Jirani yangu ni mganga, anatufanya tusilale usiku

Mohammed wa 5

JF-Expert Member
Joined
Jun 20, 2022
Posts
1,215
Reaction score
3,035
Ni mwaka na miezi 2 tokea nimeanza kuishi maeneo haya mwazoni tulikuwa tunaishi vizuri, sababu Mimi napenda maeneo yanayotulia makelele sipendagi kabisa.

Miezi 2 nyuma Jirani yangu aliuza nyumba, yake mtu alionunua Ile nyumba hatumfahamu shida imeanza wiki ya pili sasa usiku hatulali, ni makelele tu Mara ngoma zinapiga usiku majira ya saa 7 au 8 na nyimbo zinaimbwa muda huo, usiku unasikia vishindo vya mtu anakimbia anazunguka nyumba eti anakimbizana na wachawi. Usiku umelala ghafla unasikia vilio Kama watu wanalia hivi sijui ndo wateja wake ni shida.

Baada ya kuulizia Ile nyumba anaishi nani tunasikia ni Mganga wa kienyeji shughuli zake anafanyia pale kwa sasa.

Tumeongea na balozi akaongee naye kuhusu tabia yake ya kutupigia makelele usiku tunaona kimya balozi sijui anamuogopa mpaka watoto usiku wanaogopa.

Kama mganga kweli si akaishi milimani uko?

Naomba kuwasilishaa
 
Msanii tu huyo. Mganga kweli hana mbwembwe za kukera watu.

Chukueni njiwa mtoeni manyoa yote na nazi wekeni mlangoni kwake usiku. Fululizeni kama wiki hivi muone kama hajamwaga manyanga na kuondoka.

Huyo ni mganga njaa na hapo anakutengenezeeni mazingira ya kumuogopa.
 
πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…tuelekeze sasa hakika atapata wateja wengi

Gily ndhaoata mganga naenda kuwasahaulisha wote wanaonidaiπŸ˜€
Huyu mganga wa michongo. Waganga hawakai nyumba nzuri🀣🀣🀣

Leo nimeona clip Mwamposa anamuombea mtu mwaka huu madeni ayalipeπŸ€£πŸ€£πŸ˜€
 
πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…tuelekeze sasa hakika atapata wateja wengi

Gily ndhaoata mganga naenda kuwasahaulisha wote wanaonidaiπŸ˜€
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ Mganga anaonekana ni tapeli
 
Nadhani kuna utaratibu wa kuzuia makelele hususani nyakati za usiku kwenye makazi ya watu. Anza kwa kupeleka malalamiko serikali ya mitaa.
 
Huyu mganga wa michongo. Waganga hawakai nyumba nzuri🀣🀣🀣

Leo nimeona clip Mwamposa anamuombea mtu mwaka huu madeni ayalipeπŸ€£πŸ€£πŸ˜€
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ Mganga anavaa hadi suti
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…