Jirani yangu kapoteza ufahamu gafla chooni ila ni mzima

Ni hatari
 
Alichukua muda gani kuanza kupooza au ni siku ile ile..
 
Alichukua muda gani kuanza kupooza au ni siku ile ile..
Alipata maumivu siku ya pili wakaanza kumchua na ile dawa kipind kile kama sijakosea ni "salimia" inaitwa basi mpaka mkono ukaanza kuzidi duh akaepelekwa hospital kama utani ni wiki zile zile tu jamaa mkono umepooza mpaka leo Yani kama umeparalyze sema wa kushoto anapiga kazi zake kama kawa.
 
Mwambie aache wenge alikuwa anaota huyo, hajaenda toi wala nini
 
Ila kuna baadhi ya watu wanasema huwa mtu akianguka chooni akipona ni bahati sana wengi wanapata stroke,kupooza upande,kupinda mdomo au kufa kabisa ila haya yanampata pale pale chooni..sijajua kwa huyu aliyenusurika hayo.
Inategemea mkuu,

Mara nyingi sana watu wanadondoka chooni/bafuni kwa sababu ya pressure ya ghafla.

Inashauriwa mtu anapoenda kuoga asianze kwa kujimwagia maji kichwani.

Uwezekano wa mtu kupata madhara makubwa chooni ni kutokana na ufinyu wa eneo. Ni rahisi sana wakati wa kudondoka chooni kugonga kichwa ukutani hivyo kupelekea madhara makubwa kwenye mwili na maisha ya binadamu.

*Hayo mengine ya shirki sina uelewa nayo sana.
 
Baba wa rafiki yangu alianguka chooni juzijuzi na kufa.
 
Baba wa rafiki yangu alianguka chooni juzijuzi na kufa.
😥😥😥Hatar sana ...huwaga mwaka fulani nilikuwa naishi Tanga nilisikia wansema ivi eti mtu akiangua chooni kama amepata jeraha au kutumia basi Ile sehemu ya jeraha ipakwe uchafu wa chooni ndo dawa.. sasa nikawa najiuliza uchafu upi huo wa chooni?
 
Watu wanaweza kuwa na maoni mazuri tu ila wakristu na wasomi wa kizungu washazingua.muafrika wakipata elimu kidogo huwa mthani.ALISIKIKA MEMBA MMOJA WA JF MWENYE BUSARA.
 
Akili za kuambiwa changanya na za-kwako.

Kuna jamaa yangu alidondoka chooni tukamwahisha hospitali akiwa mahututi.

Hospitali baada ya kumchunguza kichwa waligundua damu imeanza kuvuja ndani ya kichwa, na angechelewa angefariki.

Cha kushukuru ni kwamba mpaka leo ni mzima wa afya na anaendelea na shughuli zake vyema baada ya upasuaji.

Je, angepaka uchafu wa chooni angepona?
 
Kazia kabisa "HALI HIYO IPO KARIBU SANA NA KIFO ”
 
Kama kiafya yupo sawa na hata hospitalini hajakutwa na tatizo basi ajue mwili wake ni nyumba ya mgeni mwingine anaishi humo ndani au kafanyiwa kibaya
 
Ila hii Dunia tunayopita inakatisha tamaa ..inamambo mengi ya kutisha mno na vita ni kubwa kwa mwanadamu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…