Jiunge nami kusema hapana kwa udhalilishaji na ubaguzi anaoufanya mmliki wa clock tower café Iringa

Jiunge nami kusema hapana kwa udhalilishaji na ubaguzi anaoufanya mmliki wa clock tower café Iringa

ila mkuu unaweza ukawa na kosa kwa namna flani na pia huyo mmiliki akutumia aproach nzuri kama binadamu mwenzake any way pole sana mkuu
 
Duh pole sana wakili, Umeomba watu wakuunge mkono, waone umedhalilishwa, naona wote waliochangia wanakupinga. Hapo ulipofungua ofisi ni muhimu kuwa na Choo, sasa ukiwa na wateja, wakishikwa na haja huwa unawaelekeza waende wapi.
Hotel ya mwarabu [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kuwa mstaarabu na kuwa na roho ya ubinadamu wewe ukibanwa na uharisho katikati ya posta pale city center utajinyea barabarani au utaenda kuomba huduma ya choo ya pale stears? Na unavyohisi unaweza kunyimwa Huduma Ya Toilet sababu Hujanunua chakula chao? Mtu muungwana hawezi fanya hayo daima. Nyie ndio mnaoweza kumpa lifti nyani binadamu mkamuacha njiani sababu tu yeye nae ni mtu kwanini asiwe na gari yake. Jifunze hekima utaish na watu vyema
Vyoo vya kulipia viko kibao Kanye huko
 
Zuberi Ngoda ni wakili mkongwe, amesoma na kuishi US muda mrefu! Aliporudi Bongo alianza kufundisha sheria ikiwemo SAUT!

Ni Muslim mwenye misimamo mikali. Amewahi kuvunja furniture za mahakama (DLHT) pale Iringa baada ya kuhisi anaonewa.

Huyu jamaa sio legelege au kanjanja kama inavyohisiwa!
Uwakili wake mkongwe hauhusiani na choo Cha mtu kwanza kaamua kukomalia choo Cha mtu Hadi kuamua kuleta Uzi wa kumchafulia biashara yake kisa choo ambacho Sio Cha kwake.Mbona anakomaa Sana na hicho choo Cha mwarabu Ana majini yake kayaweka kwenye hicho choo Cha mwarabu au Nini? Kumchafulia biashara hivi mwarabu wa watu akimtupia majini ya kumtesa huyo wakili atasema kaonewa? SI Kila mtu akionewa anaenda mahakamani aweza mtupia hata dudu baya likamtesa.Huyo wakili hajamtendea haki huyo mwarabu na cafe yake.Very unfair bila kujali kasoma wapi . Property ya mtu Ana right nayo itumikaje huwezi force eti lazima uitumie no.Huyo wakili wenye vyoo kaeni naye mbali msije mpa huduma ya choo mtata mwambieni aende vyoo vya kulipia au akajisaidie ofisini kwake
 
Pole sana mkuu...huyo mmiliki wa clock tower cafe alikosa tu ustaarabu. Angeweza kutumia njia ya busara zaidi kukwambia choo chake siyo cha umma badala ya kukudhalilisha mbele za watu.

Mfano angeweza kukuvuta pembeni akakwambia taratibu badala ya kukushushia heshima mbele za watu.

Tabia za hivi zinakera, mtu haangalii binadamu mwenzake atajisikiaje.

@saynotoclocktowercafeiringamistreatmentofclients
KWeli kabisa hilo jambo ni baya sana kumdhalilisha mtu tena mbele ya watu namna hiyo. KWani sharia inasemaje!
 
KWeli kabisa hilo jambo ni baya sana kumdhalilisha mtu tena mbele ya watu namna hiyo. KWani sharia inasemaje!
Cha mtu Cha hata Kama Ni choo usijifanye kukizoea bila ridhaa yake
 
Umeandika/Umecopy Mkeka mrefu sanaa
Jinsi wabongo walivyo wavivu,watakuwa Wamesoma na ilipofika Juu juu Waka scroll.

