Kaka, mimi ni binadamu na ninaishi mazingira hayohayo ambayo nyinyi mnaishi na hii story sijaiandika nikaikamilisha kiasi niweze kuituma muda wowote ninaotaka, ni kwamba naandika na kutuma, hivyo muda mwingine naweza nikalenga kutuma muda fulani lakini nikatokea kushindwa kwasababu tofauti tofauti, sasa siwezi kufupisha ama kutuma nusu, nitalazimika tena nikipata muda niendelee kuandika kisha ndo nitume.
Sio kila muda nakuwa na simu mkononi, na sio kila muda ninaotaraji kuwa na simu mkononi kwa muda wa kutosha basi inakuwa hivyo. I am not an automatic robot. Najitahidi kadiri na muda wangu kuja kumfurahisha huyo mtu anayenitukana matusi ya nguoni na hata wengine ambao hawajahi kucomment lakini wanapenda kusoma vilevile, kususa sio haiba yangu, na jambo hili nililianzisha mwenyewe, nitalimaliza mwenyewe. Muda mwingine ni aibu kusemasema kila kilichokukuta na unachopitia, unanyamaza tu then unaendelea, unawatazama watu ukiamini kilichowajaa ndicho kinachowatoka.