Jirani yangu wa kule Goba hakuwa mtu wa kawaida

SteveMollel amepoteza muelekeo sasa hivi nikama anakurupuka kuleta story hazina namba za episode mimi namshauri apitie zahanati iliyo karibu nae au aombe msaada kwa dr namugari aweze kupata ushauri wa kiafya ya akili....
Wewe ndiomgonjwa mkuu..
Hadithi hujatunga wewe!
Husimulii wewe
Hujalazimishwa kusoma
Bando lakw
Sasa makasiriko ya Nini !?
 
Yule Jirani yangu wa Goba hakuwa mtu wa kawaida - Bonus ya usiku ulopita.

Katika majira ya saa mbili kasoro usiku, nilitoka kazini nikipanga kwenda kwanza nyumbani, Goba, alafu ndo' niende kule Afrikana kuungana na familia yangu. Sababu ya kufanya hivyo ilikuwa ni kumtimizia Bembela takwa lake kisha nimwache aendelee kufanya kazi yake kwa usiku huo.

Nilipofika nyumbani, nilitafuta ile sarafu ya hamsini pale kwenye droo ya kitanda, sikuiona, nikakung'uta nguo zangu nilizozivaa karibuni, napo pia sikuambulia kitu, zote zilikuwa kavu mifukoni, nikatazama chini ya kitanda tena kwa kumulika na tochi ya simu yangu, sikuona kitu.

Nikaketi nikijaribu kuwaza, wapi nimeweka pesa hiyo ya sarafu? Nilifanya kila kumbukumbu na niligusa kila eneo langu la michezo lakini bado sikufua dafu.

Kidogo wazo likanijia, nikague nguo za mwanangu, haswa zile nguo ambazo alizivaa hapa karibuni, basi nikafanya hivyo kwa upesi, japo kumbukumbu yangu ya nguo zake haikuwa vema sana, nadhani zoezi hilo angelifanya mama yake lingekuwa na ufanisi zaidi kuliko mimi. Nilitazama nguo hizo moja baada ya nyingine lakini napo sikupata kitu! Sasa nikakaribia kukata tamaa. Taratibu nikaanza kuwaza huenda pesa ile haimo ndani.

Nikiwa hapo nawaza, kama bahati tu nikasikia watu wakiwa wanaongea huko nje, walikuwa ni wanawake katika bomba la maji, sauti ya mmojawapo ikanipatia wazo, nayo haikuwa ya mwingine bali ya Mama Tarimo, upesi nikatoka ndani kwenda nje kuonana naye, nilipomfikia nikamuuliza, japo kwa taabu sana kwasababu ya mdomo wangu kuuma, kama amepata kuona popote pale mwanangu akiwa na sarafu mpya ya hamsini, akanijibu hakupata kuona.

Lakini wakati naondoka, akaniita na kuniuliza kuhusu sarafu hiyo, alistaajabu ni kwanini naitafuta maana haiwezi kunipa chochote kwenye duka la sasa, nikamweleza nilikuwa na kazi nayo fulani, kazi ambayo mimi sikutaka aifahamu kwa muda huo, lakini ajabu, wakati nikiagana naye nipate kwenda, aliniambia: "lakini ninazo sarafu zingine kama hiyo unayoitafuta."

Nikasita nikimtazama, naye akatazama watu wengine kabla hatujasogea kando kidogo tupate kuongea. Huko pembeni akaniambia jambo ambalo lilinistaajabisha kidogo, mama huyo alisema anazo sarafu kama ishirini hivi za shilingi hamsini hamsini, sarafu mpya kabisa kana kwamba zimetoka benki muda huu, mimi upesi nikamuuliza sarafu hizo amezitoa wapi? Kwa sauti ya chini akanijibu alimwona nazo mwanaye mdogo, naye alipomuuliza akasema alipewa na yule mtoto wa BIGI mwenye matatizo ya akili.

Aliniambia, "yule mtoto huwa anakuwa na hizo sarafu kedekede anawagawia wenziwe wakiwa naye, siku ya kwanza niliziona nikazipuuzia lakini kadiri nilivyokuwa naziona tena mara kwa mara, nikaanza kuzitunza, hata sasa ninazo kama za alfu mbili hivi!"

Nikamuuliza kama pesa hizo ameshawahi kuzichanganya na pesa zingine, akaniambia hajawahi kamwe, pesa hizo amekuwa akizitenga mbali kabisa na pesa zake za kila siku kwani alizihofia na hakuziamini kabisa.

Hofu hiyo ikanipa mimi maswali - nini kilimfanya akahisi mawazo hayo? ... Nadhani aliusoma uso wangu wenye maulizo akaamua kufunguka mwenyewe, akaniambia namna mume wake alivyokuwa na mashaka juu ya yule jirani yetu na alishamweleza mambo kadha wa kadha kabla hajapata kulala kwenye kitanda cha hospitali kwasababu ya ajali.

Baada ya maelezo hayo, nikaongozana naye mpaka kwake, akanipatia sarafu tano za shilingi hamsini, sarafu ambazo zilikuwa zinang'aa kana kwamba lulu, kisha akanitakia mema na hicho ninachoenda kufanya nazo, mimi kutoka hapo nikaenda moja kwa moja kwenye mlango wa Bembela, nikagonga na punde mwanamke huyo akanikaribisha mpaka ndani.

Humo nilimkuta akiwa na mwanamke mwingine ambaye mimi sikuwa namfahamu, mwanamke huyo ni mzee wa makamo ya miaka hamsini na kitu hivi, Bembela akanitambulisha kuwa ni shangazi yake, na mwanamke huyo ndiye aliongozana naye kwenda huko Tanga kwa mtaalam hivyo basi mimi niwe huru mbele yake.

Lakini mbali na hilo, kwasababu uso wa mtu haujifichi kama sehemu za siri, Bembela aliniona na alistaajabu kuhusu mdomo wangu ulopinda, alinihurumia sana namna ninavyoongea na namna nilivyohisi maumivu nikifanya hivyo lakini akaniahidi yote yatakuwa sawa muda si mrefu.

Alisema, "najua hii ni kazi ya mikono yake, hamna mtu mwingine, ila mwisho wake sasa umefika, atalipa yale yote aliyoyafanya!"

Mwanamke huyo alinieleza mambo mengi ya pale nyumbani, mambo ambayo alipata kuyaona kule alipokuwa kwa mtaalamu, jinsi gani bwana BIGI alivyofanikiwa kugusa kila mlango wa kila nyumba hata wengine wakiwa hawana ufahamu mpaka sasa, lakini katika yote alokuwa ananieleza, mimi likanigusa sana jambo la bwana Tarimo na la jirani mwingine mmoja ambaye kazi yake ilikuwa ya kiwandani, Twiga Cement, nikaamini kweli hasidi haitaji sababu. Bwana huyo, pamoja na kazi yake kuwa ngumu na ya kutaabika kiwandani, hakuwa anaionja pesa yake hata thumni. Kila alipokuwa akipata ujira wake, matatizo yaliamka kutoka kila kona nane za dunia yakamwandama na kumwacha mtupu!

Haikujalisha namna gani alihangaika na kujipanga, hakuwahi kutoka katika huo mtego kamwe.

Akiwa ananieleza hayo, mara kidogo mlango ukagonga na kufunguliwa, kutazama alikuwa ni shoga yake na Bembela, sasa nikaona ni muda wangu sahihi kuondoka, nilisimama kumpisha maana sehemu ya kukaa ilikuwa finyu kisha nikawaaga niende zangu, hapo tayari nishamkabidhi Bembela mzigo wake wa zile sarafu.

Kabla sijatoka, Bembela alinikabidhi kimfuko kidogo cha 'nylon' kilichofungwa fundo moja kubwa, ndani yake kuna unga laini wa kahawia, akaniambia, "kachanganye dawa hii na maji yako ya kuogea, utakuwa unaoga asubuhi na jioni, ni dawa ya kujisafisha na dhalili zote zilizowekwa na mtu mbaya, tena ni vema ukampatia mke wako na mtoto wako."