In summary

Hilo bandiko Linahusu Ubaguzi (kwa mujibu Wake)
Muandishi Ni mwanasheria/wakili
anaishi Iringa.
Ni mteja mzuri sana wa Mgahawa uliopo Clock Tower Iringa dodoma road.
Akiwa katika harakati Zake za Kuweka mkono kinywaji,alibanwa na haja Sasa kwa Kuwa Ni mteja wa pale na Ni mwez mtukufuku (ramadhani) akaon ngoja nikaji sitili pale (kujisaidia japo hajasema Kama ilikuwa kubwa au ndogo haha yamkini Kubwa).

wakati kashamaliza kuji hajabisha,ghafla mhudumu akamuambia Kuwa "Yeye c Mteja mzuri na anatakiwa asikanyage Tena pale"

na hiyo ndiyo hoja yake Kuwa. aliambiwa asikanyage Tena hapo.bila sababu ya Maana.
so akaona Kuwa ame baguliwa (C unajua Wanasheria tena?!).

Kupitia Ubaguzi wake akatumia ref za wakati wa ukoloni jinsi watu walivyokuwa wanabaguliwa katika nchi yao.

Ni Hayo TU.
Bado lakini hajatuambia ugomvi wake na mmiliki ni nini ?maana hiyo person non grata aliyopewa ina kisa nyuma yake afunguke bwana wakili asiuejua kupangilia story yake !
Aseme tu kuwa anakopa sana anaiba vijiko au akienda msalani anachafua sana au ndio wale soda moja anakaaa siku nzima anakula free wifi
 
huyo mwenye hiyo cafe chama gani ? kama ni chadema hapo Iringa tunaye mwenyekiti wa Kanda ya Nyasa anaitwa Msigwa , ni suala la kumjulisha tu na hatua zitafuatwa
Hahaha hivi kweli kuna shida hapo hadi kuingiza siasa? Huyo mlalamikaji anamatatizo, huwezi kuwa wakili au mwanasheria halafu ukaanza kulazimisha kutumia mali ya mtu bila ridhaa yake. Hicho choo siyo choo cha umma, hicho choo huyo aliyekataa kisitumiwe ndiye mmiliki, ni mali yake. Mlalamikaji angetafuata choo cha umma aone kama kuna mtu angemzuia, eti ana swaumu, kwani inakupa uhalali wa kutumia vitu visivyovyako? uwakili wake pia haumpi uhalali wa kutumia visivyo vyake, alipaswa alilalamikie jiji la Iringa kukosa vyoo vya umma, siyo kulalamikia choo kinachomilikiwa na mtu binafsi. Hicho choo kikijaa mlalamikaji anaweza kumsaidia mwenye café kukivuta uchafu?.
Hakuna ubaguzi wa rangi hapo, sema mlalamikaji kakosa busara. Alipaswa aombe kutumia choo, hakuwa mteja siku hiyo hivyo alipaswa aombe kutumia choo, asilazimishe uteja wa zamani kumpa mamlaka kutumia visivyo vyake. Hivi wateja wote wakikitumia choo hicho kila siku unadhani kitajaa baada ya muda gani? na je kuna mteja kawahi kusaidia kuvuta choo cha café hiyo, akiwemo mlalamikaji?!
 
Uwakili wake mkongwe hauhusiani na choo Cha mtu kwanza kaamua kukomalia choo Cha mtu Hadi kuamua kuleta Uzi wa kumchafulia biashara yake kisa choo ambacho Sio Cha kwake.Mbona anakomaa Sana na hicho choo Cha mwarabu Ana majini yake kayaweka kwenye hicho choo Cha mwarabu au Nini? Kumchafulia biashara hivi mwarabu wa watu akimtupia majini ya kumtesa huyo wakili atasema kaonewa? SI Kila mtu akionewa anaenda mahakamani aweza mtupia hata dudu baya likamtesa.Huyo wakili hajamtendea haki huyo mwarabu na cafe yake.Very unfair bila kujali kasoma wapi . Property ya mtu Ana right nayo itumikaje huwezi force eti lazima uitumie no.Huyo wakili wenye vyoo kaeni naye mbali msije mpa huduma ya choo mtata mwambieni aende vyoo vya kulipia au akajisaidie ofisini kwake
Mimi nimeeleza tu wasifu wa huyu Zuberi Ngoda kwa ufupi, sijaeleza whether he is right or wrong as far as the current situation is concerned!
 
