Jiunge nami kusema hapana kwa udhalilishaji na ubaguzi anaoufanya mmliki wa clock tower café Iringa

Ndio maana mimi napigaga msosi five stars hotels tu. Nikisikiaga njaa naibukaga dubai tu
naona tatzo lako la stroke ya akili limerudi tena, pole sana amka ujiandae uende kwa gwaima ukapate maombi, pili acha kufunga muumba anajua haya matatzo yako, haya sasa umekula daku lijisaa lililipita asaiv swaumu ishaleta stroke ya ubongo, wana jf naombeni radh kwa huyu ndugu yangu kila anapokosea, ana matatzo ya ubongo hasa akimaliza dk 30 bila kula.
 
Watu wanajua kujitangaza aiseee

Hongera advocate!
 
JIUNGE NAMI KUSEMA HAPANA KWA UDHALILISHAJI NA UBAGUZI ANAOUFANYA MMLIKI WA CLOCK TOWER CAFÉ IRINGA.

#SAYNOTOCLOCKTOWERCAFEIRINGAMISTREATMENTOFCLIENTS#
Nimekuwa mteja wa mgahawa wa Clock Tower Café uliopo barabara ya Dodoma/Uhuru Avenue katika Manispaa ya Iringa tangu uanzishwe mwaka jana. Nimekuwa nikipata huduma ya chakula katika Mgahawa wa Clock Tower nikiwa ama peke yangu au nikiwa na wageni au wateja wangu kwa kuwa ofisi yangu ya Uwakili ipo jirani tu na mgahawa huu. Hata hivyo jana tarehe 9 mwezi Mei mwaka 2019 limetokea tukio ambalo limenisononesha na kunifanya nisiwe tena na hamu ya kupata huduma ya chakula katika mgahawa wa Clock Tower Café wa hapa Iringa.

Jana ilikuwa ni siku ya tatu/ya nne ya mwezi wa Ramadhan. Nami nilikuwa katika saumu lakinijana wakati natoka mahakamani wakati napita Clock Tower Café nilijisikia haja nikaona niinge ili nijisaidie. Mnamo saan 4.00 asubuhi hivi niliingia Clock Tower Café. Nilipoingia nilimkuta Mmiliki wa Clock Tower Café, Iringa akiwa na mfanyakazi wake wa muda mrefu tangu enzi eneo hilo lilipokuwa Iringanet ikitoa huduma za mtandao wa internet. Kama ilivyo desturi niliwasalimia na kuingia ndani nikapita chooni.

Wakati nataka kutoka Clock Tower Café, niliwakuta Mmiliki na mfanyakazi wake wakiwa eneo lile lile na Mmiliki alinikabili kwa ujeuri na katika hali ya udhalilishaji na kashfa kwangu. Mbele ya wateja na wafanyakazi wa Clock Tower Café Iringa alinionyesha kwa sauti ya ukali kama vile mimi ni motto mdogo sana poster yenye maneno “Management reserves the right to refuse admission” iliyobandikwa ukutani. Maneno hayo ya Kiingereza yanamanisha: “Utawala unayo haki ya kumkataza mtu yoyote kuingia”. Na kisha kwa maneno makali akaniambia eti mimi ni mteja mbaya na kamwe hataki kuniona nikiingia au kununua chochote katika mgahawa wake wa Clock Tower Café Iringa na kwamba choo chake sio choo cha umma.

Kwa kweli nilifedheheka sana na kuvunjiwa heshima yangu katika jamii kwa tukio hili na sikuamini kinachotokea. Nimekuwa ninamfahamu Mmiliki huyo wa Clock Tower Café Iringa kwa miaka mingi sana name nimekuwa nikimchukulia kwamba ni jamaa yangu na yeye ananifahamu kwa kina na kazi ninazofanya hapa Iringa na hata baba yake namfahamu na tuna mahusiano mazuri tu kwa miaka mingi. Nimemfahamu Mmiliki huyu wa Clock Tower Cafe Iringa tangu mwaka 2015 nilipokuwa nafanya kazi Iringa na nikiwa mteja wa Iringanet tangu ilipokuwa jingo la Ghorofa pale Mshindo hadi anahamia hapa Barabara ya Dodoma. Kwa upole, nilimsihi na kumkumbusha kwamba tuko ndani ya mwezi wa Ramadhani na si vizuri kunifanyia kitendo cha udhalilishaji lakini alibaki na msimamo wake kuwa hanihitaji mimi wakla wananihusu kuwa wateja wa Clock Tower Café na kwamba niondoke na kamwe nisiingie tena Clock Tower Café Iringa. Ilibidi niondoke kwa aibu kimya kimya kwa unyonge mithili ya mbwa aliyemwagia maji akiogopa hata kubwekawa. Na jambo hili lilinishangaza sana kwa sababu sehemu ya biashara ni sehemu ya umma ambapo kila mtu anaweza kuingia na kutoka.