Nikamshukuru kisha nikaenda zangu. Niliwasha pikipiki moja kwa moja mpaka maeneo ya Afrikana, Mbezi Beach, kabla ya kwenda nyumbani nikaona ni stara kupitia kwenye duka moja la dawa kuchukua dawa fulani za maumivu kwaajili ya taya zangu. Kwasababu nilipitia njia ya 'Kwa Zena' niliingia pale 'Yes Pharmacy', moja ya famasi kongwe eneo lile, nikaeleza hitaji langu, lakini punde mfamasia aliponiona na hali yangu akaanza kunipa maelezo kedekede, maelezo ambayo kwakweli yalinitisha sana.

Aliniuliza kwanza najiskiaje na miguu na mikono yangu,vidole na maungo yangu, kisha akaniuliza tena najiskiaje ninapotembea, nilipomwambia nimekuja na pikipiki akastaajabu sana, aliniambia niende hospitali haraka kwani yawezekana kabisa nipo kwenye hatari ya kupata kiharusi, hemiplegia, basi nikaondoka hapo nikiwa ma msongo wa mawazo kweli.

Nilipowaza pia na nyumbani ninapoenda itabidi nikaanze kutoa maelezo ya nini kimenikumba na huu mdomo, nikachoka zaidi.

Nilipofika nikamweleza mama na mke wangu yale yalonisibu alafu nikapata kwenda kitandani mapema kabisa kabla baba hajarejea maana nilijua ningeanza kurudia tena maelezo ambayo tayari nimeshayatoa, lakini katika yote hayo niliyoeleza sikusema lile la famasi kamwe, niliona itakuwa nongwa kubwa nikilitamka, watu watajawa na hofu kisha wakaniparamisha.

Lakini usiku huo mimi sikupata usingizi kabisa, nilikuwa najigeuza huku na huku nawaza, najigeuza kule kule nawaza, najigeuza hapa na pale maumivu.. najiuliza hali yangu na yale yanayoendelea nyumbani.

Nilikuja kupata usingizi saa kumi na moja alfajiri, nakuja kuamshwa baadae na mke wangu, majira ya saa tatu asubuhi, baada ya simu yangu kuita mara kadhaa na yeye kupokea simu kutoka nyumbani, yani kule Goba.

Aliniambia amepigiwa simu hiyo na jirani Mama Tarimo ya kwamba nyumbani kuna taarifa mbaya. Kusikia hivyo, moyo wangu ukaruka pigo. Nilijikuta akili yangu inafikiria upesi kila kitu cha jana yake, kabla sijaanza kutunga yatakayokuwa yamesibu huko, akaniambia ni taarifa za msiba.

Kuna mtu amefariki usiku wa kuamkia siku hiyo.
Yule Jirani yangu wa kule Goba hakuwa mtu wa Kawaida - 11

"Baba fulani, mtoto wa BIGI amefariki."

Kusikia hizo habari ikabidi ninyanyuke kuketi, nikawaza ina maana lile swala la Bembela lilikuwa ndio hilo? Yaani amemuua yule mtoto? Ndicho nilichofikiria, nilinyanyuka upesi maana usingizi na mang'amung'amu yake yote yalikuwa yamekata, nikaenda kuoga na kuketi mahali kwanza ili nipate kuandika ujumbe wa 'excuse' kwenda kazini maana tayari 'enyewe nilikuwa n'shachelewa kwenda huko, ni saa nne kasoro ya asubuhi sasa, alafu baada ya hapo ndo' nikamtafuta Bembela kwa kumtumia ujumbe, niliona hiyo ni njia bora zaidi kwangu kuliko kumpigia simu kwasababu ya madhila yangu ya mdomo, nilipotuma ujumbe huo nikakaa kungoja.

Ni baadae, kama nusu saa mbele, nikiwa napata kifungua kinywa kwa tabu yangu ya mdomo ndipo nikasikia ujumbe umeingia kwenye simu, kutazama upesi nikakuta ni ujumbe kutoka kazini, kinyume kabisa na matarajio yangu, basi nikang'aka kwa hasira, nikaona sasa bora nipige simu huenda mhusika wangu yu mbali na kifaa chake cha mawasiliano, simu nayo ikaita lakini haikujibiwa.

Nilipopiga mara mbili, nikaachana nayo nikiamini zile 'missed calls' zilikuwa zinatosha, mhusika atakapoziona basi atanitafuta kwa muda wake, mimi nikaendelea na mambo yangu.

Baadae majira ya mchana, nikiwa hapohapo nyumbani, sijatoka kwenda mahali popote pale, nikaonana na mama yangu ambaye tangu naamka sikupata kuonana naye, alikuwa amerejea kutoka mahali fulani, na punde baada ya kufika na kunitazama usoni, kwa huruma ya mama, akaanza kunipa nasaha za janga lile lililonikumba.

Alinisihi sana niende hospitali na tayari alishamweleza baba kuhusu hali yangu hiyo, hata na hivyo alishangaa sana mpaka muda huo sikuwa nimejigusa kwenda kutafuta tiba, alisema nina roho ngumu kweli, lakini kitu ambacho hakujua mimi mwenzake tayari nilishaogea ile dawa nlopewa na Bembela tangu asubuhi, dawa ya kuondoa mabaki yote yalotupwa na wabaya wangu kwa mujibu wa maneno yake, nikawa naamini dawa hiyo huenda ikanisaidia, niwe tu mvumilivu.

Basi masaa ya siku hiyo yakazidi kusogea, bado nipo hapo nyumbani na bado sijapokea ujumbe wowote toka kwa Bembela, kila nilipopata nafasi nilitazama simu yangu lakini sikuambulia kitu, sio 'call' wala 'message', mwanamke yule hakunitafuta kabisa, mpaka giza jepesi linaingia, kimya tu.

Nikajaribu kuongea na mke wangu ampigie simu Mama Tarimo kumuulizia Bembela kwani nina shida naye, nilimweleza ni shida ya dawa ya ugonjwa wangu ili kupunguza maswali yake mengi, mwanamke huyo akaridhia na punde akapiga simu ambayo aliiweka 'loudspeaker', kidogo simu kuita ikapokelewa na Mama Tarimo, mke wangu akamwelezea shida yangu, mama huyo akamjibu: "nimetoka nyumbani majira ya mchana mpaka sasa bado sijarejea, nilienda hospitali kumwona mgonjwa wangu, walakini niko njiani narudi, ningoje kidogo nikifika nitamtazama."

Baada ya hapo kazi ikawa ni kungoja. Kichwani najiuliza kwanini Bembela alifanya kile kitendo? Kwanini mtoto? Sasa kwa kufanya hivyo tofauti yetu na BIGI itakuwa nini kama wote ni wauaji? Yani nilikuwa na hamu kweli ya kuongea naye, nilihisi maswali yangu yananikaba kooni nashindwa kuhema, naona kama muda hauendi.

Kweli baadae, kama lisaa hivi kupita, Mama Tarimo akatimiza ahadi yake kwa kupiga simu, nilimwona mke wangu akinijia upesi huku simu ameiweka 'loudspeaker', aliponikaribia nikasikia Mama Tarimo akisema, "Nimefika lakini Bembela hayuko nyumbani, sio yeye wala shoga yake niliyemwona, nadhani wametoka, wakirejea nikafanikiwa kuwaona basi ntakujuza."

Baada ya hapo hata mimi binafsi nilipojaribu kumpigia Bembela sikumpata, sio tena hapokei simu bali hapatikani hewani kabisa. Hata yule shoga yake mke wangu alipojaribu kumtafuta kwa namba alonayo, naye hakumpata hewani! Sikujua nini kiliwakuta? Nilijipata najawa na hofu kifuani mwangu nikiomba yote yawe salama maana mpaka hapo sikuwa na lingine la kufanya zaidi ya hilo.

Kama utani, usiku ule ukapita kimya, kesho yake asubuhi niliamka mapema majira ya saa kumi na mbili, bado taya yangu inasumbua na imegoma kurejea kwenye hali yake ya kawaida, ile dawa ninayotumia bado haijanisaidia, mara kidogo nikiwa najiandaa ndipo simu yangu ikapokea ujumbe kutoka namba niliyoitambua upesi kuwa ni ya Bembela, ujumbe huo ulisomeka hivi:

"Habari yako shemeji, nimeona ulinitafuta tunaweza tukaongea saa hii kama una muda."

Haraka nikamrudishia majibu kwamba ni vema tukachat maana mimi bado siwezi kuongea vizuri, basi baada ya hapo tukalowea kwenye 'messages'. Nilimuuliza yuko wapi, hakutaka kuniambia, alichosema yeye yuko mbali ila salama, huko ameongozana na shangazi na shoga yake kwasababu fulani ambayo nayo pia hakutaka kuniambia.

