Jirani yangu wa kule Goba hakuwa mtu wa kawaida

Jirani yangu wa kule Goba hakuwa mtu wa kawaida

Huyu msimuliaji ana vitu vifuatavyo:-
1. Ana kiasi kikubwa sana cha umbea, kuacha uaingizi saa tisa usiku kukaa dirishani kuangalia nani ataingia.
2. Ulinzi ungemfaa zaidi kuliko kazi anayofanya kwa sasa, haiwezekani ukeshe usiku kucha kulinda nyumba kwa niaba ya wapangaji wote ambao hawajakuomba.
Boda yake inalala nje hata mimi wakati sijaweka Geti nyumbani kwangu ikikuwa nalaza mkokoteni wangu chini ya dirisha langu basi nilikuwa silali aisee ukisikia chaka unachungulia lakini hata hivyo kuna siku nikakuta betry imeondoka
 
kuna watu wanafikiri wao wanavolala saa4 basi wote ndo hivyo, mtu kama Steve ninavoelewa anasubiri Mke na mtoto wakishalala yeye ndo anaweka zile movie zetu sasa za blood red sky mpaka usiku mwingi, kwahiyo hizo pilika zinapoanza most of time anakuwa macho wakati huo familia imelala na haina habari,
Halafu mke akilala ndio huwa tunachati na michepuko ukistuka saa8
 
Mambo kama hizi zilinifanya mimi nikaachana na story yangu ‘Nilivyokwenda South Africa bila kuwa na ndugu wala rafiki kule’

Watu humu wana ujuaji mwingi wakati mtu anaelezea story ya kweli ya maisha yake
@Keagan Paul kiukweli ile thread yako ulitukatili sana ila ni changamoto watu hatufanani
 
Utake ama usitake sisi kusema ni lazima tu mkuu na ukiona unakasirika basi ujue wewe si muungwana. Cheki haya:-
A.Mke kwenye intro unae lakini Stori ilivyoanza hukuwa nae (na ikapendeza uwe huna mke). Kuna waliotetea kwamba mke alitajwa kwenye geti limefungwa na Bonge huku ukiwa bafuni. Labda wenzetu hawawezi kusoma maana ulisema ulisogelea madirisha ya waliokuwa ndani (majirani) na mpaka jirani mwenyewe akakuona kabla hujagonga Wala kumwita sasa hapo mke yukwapi?

B.Umesema mke hakukuwA na sababu ya kumtaja maana hakukuwA na sehemu ya mojakwamoja ya yeye kuingia mapema ikaendana na stori. Wakati huohuo umesahau Kuna Stori kibao umezirefusha ambazo basins muunganiko wa mojakwamoja na stori. Mfano story za agenda za mkutano mpaka zilivyowasilishwa, Stori ya mama Bembela, na mifano mingine

C.Unalala kesho yake lakini hakuna hata mke kukuamsha kwenye usingizi mzito. Unatulia dirishani si chini ya nusu saa lakini hakuna hata mke kushtuka siku moja na kushangaa hata akakuuliza kulikoni. Hospital sijui zahanati mkitaka kwenda mke hakushiriki hata kunyanyua gauni la jirani yake lisiingie kwenye tairi ya pikipiki.

D.Bembela ni jirani yako lakini tena Bembela ni mtoto wa huyohuyo jirani yako. Halafu walikuwa wanazozana lakini kumbe kutoka ni Bembela kamleta mtoto apigwe na kwa Big hayupo aliyetoka sasa sijui alikuwa anazozana na nani. Mtoto wa big ulisema ni chizi like lakini hapo mwisho umetaja watoto kukaongezeka tena kama chizi wa pili ambapo umesema mkeo hakuwa akimjua vizuri kwakuwa alikuwa akifungiwa (au ni Mimi nimeshindwa kusoma na kuelewa labda).

E.Kwa macho ya wanawake lakini mkeo hakuweza kuona mke wa Big anavyokukata jicho. Hakuandalii maji, chakula, hakupokei, Wala hamuagani ukitoka. Tufanye hakuwepo kikaoni basi au alisafiri Kipindi chote Cha mauzauza. Una Kazi Fulani unamalizia kwa Laptop lakini... au basi!

Kuna mtu alisema kadiri unavyoirefusha Stori ndo unavyozidi kuiharibu, nimeamini nilipofika sehemu ya 8. Labda tu niseme wazi Mimi sinaga tabia ya kufuatilia maseason au mastori yenye episodes lakini hii ilinivutia kuifuatilia nikaisoma yote. Kusema ukweli ilipofika kwenye unaenda kilabuni kutafuta mbege nikaanza kukosa mvuto ila nikajikaza nikijua mbele itarudi itakuwa nzuri lakini kwa mpaka kufikia sehemu ya 8 niseme tu safari imenishinda nakung'uta matako naaga mashindano rasmi.
Mtanipa summury mtakaomaliza yote
,lubawa
 
Hili ni tatizo la afya ya akili.. wewe unatakiwa ikamatwe ufungwe na kamba mikono nyuma na miguu yote miwili upakiwe kwenye ambulance huku ikipigwa ng’ora kwa speed kali.. upelekwe Milembe
 
Mbona ni mtiririko unaoeleweka jamaa alienda kununua mbege akakosa akabidi aanze kupiga bia kuja kushtuka saa mbili akaamua arudi home kupitia njia ya korongoni ndio akaona mifuko anayotupa big kwenda kuchek anakuta kichwa cha mbuzi na nywele nyewel + plus sh. 50. Hicho ni kipande muhimu kuendelea kumjua big ni mtu gani.
Tushakubaliana kuwa humu ndani kuna wajinga wengi sana mkuu.
 
Kaka unanikumbusha humu Jf. Kuna jamaa alileta stori yake ya kusaka utajiri Kwa njia za kishirikina. Alienda mpaka Congo kupitia Kigoma. Baadae akakataa kuendelea kuandika akadai Kuna watu wamesema akiendelea watamuua. Akapost na sms za vitisho alizokuwa anatumiwa. Yule jamaa popote alipo natamani nijue stori yake mpaka mwisho.
Jamaa alikatisha story na kuhamia telegram, baadhi tuliamua kumfuatilia huko huko hadi mwisho wa story.
 
SteveMollel wakikuzingua zaidi twende Telegram, anzisha channel ufunge comments sie tutajiunga na kukufuatilia huko, yaan hapa ukitazama episode ya mwisho uliyoitoa iko mbali sana inamlazimu mtu kuingia kila page kutafuta kama kuna muendelezo ad tunakata tamaa 🙁
 
Story imejaa sana uongo, baada ya watu kuulizia mkeo naona Sasa umeanza kumchomeka kwenye story tena hata sehemu ambayo hakupaswa kutajwa.

UONGO
Truly nmerealize huyu jamaa ni muongo hata kama atakataa ila hii story ni ya kutunga na siyo ya kweli kama asemavyo.

Sent from my SM-G9350 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom