Aliko Musa
JF-Expert Member
- Aug 25, 2018
- 209
- 315
Naitwa Aliko Musa kutokea jiji la Mbeya. Mimi ni mwandishi mbobezi wa makala na vitabu vya mbinu bora za kuwekeza kwenye viwanja na nyumba. Ninawafikia wawekezaji kupitia mtandao wangu uitwao UWEKEZAJI MAJENGO.
Nimekuandalia mafunzo mazuri sana ambayo yatakuwezesha kuanza na kuendelea na safari ya kujenga utajiri wako kupitia uwekezaji kwenye ardhi na majengo.
Maswali 10 Muhimu Kuhusu Mafunzo Haya.
(1) Je nani anafaa kujiunga mafunzo haya?.
Kuna makundi mawili ambayo yanatakiwa kujiunga na programu hizi ya mafunzo. Kundi la kwanza ni yeyote anayetaka kujenga utajiri kupitia viwanja na nyumba. Kundi la pili ni mtu yeyote anayetaka kutunza utajiri kupitia viwanja na nyumba.
(2) Je mafunzo yatakuwa ya muda gani?.
Mafunzo yatakuwa ni ya siku 10 tu. Lakini kwenye kundi hili la TANZANIA REAL ESTATE TEAM (TRT) tutaendelea na programu nzuri sana ambazo nitawashirikisha malengo 3 ya kundi hili.
Hivyo baada ya mafunzo ya siku 10 wanachama wataendelea kujenga mtandao, kupata uzoefu na hamasa na kushirikishana taarifa na maarifa ya viwanja na nyumba.
(3) Je gharama za mafunzo itakuwa ni shilingi ngapi?.
Hakuna gharama za mafunzo ya siku 10. Unajiunga bure ili kujifunza.
(4) Je mafunzo yatafanyika wapi?.
Mafunzo yatafanyika kwa njia ya mtandao katika kundi la whatsapp liitwalo TANZANIA REAL ESTATE TEAM (TRT). Mafunzo yote yatawekwa kwenye blogu iitwayo UWEKEZAJI MAJENGO. Hivyo yeyote ataweza kuyapata kwa njia ya mtandao hata siku zijazo.
(5) Je kuna njia nyingine ya kupata mafunzo kwa watakaokosa fursa hii?.
Ndio. Njia mbadala ya kupata mafunzo hayo ya siku 10 itakuwa ni kulipia ada ya uanachama wa kundi la UWEKEZAJI MAJENGO. Kisha utaweza kupata mafunzo yote moja kwa moja kutoka kwangu.
(6) Je kuna fursa nyingine ya kutumia maarifa sahihi tutakayojifunza?.
Ndio, kuna fursa nzuri sana ukiacha maarifa sahihi utakayopata. Fursa yenyewe nitaitangaza mwisho wa wiki ya mafunzo haya.
(7) Je kutakuwa na nafasi ya kujitambulisha na kutangaza huduma au bidhaa zinazohusiana na viwanja na nyumba?.
Ndiyo.
Wanachama wote watakuwa na nafasi ya kutangaza na kujitangaza kwa lengo la kukuza mtandao ili waweze kujenga mtandao mkubwa wa fursa.
(8) Nina kiasi fulani cha mtaji wa fedha, je nitapata ushauri wa jinsi ya kuanza kuwekeza kwenye viwanja na nyumba?.
Ndiyo.
Kutakuwa na fursa kwa kila mwanachama kueleza malengo yake makuu kwenye uwekezaji huu. Njia ya kujieleza inaweza kuwa ni ile ya faraghani au kwenye kundi la mafunzo.
(9) Mimi sina kiasi chochote cha mtaji fedha, Je nifanyaje ili nianze kuwekeza kwenye viwanja na nyumba?.
Mafunzo yatalenga wale wenye mitaji mikubwa ya fedha, wasio na mitaji ya fedha na wenye kiasi cha kawaida cha mtaji wa fedha. Hivyo, kila mmoja ataweza kupata njia inayomfaa kuanza kuwekeza kwenye viwanja na nyumba.
(10) Je kuna kazi ya ziada kwa kila mwanachama baada ya kujifunza mafunzo hayo?.
Ndiyo.
Kazi ya kipekee sana ambayo itakuwa inafanyika na kila mwanachama ni kuhakikisha anachangia kutimizwa kwa malengo matatu (3) ya kundi.
Malengo ya kundi nitawashirikisha baada ya mafunzo ya siku 10. Lakini tunaweza kuboresha malengo ya kundi kwa kujadili wanachama wote.
Nimeandika vitabu vitatu kama vilivyo orodheshwa hapo chini;-
(a) Lugha Ya Biashara Ya Viwanja Na Nyumba Na Aliko Musa. Hiki kinauzwa Tshs.6,000/= (Elfu sita tu).
(b) Njia 120 Za Kutengeneza Fedha Kwenye Ardhi Na Majengo Na Aliko Musa. Kitabu hiki kinauzwa Tshs.6,000/= (Elfu sita tu).
(c) Usimamizi Wa Uwekezaji Kwenye Ardhi Na Majengo Na Aliko Musa. Kitabu hiki kinauzwa Tshs.10,000/= (Elfu kumi tu).
Bofya hapa kujiunga na mafunzo...
Karibu sana.
Rafiki yako,
Aliko Musa.
Mbobezi wa majengo.
0752 413 711