Nikamuuliza kuhusu kifo cha mtoto wa BIGI, hapo kidogo akakwama, nadhani aliogopa kujibu swala hilo kwa njia ya ujumbe ama aliona hatoweza kulielezea vema vile anavyotaka yeye basi muda kidogo akaamua kunipigia simu kwaajili ya kuniweka sawa. Mwanamke huyo, kwa sauti ya chini, alinambia hafahamu chochote kuhusu kifo cha yule mtoto, yeye alichokifanya usiku ule ni kilekile alichoelekezwa na mtaalam kwaajili ya kumwadabisha BIGI na si vinginevyo.

Kwa maneno yake alisema, "mtaalam aliniambia nikikamilisha zoezi la kunuwia, kukoga na kumwaga dawa kisha nikamwita nikiwa nimeshikilia kitu ambacho ni mali yake binafsi basi bwana huyo atapoteza nguvu zake zote, na tena nitamkuta pale kibarazani akiwa uchi wa mnyama ili kila mtu apate kumshuhudia na kumjua kuwa ni mchawi, lakini ajabu nilipofanya hivyo asubuhi yake saa kumi na moja, nilimkuta yule mtoto, akiwa uchi wa mnyama, ameshikilia nguzo ya kibarazani, mwili wake hauna hata tone la pumzi. Mikononi mwake na miguu pake pana sarafu zile za hamsini hamsini!"

Kwakweli maelezo hayo yakaniacha mataa ya bumbuwazi. Kuna muda nilihisi nasikiliza tamthilia lakini kumbe ndo uhalisia wenyewe, nikaamini kweli ya dunia ni mengi sana!

Mwanamke huyo aliendelea kuniambia ya kwamba wakati mwili wa mtoto huyo ukiwa hapo kibarazani pasipo uhai, shangazi yake alimshuhudia BIGI kwa macho yake mwenyewe akiwa amesimama mwisho wa korido, amesimama hapo akiwa anamtazama kama paka aliyefura kwa kipigo, bila kufanya jambo akajiondokea zake na hapo ndipo wakakata shauri kuyeya hapo nyumbani baada ya shangazi yake kumsihi.

Hivyo mpaka wanaondoka, yeye, shangazi yake na shoga yake kwenda huko waliko, mwili wa yule mtoto ulikuwa palepale, hawakujua tena nini kilichofuatia baada ya hapo na hawakuwasiliana na mtu yoyote wa pale nyumbani mpaka asubuhi ya siku hiyo ambapo kabla hajawasiliana na mimi alipata kuongea na mwenye nyumba kwanza.

Baada ya kuhitimisha maongezi hayo, mimi niliendelea na maandalizi yangu, nilipokamilisha nikapitia hospitali kucheki tatizo langu maana niliona ni vema pia nikafanya hivyo, lakini huko kote hamna nilichofanya zaidi ya kupoteza tu pesa maana hamna chochote nilichoambwa na daktari, nikarejea zangu nyumbani, Afrikana.

Baadae majira ya jioni nilipata wasaa wa kuongea na wazazi wangu nikawaeleza juu ya yale niliyoambiwa kule hospitali, tena nikiongea kwa tabu sana, kuna muda machozi yalikuwa yananilenga nilipokuwa najitazama kwenye kioo nikiona namna nilivyobadilika kuwa wa ajabu, yani nakuwa mlemavu huku najiona, lakini ndo' hivyo sikuwa na namna.

Baba yangu alinishauri tufanye namna ya kumwona daktari bingwa wa mifumo ya fahamu, Neurologist, ili apate kunisaidia lakini mimi sikuwa radhi kabisa na hilo kwasababu niliamini lile tatizo nililokuwa nalo lilikuwa ni la kiimani zaidi kuliko hospitali, lakini kwasababu nalimfahamu mzee wangu vema, sikumwambia kitu maana hata kama ningemwelezea basi asingeniafiki hata kidogo, si mtu anayeamini kwenye mambo ya kishirikina na mimi simlaumu maana mambo haya kama hujapata kuyaona kwa macho yako ya nyama basi hutakaa uamini,kila atakayekueleza utaona ni ngano na visasili tu, hata mimi nilikuwa vivyo hivyo lakini nilikuja kujifunza katika njia ngumu hapo mbeleni.