Kwa kweli tukio hili lininsononesha, kunidhalilisha na kunikumbisha si tukio lilimtokea mmoja wa wagombe Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye alipoingia katika Hotel moja Mjini Dar es Salaam, Uongozi wa Hotel ulikataa hata kumhudumia maji ya kunywa na pia unakumbusha madhila ya siku za ukoloni ambapo watu waafrika licha ya kuwa ndiyo wenyeji wa nchi hii walikuwa wanabaguliwa kwa rangi na hadhi yao na kukatazwa kuingia katika mahoteli au migahawa ya watu weupe. Pale jijini Tanga ilikuwa rahisi mbwa kuingia Planters Hotel lakini si Mwaafrika. Na marehemu Mzee Erasto Mang’enya katika kitabu chake kimoja anaeleza madhila haya ya ubaguzi kwa waafrika pamoja na elimu yake na kuwa mjumbe wa Mamlaka ya Mji alikuwa haruhusiwi kuingia katika Hotel za watu weupe kwa kuwa tu alikuwa ni Mwaafrika.

Na ni jambo la kusikitisha zaidi kuona kuwa baada ya zaidi ya nusu karne ya nchi yetu ya Tanzania na pia Visiwa vya Unguja na Pemba kuwa nchi huru, bado wapo watu kama Mmiliki wa Clock Tower Café Iringa ambao wanaona wanayo haki ya kumnyanyasa Mtanzania na kwamba Mwaafrika kwao ni mtu dhalili asiye na hadhi au haki ya kupata huduma katika biashara zao. Jambo hili halivumiliki hata kidogo na kamwe siwezi kukaa kimya katika hili kuona mtu kwa sababu yeye ni Mwaarabu au Mweupe anayo haki ya kumnyanyasa mtu mweusi katika ardhi ya mababu zake. Je mtu mwenye rangi nyeupe akiingia Clock Tower Café kwenda choo kujisaidia na kasha kutoka bila ya kupata huduma yoyote, je Mmiliki huyu angemsemesha katika kama alivyonisemesha mie kijeuri?

Kama Mtanzania na Mwaafrika naona fahari kuwa nimepata bahati ya kutembelea au kuishi katika nchi zingine za Afrika Mashariki, Ulaya (Norway) na Marekani (USA) lakini katika kutembea kwangu kote huko sijawahi kukatazwa kupata huduma hata ya kujisaidia chooni katika mgahawa au Hotel yoyote kokote kule duniani isipokuwa hapa Iringa katika mgahawa huu wa Clock Tower Café. Kote nilipopata huduma hotelini au mgahawani nimekuwa nikipata heshaima ya utu wangu kwa usawa bila ya kujali hali yangu, rangi yangu au Utaifa wangu hata kama nilikuwa Mwaafrika pekee mahali hapo. Kamwe sijawahi kutokewa na tukio la kubaguliwa na kuonekana dhalili na nisiye na hadhi yoyote isipokuwa jana mbele ya Mmiliki, wafanyakazi na wateja wa Clock Tower Café Iringa ndani ya Mji na nchi yangu. Jambo hili halivumiliki na ni lazima kwa vitendo tulikemee.

Msimamo wangu ni kwamba tukio lililonitokea jana kamwe lisimtokee mkazi au mtu yoyote anayetembelea Iringa. Rai yangu ni kuwa wakazi na watu wote wanaotembelea Iringa kamwe tusiingie kupata huduma Clock Tower Café Iringa kwani Mmili hatuhitaji sisi anao wateja wake wenye hadhi ya kupata huduma ya chakula chake na sio sisi wakazi na watu wanaotembelea Iringa. Tusimmudhi tuwache Mmiliki huyu awahudumie wateja wake anaowataka kwa raha zake.

