Jirani yangu kapoteza ufahamu gafla chooni ila ni mzima

Ninyi mnao jifanya hamuamini kama ushirikina upo ndio huwa washirikina wenyewe , haya mambo yalisha kuwepo tangu enzi za mitume na manabii
Mambo mengi sana yaliaminiwa ni ya kishirikina lakini sayansi imegundua sivyo, lakini washirikina mmezidi kukomaa na imani zenu. Wengi bado wanaamini radi inatumwa na watu na ikipiga sehenu huwa inataga mayai😀
 
Kuna ile ya nguvu za Giza ,ila kama kawaida kuteleza Haina noma mi mara kibao ile kukanyaga sabuni😂😂😂nikapiga kichwa kweny koki
 
Kuna ile ya nguvu za Giza ,ila kama kawaida kuteleza Haina noma mi mara kibao ile kukanyaga sabuni😂😂😂nikapiga kichwa kweny koki
Possibilities ni nyingi sana, na wala siwezi kukataa uwezekano wa yoyote.

Lakini kwa case ya hospitali kutumia shirki ndo nitolee hivyo, au kwa issue ya shirki kutumia hospitali ndo balaa tena.

Jinsi ya kuvi-balance ndo changamoto ilipo my friend- kufanya maamuzi sahihi wakati sahihi.

Kama hizo possibility za kudondoka bafuni zinakutokea mara kwa mara, best chukua tahadhari mapema usikute ndo majaribio ya kufa au balaa.

Wahenga walisema "mzaa mzaa hutumbua usaha"

Kikubwa kuna malapa maalumu kwa ajili ya kutembelea kwenye tiles na sehemu za utelezi, tumia hizo ili kuwa salama, bado tunakuhitaji.

Binafsi mwaka huu niliteleza kwenye tiles kama siyo Mungu tungekuwa tunaongelea habari nyengine. Niliteleza, kabla ya kufika chini akili kama ikagoma, ile nakaribia chini nikakunja shingo nisigonge ukutani, hivyo nikapiga mikono yote chini kwa nguvu, kiasi kwamba maumivu yalichukua mda sana. Ningegonga kichwa sina mashaka ningekula udongo kabisa moja kwa moja.

Haya maisha tujifunze tu kuwa humble, muda wowote safari.
 
Ebwana kama Yuko dar au mkoani mwambie aende eagt city centre Kwa pastor Katunzi aende Tu Kwa ibada at aki Google atapata kanisa lilipo njia ya mbagala nakwambia hapo atapata uponyaji bure kanisa Kwa Jina la Yesu niamini nimempeleka wengi mapepo yamekimbia afanye hima wasije muwahi msaidie kwenda kanisani kama unampenda hapa Nina uhakika Napo...
 
mwambie aend hospital hakun jamb la ajab hapo ila km anatak namba ya mtaalamu me nnayo 😁😁😁🤔
 
Amesema alivyomaliza kukojoa akatema mate pale chooni ile anatoka akajikuta amepata kizunguzungu nakupoteza ufahamu gafla akajikuta amepiga magoti karibu na mlango.
Labda aliwatemea wenyewe humo chooni walikua wamepozi akawakasirisha wakampa adhabu kwanza ya kupiga magoti adhabu nyingine wanajifikiria.
 
Iliwahi kunitokea pia. Mimi nilianguka nikapigiza kichwa though sikuanguka vibaya..

Mke wangu alinisikia nikikoroma, akaja kanikuta chini.

Nilikua naona kama naota kama kizungu zungu hivi..


Ilikua immediately baada ya haja ndogo...


Nilienda hospital moja kubwa kuchunguzwa, nikaanza na neurosurgeon kucheck mifumo ya fahamu...

Nilifanya vipimo, ECG, MRI na vingine sivifahamu. Lakini hawakuona shida yoyote... nikafanya na vipimo vya kawaida hawakuona shida yoyote.

Wakashauri nikafanyiwe kipimo cha moyo kwa kufatilia mapigo ya moyo kwa masaa 24 (kulala hapo hapo hospital)... kipimo hiki sikukifanya na imepita miaka miwili sasa sijaona shida yoyote tena.

Sijawahi kuwa na historia yoyote ya kupoteza fahamu.

Kwa kweli kuna mambo hayana majibu, na hapo ndio ukuu wa Mungu unapokuja. Madaktari waliniambia mimi ni mzima niendelee kupiga kazi. Ila mpaka leo nina maswali, nini kilitokea? Sina majibu.
 
Ndiyo maana inashauriwa, mara unapoamka kutoka usingizini usikurupuke kusimama kwa haraka. Unatakiwa kukaa kitandani japo kwa dakika 3 ndipo uinuke.
 
Umeelezea vizuri sana
Tatizo watu wanapenda ushirikina na hawajiamini ndio maana wanatapeliwa kizembe
 
Hahahaha Umeua!
 
Pole sana..Dunia tuna pita ila baadhi ya wanadamu tunavita kubwa na sababu ya vita haujui na haipo sababu.
 
Akapime afya yake kwa ujumla...
 
Nimewahi kukutwa na hili jambo zaid ya mara nne,na inatokea kila nikienda haja ndogo usiku(kushtuka/kuamka na kwenda haja ndogo)
Nachukuliaga kawaida tu mana nikihisi kizunguzungu huwa natulia hadi kiishe ndo nitoke
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…