Nakumbuka mama yangu alikuwa akinikandika mafuta ya Mwamposa na sala kedekede, lakini tena naendelea kuogea ile dawa nlopewa na Bembela, yaani tafarani tu, sijui hata kipi kilikuja kunisaidia kuniponya kati ya hivyo viwili. Mungu mwenyewe anajua.

Baada ya siku kama tatu hivi kupita baada ya kile kikao kidofo na wazazi, nilirejea nyumbani kule Goba, na kesho yake tu baada ya kufika, alikuja mwenye nyumba akitaka kukaa kikao na sisi wote kwa pamoja, siku hiyo ilikuwa 'weekend' kama si Jumamosi basi Jumapili, na taarifa ya kikao nadhani kila mmoja alikuwa ameshaipata, mimi binafsi niliupokea ujumbe siku mbili nyuma yake, hivyo kwenye kile kikao kulikuwapo na watu karibia wote, mtu pekee mzima wa afya ambaye hakuwapo ni BIGI, na hiyo haikuwa ajabu, tulishazoea, Bembela yeye alifika wakati kikao kimeshaanza, alikuja akiongozana na shangazi yake lakini mwanamke huyo mzee hakupata kujiunga na sisi kikaoni isipokuwa Bembela pekee.

Katika kikao hicho, mwenye nyumba alieleza kuwa jambo pekee lililomleta na kutukutanisha na sisi hapo ni swala la mpangaji mwenzetu ambaye alikumbwa na ile kadhia ya mwanae kufariki katika mazingira ya kutatanisha mbele ya kibaraza, bwana huyo alisema namna alivyokuwa anapitia matatizo na vyombo vya usalama, mathalani polisi na ulinzi shirikikishi, kwasababu ya mpangaji yule ambaye alienda mbele zaidi kumwita 'mpangaji asokuwa na mkataba'.

Alituambia pia namna alivyopokea malalamiko kadha wa kadha kumhusu bwana yule kutoka kwa wapangaji, majirani na Mjumbe, hivyo basi akawa amefikia maamuzi ya kutamatisha uwepo wake hapo akiahidi kurejesha pesa yake ya miezi michache ilobakia ili aende kwa amani, habari za nyumba yake kusemwa vibaya hata na watu wanaokaa nje ya zile kuta, tena huku na kule, zilimfanya ahofie kama atapata mpangaji mwingine hivi karibuni.

Baada ya maelezo hayo, kila mtu akiwa amemwelewa na kasema ya kwake, swala likabakia huyo bwana BIGI atapatikanaje? Kila mpangaji hakuwa anakumbuka alimwona lini bwana huyo jua likiwa linawaka, mwenye nyumba akasema yeye siku hiyo atangoja mpaka amwone, hatoondoka hapo mpaka atakapotimiza adhma yake, basi na kikao kikaparangayika, mimi nikapata wasaa wa kumsalimu Bembela na hata kumkaribisha ndani kwangu tupate kuongea mambo kadhaa, Bembela akiongozana na shangazi yake, wakajumuika na sisi sebuleni.

Katika mengi waliyoongea, moja ya machache niliyopata kuyashika ni maneno fulani ya yule Shangazi. Mwanamke yule mzee, kwa muda mchache niliokaa naye na kumsikiza, nilibaini ni mtu mwenye uzoefu kamilifu na mambo haya ya gizani, kama ni wataalamu na mambo yao, walozi na vituko vyao, basi yu kwenye kina cha peke yake, na kwa namna alivyokuwa anaongea, niliiona kabisa picha kichwani mwangu kuwa yeye ndo' aliyefanya lile zoezi usiku ule, wala sio Bembela.

Mwanamke huyo alisema hivi, kwa nadhiri ile waliyoifanya siku ile alafu matokeo yake wakajikuta dhahama inamwangukia yule mtoto badala ya mwenyewe bwana BIGI, anaamini kabisa kilikuwa ni kiashiria kuwa mtoto yule ni sehemu ya ndani ya yule bwana ama ni bwana yule kabisa aliyegawanyika katika maumbo mawili, moja la mkewe na jingine la mtoto, kila umbo likiwa na kazi yake maalum, mtoto yule kazi yake kukusanya pesa na ndo maana alikuwa hakaukiwi na sarafu na mwanamke yule kazi yake ilikuwa kulinda usalama wa BIGI na pesa hizo.

