale pale chooni..sijajua kwa huyu aliyenusurika hayo.
Nasikiaga kwamba kule chooni hua kuna viumbe visivyoonekana hua vinaishi ukifanya tofauti na inavyotakiwa kufanya ukiwa chooni ndio hivyo unajikuta umekalishwa kikao

Huyo mhusika aseme ukweli alifanya nini huko chooni hadi wakulungwa wakamuweka mtu kati

Nilisikia tu kwenye kijiwe chetu cha kahawa sio kijiwe cha chai

Nitakuja tena..
 
Nasikiaga kwamba kule chooni hua kuna viumbe visivyoonekana hua vinaishi ukifanya tofauti na inavyotakiwa kufanya ukiwa chooni ndio hivyo unajikuta umekalishwa kikao

Huyo mhusika aseme ukweli alifanya nini huko chooni hadi wakulungwa wakamuweka mtu kati

Nilisia tu kwenye kijiwe chetu cha kahawa sio kijiwe cha chai

Nitakuja tena..
Amesema alivyomaliza kukojoa akatema mate pale chooni ile anatoka akajikuta amepata kizunguzungu nakupoteza ufahamu gafla akajikuta amepiga magoti karibu na mlango.
 
Mazingira niliyokaa watu wengi wamepata vilema hata kupooza mikono yupo jamaa aliangua chooni kiutani utani na vile mlevi tukachukulia poa ila alipooza mkono alioangukia wamezunguka hospital mpaka basi mpaka kashazoea ni miaka karibia 15 iliyopita na anaishi kama kawa ila mkono umepooza..
 
Back
Top Bottom