Tuungane pamoja kusema hapana kwa udhahlilishaji na ubaguzi anaoufanya Mmiliki wa Clock Tower Café katika nchi yetu na mji wetu!

Tafadhali mhabarishe na mwingine!

ZUBERI HAMISI NGODA
Iringa, Tanzania
Simu: +255 655 200 200
E-Mail: advocate.ngoda@gmail.com
May 10 , 2019

Tatizo la wanasheria jambo dogo maneno mengiiii, inachosha kusoma!
 
Mkuu mimi sikubaliani na wewe na ninahisi wewe ndo ulikuwa na makosa...choo ni kwa ajili ya watu wanaopata huduma hapo na si kwa ajili ya nyi wapita njia...eti kwa sababu tu ushawahi pata huduma hapo so unaona ndo sehemu ya kwenda kumaliza haja zako mda wowote ukijiskia katika mizunguko yako...choo ni kwa ajili ya watu wanaopata huduma kwa mda ule pale
Kuwa mstaarabu na kuwa na roho ya ubinadamu wewe ukibanwa na uharisho katikati ya posta pale city center utajinyea barabarani au utaenda kuomba huduma ya choo ya pale stears? Na unavyohisi unaweza kunyimwa Huduma Ya Toilet sababu Hujanunua chakula chao? Mtu muungwana hawezi fanya hayo daima. Nyie ndio mnaoweza kumpa lifti nyani binadamu mkamuacha njiani sababu tu yeye nae ni mtu kwanini asiwe na gari yake. Jifunze hekima utaish na watu vyema
 
Huyu jamaa anadai ni wakili ?😲😲😲 Jambo la Aya tatu anaandika gazeti? Sasa sishangai kwa nini Huyo Mmiliki amekufukuza.

Maana umeandika mambo mengi unalia lia na sijui uwakili ambao unataka watu wajue umekusaidiaje. Unafanyaje kazi ikiwa kuandika kifupi tu huwezi unalia lia? Si ukamshtaki mhusika basi mahakamani kuliko kuja mshtaki JF?
Zuberi Ngoda ni wakili mkongwe, amesoma na kuishi US muda mrefu! Aliporudi Bongo alianza kufundisha sheria ikiwemo SAUT!

Ni Muslim mwenye misimamo mikali. Amewahi kuvunja furniture za mahakama (DLHT) pale Iringa baada ya kuhisi anaonewa.

Huyu jamaa sio legelege au kanjanja kama inavyohisiwa!
 
Wakili wenyewe ndo hawa wa vyuo hivi ninavyoviona? We acha kabisa hamna kitu.... Weupe sana na huu ni mfano tosha. Huyu unamwambiaje akutetee yeye tu kujitetea ameshindwa? Anakuja hapa analia lia asaidiwe.

Zuberi Ngoda ni wakili mkongwe, amesoma na kuishi US muda mrefu! Aliporudi Bongo alianza kufundisha sheria ikiwemo SAUT!

Ni Muslim mwenye misimamo mikali. Amewahi kuvunja furniture za mahakama (DLHT) pale Iringa baada ya kuhisi anaonewa.

Huyu jamaa sio legelege au kanjanja kama inavyohisiwa
 
Alaf wew mtoa mada usituchoshe, pengine ulipita direct bila kusalimia ukaenda washroom. What do you expect
 
Zuberi Ngoda ni wakili mkongwe, amesoma na kuishi US muda mrefu! Aliporudi Bongo alianza kufundisha sheria ikiwemo SAUT!

Ni Muslim mwenye misimamo mikali. Amewahi kuvunja furniture za mahakama (DLHT) pale Iringa baada ya kuhisi anaonewa.

Huyu jamaa sio legelege au kanjanja kama inavyohisiwa
Hakika mkuu
 
Kuepuka hizi Kero za Haja tumia vyoo vya umma. Kimtazamo umeona jamaa kakubagua lakini inaweza isiwe hivyo. Watu wengi hawana ustaarabu wa kutumia maliwato(Choo) wakijisaidia kusafisha(ku-flush) huwa ni shidaa, kitendo ambacho kimekuwa ni kero kwa wanaomiliki vyoo haswa vya migahawani kwani inawaharibia sifa kwa wateja. Sasa kama wewe si mteja alafu umeenda kutumia choo tu na kutoka basi lazima utakutana na kadhia kama hiyo.
 
Mkuu mimi sikubaliani na wewe na ninahisi wewe ndo ulikuwa na makosa...choo ni kwa ajili ya watu wanaopata huduma hapo na si kwa ajili ya nyi wapita njia...eti kwa sababu tu ushawahi pata huduma hapo so unaona ndo sehemu ya kwenda kumaliza haja zako mda wowote ukijiskia katika mizunguko yako...choo ni kwa ajili ya watu wanaopata huduma kwa mda ule pale
Nakubaliana nawe 💯
 
Mimi nahisi kuna chuki binafsi huyo mmiliki anayo dhidi yako. Inaweza ya moja kwa moja au ameletewa na wabaya wako.
Pili: inawezekana unapopata huduma hapo kuna tabia ambayo aidha huwa unawakera wafanyakazi na wanamlalamikia boss wao sasa siku ulipoingia hapo wakamwambia; ni huyu boss!!
Tatu: Kuna uwezekano katika shughuli zako za uwakili ushamsaidia mtu akashinda kesi ambayo huyo Mwarabu alikuwa mnufaika au alitaka ashinde kwa mizengwe
NB: Shukru amekuambia direct kuliko kukuwekea sumu
 
JIUNGE NAMI KUSEMA HAPANA KWA UDHALILISHAJI NA UBAGUZI ANAOUFANYA MMLIKI WA CLOCK TOWER CAFÉ IRINGA.

#SAYNOTOCLOCKTOWERCAFEIRINGAMISTREATMENTOFCLIENTS#
Nimekuwa mteja wa mgahawa wa Clock Tower Café uliopo barabara ya Dodoma/Uhuru Avenue katika Manispaa ya Iringa tangu uanzishwe mwaka jana. Nimekuwa nikipata huduma ya chakula katika Mgahawa wa Clock Tower nikiwa ama peke yangu au nikiwa na wageni au wateja wangu kwa kuwa ofisi yangu ya Uwakili ipo jirani tu na mgahawa huu. Hata hivyo jana tarehe 9 mwezi Mei mwaka 2019 limetokea tukio ambalo limenisononesha na kunifanya nisiwe tena na hamu ya kupata huduma ya chakula katika mgahawa wa Clock Tower Café wa hapa Iringa.

Jana ilikuwa ni siku ya tatu/ya nne ya mwezi wa Ramadhan. Nami nilikuwa katika saumu lakinijana wakati natoka mahakamani wakati napita Clock Tower Café nilijisikia haja nikaona niinge ili nijisaidie. Mnamo saan 4.00 asubuhi hivi niliingia Clock Tower Café. Nilipoingia nilimkuta Mmiliki wa Clock Tower Café, Iringa akiwa na mfanyakazi wake wa muda mrefu tangu enzi eneo hilo lilipokuwa Iringanet ikitoa huduma za mtandao wa internet. Kama ilivyo desturi niliwasalimia na kuingia ndani nikapita chooni.

Wakati nataka kutoka Clock Tower Café, niliwakuta Mmiliki na mfanyakazi wake wakiwa eneo lile lile na Mmiliki alinikabili kwa ujeuri na katika hali ya udhalilishaji na kashfa kwangu. Mbele ya wateja na wafanyakazi wa Clock Tower Café Iringa alinionyesha kwa sauti ya ukali kama vile mimi ni motto mdogo sana poster yenye maneno “Management reserves the right to refuse admission” iliyobandikwa ukutani. Maneno hayo ya Kiingereza yanamanisha: “Utawala unayo haki ya kumkataza mtu yoyote kuingia”. Na kisha kwa maneno makali akaniambia eti mimi ni mteja mbaya na kamwe hataki kuniona nikiingia au kununua chochote katika mgahawa wake wa Clock Tower Café Iringa na kwamba choo chake sio choo cha umma.

Kwa kweli nilifedheheka sana na kuvunjiwa heshima yangu katika jamii kwa tukio hili na sikuamini kinachotokea. Nimekuwa ninamfahamu Mmiliki huyo wa Clock Tower Café Iringa kwa miaka mingi sana name nimekuwa nikimchukulia kwamba ni jamaa yangu na yeye ananifahamu kwa kina na kazi ninazofanya hapa Iringa na hata baba yake namfahamu na tuna mahusiano mazuri tu kwa miaka mingi. Nimemfahamu Mmiliki huyu wa Clock Tower Cafe Iringa tangu mwaka 2015 nilipokuwa nafanya kazi Iringa na nikiwa mteja wa Iringanet tangu ilipokuwa jingo la Ghorofa pale Mshindo hadi anahamia hapa Barabara ya Dodoma. Kwa upole, nilimsihi na kumkumbusha kwamba tuko ndani ya mwezi wa Ramadhani na si vizuri kunifanyia kitendo cha udhalilishaji lakini alibaki na msimamo wake kuwa hanihitaji mimi wakla wananihusu kuwa wateja wa Clock Tower Café na kwamba niondoke na kamwe nisiingie tena Clock Tower Café Iringa. Ilibidi niondoke kwa aibu kimya kimya kwa unyonge mithili ya mbwa aliyemwagia maji akiogopa hata kubwekawa. Na jambo hili lilinishangaza sana kwa sababu sehemu ya biashara ni sehemu ya umma ambapo kila mtu anaweza kuingia na kutoka.

Kwa kweli tukio hili lininsononesha, kunidhalilisha na kunikumbisha si tukio lilimtokea mmoja wa wagombe Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye alipoingia katika Hotel moja Mjini Dar es Salaam, Uongozi wa Hotel ulikataa hata kumhudumia maji ya kunywa na pia unakumbusha madhila ya siku za ukoloni ambapo watu waafrika licha ya kuwa ndiyo wenyeji wa nchi hii walikuwa wanabaguliwa kwa rangi na hadhi yao na kukatazwa kuingia katika mahoteli au migahawa ya watu weupe. Pale jijini Tanga ilikuwa rahisi mbwa kuingia Planters Hotel lakini si Mwaafrika. Na marehemu Mzee Erasto Mang’enya katika kitabu chake kimoja anaeleza madhila haya ya ubaguzi kwa waafrika pamoja na elimu yake na kuwa mjumbe wa Mamlaka ya Mji alikuwa haruhusiwi kuingia katika Hotel za watu weupe kwa kuwa tu alikuwa ni Mwaafrika.

Na ni jambo la kusikitisha zaidi kuona kuwa baada ya zaidi ya nusu karne ya nchi yetu ya Tanzania na pia Visiwa vya Unguja na Pemba kuwa nchi huru, bado wapo watu kama Mmiliki wa Clock Tower Café Iringa ambao wanaona wanayo haki ya kumnyanyasa Mtanzania na kwamba Mwaafrika kwao ni mtu dhalili asiye na hadhi au haki ya kupata huduma katika biashara zao. Jambo hili halivumiliki hata kidogo na kamwe siwezi kukaa kimya katika hili kuona mtu kwa sababu yeye ni Mwaarabu au Mweupe anayo haki ya kumnyanyasa mtu mweusi katika ardhi ya mababu zake. Je mtu mwenye rangi nyeupe akiingia Clock Tower Café kwenda choo kujisaidia na kasha kutoka bila ya kupata huduma yoyote, je Mmiliki huyu angemsemesha katika kama alivyonisemesha mie kijeuri?

Kama Mtanzania na Mwaafrika naona fahari kuwa nimepata bahati ya kutembelea au kuishi katika nchi zingine za Afrika Mashariki, Ulaya (Norway) na Marekani (USA) lakini katika kutembea kwangu kote huko sijawahi kukatazwa kupata huduma hata ya kujisaidia chooni katika mgahawa au Hotel yoyote kokote kule duniani isipokuwa hapa Iringa katika mgahawa huu wa Clock Tower Café. Kote nilipopata huduma hotelini au mgahawani nimekuwa nikipata heshaima ya utu wangu kwa usawa bila ya kujali hali yangu, rangi yangu au Utaifa wangu hata kama nilikuwa Mwaafrika pekee mahali hapo. Kamwe sijawahi kutokewa na tukio la kubaguliwa na kuonekana dhalili na nisiye na hadhi yoyote isipokuwa jana mbele ya Mmiliki, wafanyakazi na wateja wa Clock Tower Café Iringa ndani ya Mji na nchi yangu. Jambo hili halivumiliki na ni lazima kwa vitendo tulikemee.