Kwasababu hiyo, wale viumbe wawili, yaani mtoto na yule mwanamke, hawawezi wakawa binadamu walokamilika kamwe, wote watabakiwa kuwa nusu inayokamilisha mwili mmoja wa BIGI, na jukumu la BIGI kwao ni moja tu, kuwalisha na kuwahudumia viumbe hivyo kwa hali na mali.

Alisema: "ukihangaika na BIGI hutakaa ufanikiwe kamwe, hata ukitumia silaha gani, lakini ukicheza na ile mikono yake miwili, utamshinda kama ubua. Laiti tungepata chochote kinachomilikiwa na yule mwanamke kama vile tulivyopata sarafu zilizokuwa zinamilikiwa na yule mtoto, basi naye tungemwangamiza bwana BIGI akabakia mpweke kama binadamu wengine."

Hapo nikajikuta nakumbuka zile nywele kwenye viroba, nikawaza hazikuwa za mwanamke yule kweli? ... maana siku ile namwona kichwa chake kilikuwa cheupe peh, kimenyolewa, kitu ambacho sikuwahi kuelewa ni namna gani nywele hizo zilivyokuwa zinamea na kunyolewa mara kwa mara. Lakini pia nikakumbuka yale matone yake ya damu aliyoyachuruza siku ile wakati akipelekwa na bwana BIGI maliwatoni, nikabaki mwenyewe na hizo fikra nisithubutu kuunyanyua mdomo.

Kwani,

Binafsi niliyachukulia maneno ya yule mama kama nadharia tu, ya kwamba anajaribu kuoanisha mawazo yake kichwani na matukio yanayotokea ili kupata uhalisia ila hamna kitu cha uhakika ndani yake hivyo sikuyapa mazingatio sana, ila kilichofuata kesho yake kikanifanya nimkumbuke mama huyo na maneno ya kinywa chake.

Baada ya siku ile Baba mwenye nyumba kukaa mpaka usiku mkubwa akimngoja BIGI pasipo mafanikio, aliondoka akarejea kesho yake katika majira ya mchana akiwa ameongozana na mjumbe na wanaume wawili ambao niliwatambua kama ulinzi shirikishi.

Alipofika alitusalimu kama kawaida yake kisha akaulizia kama bwana yule ameonekana, kila mtu akasema hakumwona. Alipopata majibu hayo, akiwa ameongozana na mjumbe, aliufungua mlango wa BIGI kwa kutumia funguo yake ya ziada kisha wakazama humo ndani.

Baada ya muda kidogo, mara tukaitwa wanaume wengine wawili kwaajili ya kutoa msaada, mimi nikiwa mmojawapo, kuingia tu ndani pale chini sakafuni namwona BIGI amejilaza chali anatazama dari, taya yake ya chini imeelekea kushoto kama ilivyokuwa kwangu, pembeni yake amelala yule mke wake akiwa amefumba macho kama mtu aliyepotelea usingizini, wote wamevalia kaniki nyeusi.

Nikiwa bado nashangaa nikamsikia Mjumbe anasema,

"Haya, huyu amepooza, tumbebe tumpeleke kwenye gari la mzee ...(hapa alitaja jina la baba mwenye nyumba)."

Nakwambia sijui ni nini kilitokea hata leo hii sielewi, lakini nilijikuta akili yangu inanikumbusha upesi taswira ya yule shangazi yake Bembela.

Nilijiuliza hivi yule mwanamke alikuwa kweli ni shangazi yake kama alivyosema ama ndiye ........

MUENDELEZO, SOMA=> Sehemu ya 12
 
Doh! Nilale sasa maana nimesubiria usingizi ulikua hauji kabisa.
 
Shukrani
 
Yamoto kabisa!

Big up Mkuu!🤛
 
Story Moja nzuri sana umefanya tuwe na alosto na hii story
 
baby zu Darlin Shunie
 
Get Rich atlas copco Watu8
 
Back
Top Bottom