Msimamo wangu ni kwamba tukio lililonitokea jana kamwe lisimtokee mkazi au mtu yoyote anayetembelea Iringa. Rai yangu ni kuwa wakazi na watu wote wanaotembelea Iringa kamwe tusiingie kupata huduma Clock Tower Café Iringa kwani Mmili hatuhitaji sisi anao wateja wake wenye hadhi ya kupata huduma ya chakula chake na sio sisi wakazi na watu wanaotembelea Iringa. Tusimmudhi tuwache Mmiliki huyu awahudumie wateja wake anaowataka kwa raha zake.

Tuungane pamoja kusema hapana kwa udhahlilishaji na ubaguzi anaoufanya Mmiliki wa Clock Tower Café katika nchi yetu na mji wetu!

Tafadhali mhabarishe na mwingine!

ZUBERI HAMISI NGODA
Iringa, Tanzania
Simu: +255 655 200 200
E-Mail: advocate.ngoda@gmail.com
May 10 , 2019

#SAYNOTOCLOCKTOWERCAFEIRINGAMISTREATMENTOFCLIENTS#
Ndugu nakuomba uedit huu uzi uwe mfupi Watanzania ni wavivu kusoma thread ndefu. Wao ukiweka uzi wa majungu watausoma hata kwa masaa mawili na kukomenti
 
Ujumbe wako nmekuelewa Kaka vizuri Sana.Ila tatizo nyie waislam huwa mnawaonaga waarabu Kuwa ni Mungu wenu wa pili Ila wao waarabu wanawadharau watu weusi na kuwaona kituko. Pole Ila nafikiri kuna kitu umejifunza kutoka kwa hawa jamaa. Waarabu na Wahindi ni watu tulioishi nao Tanzania miaka mingi Ila Wana Racism. Mimi niliwahi kusoma na Wahindi flani Thailand walikuwa very Racism.
Ilipaswa kuwa very racist
 
Kama unaona umekuwa defermed/kudhalilishwa kafungue kesi....wakili unapaswa kuwa aggressive bana...sio unalia lia.....vitu kama hv sio vya kuweka public hata wateja wako wanaweza kukosa imani na ww....
 
Kuwa mstaarabu na kuwa na roho ya ubinadamu wewe ukibanwa na uharisho katikati ya posta pale city center utajinyea barabarani au utaenda kuomba huduma ya choo ya pale stears? Na unavyohisi unaweza kunyimwa Huduma Ya Toilet sababu Hujanunua chakula chao? Mtu muungwana hawezi fanya hayo daima. Nyie ndio mnaoweza kumpa lifti nyani binadamu mkamuacha njiani sababu tu yeye nae ni mtu kwanini asiwe na gari yake. Jifunze hekima utaish na watu vyema
Huo unaosema wewe ndo sio ustaarabu...mtu ameweka choo kwa ajili ya biashara yake then wewe ambae si mteja unataka ukatumie tena usivyo na akili unaona kabisa eti una haki zote za kukitumia...umeambiwa kile ni public toilet????...kama umezidiwa si kuna vyoo vya kulipia or unafikiri vyoo vya kulipia vimewekwa sababu ya kina nani...na ukiruhusu kila mtu anayebanwa atumie hicho choo unafikiri sehemu zenye mzunguko tena mkubwa wa watu kama huo nini kitakachotokea si watu watageuza public toilet...jifunzeni kuheshimu biashara za watu kama wewe umebanwa nenda kaombe tena omba kabda hujaingia nauhakika kwa binadamu yoyote mwenye akili timamu atakuruhusu but sio tu unafika unaingia wakati wa kutoka unaulizwa unadai mimi huwa nakuja kula hapa alafu unaondoka...tena kama ni mtu mstaarabu kama umeingia bila ruhusa ukitoka jifanye unanunua hata vimaji vidogo vile vyakunywa nauhakika hakuna atakaekuuliza but si kuleta ujuaji...kama we umebanwa kweli siku moja ingia choo cha bank alafu uulizwe useme mi nakuwaga mteja wa hii bank huwa nakuja kuingiza na kutoa hela hapa then uone kitakachotokea...tena huyo mwenye iyo restaurant mstaarabu sana ingekuwa ni mimi li mtu halijulikani lilipotoka linakuja kuingia kwenye restaurant yangu bila ustaarabu na kujiingilia chooni alafu linatoka unaliuliza linakupa majibu kama haya nakwambia ningekufundisha adabu na usingekuja kunisahau...
 
Kanjanja.... Umekuja na Id nyingine kujipa nguvu.

Back
Top Bottom