Huo unaosema wewe ndo sio ustaarabu...mtu ameweka choo kwa ajili ya biashara yake then wewe ambae si mteja unataka ukatumie tena usivyo na akili unaona kabisa eti una haki zote za kukitumia...umeambiwa kile ni public toilet????...kama umezidiwa si kuna vyoo vya kulipia or unafikiri vyoo vya kulipia vimewekwa sababu ya kina nani...na ukiruhusu kila mtu anayebanwa atumie hicho choo unafikiri sehemu zenye mzunguko tena mkubwa wa watu kama huo nini kitakachotokea si watu watageuza public toilet...jifunzeni kuheshimu biashara za watu kama wewe umebanwa nenda kaombe tena omba kabda hujaingia nauhakika kwa binadamu yoyote mwenye akili timamu atakuruhusu but sio tu unafika unaingia wakati wa kutoka unaulizwa unadai mimi huwa nakuja kula hapa alafu unaondoka...tena kama ni mtu mstaarabu kama umeingia bila ruhusa ukitoka jifanye unanunua hata vimaji vidogo vile vyakunywa nauhakika hakuna atakaekuuliza but si kuleta ujuaji...kama we umebanwa kweli siku moja ingia choo cha bank alafu uulizwe useme mi nakuwaga mteja wa hii bank huwa nakuja kuingiza na kutoa hela hapa then uone kitakachotokea...tena huyo mwenye iyo restaurant mstaarabu sana ingekuwa ni mimi li mtu halijulikani lilipotoka linakuja kuingia kwenye restaurant yangu bila ustaarabu na kujiingilia chooni alafu linatoka unaliuliza linakupa majibu kama haya nakwambia ningekufundisha adabu na usingekuja kunisahau...
Umeshakariri sababu maisha yako yameshafunikwa na ego na roho chafu. Hakika kama ungetambua kama simba mla nyama siku akizidiwa hula majani, basi hilo suala lisingekuchanganya. Hivyo vyoo vya kulipia haviko kila hatua mbili, na haja ya mtu haina macho kusema ikuhurumie mahali penye vyoo visivyo public. Kinachofuata pale ni ubinadamu ndio hutawala sio biashara. Si sawa mtu kwenda kujisaidia kwenye vyoo vya biashara ila ikitokea dharula ya kibinadamu hekima hutumika mzee. Hilo nalo linahitaji shule?
 
Wakili ana tabia ya kutoflash [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Mkuu ni heri ungeandika Kiswahili maana hapa ushavuruga. Racism ni ubaguzi wa rangi sasa hapo umeona kuna racism yoyote imefanyika?
Kuna different forms of racism.
Google aisee usiongee upupu tu. Elimu ni pana sana uaiwe ignorant.
 
Mkuu jifunze kusubiri muda wakuchimba dawa kama umeshindwa kulipia choo cha stendi.

Acha mazoea na Ofisi za watu, kwanza hujasema kama ulitoa salamu ulipoingia? kwanini usiombe mwanzo kwa vile unajua ni kwa ajili ya wateja ili uruhusiwe.?

Wakili unafeli sana, swala la mistari minne unaeleza page nzima unarudia yale yale
 
kuna watu hapa tanzania wanajiona kama wao ndio wao, hii si mara ya kwanza

Nchi ytu lakini bafo tunyanyasike, pole kak ngoda tuko pamoja huyu awe mfano
 
Tatizo watanzania wengi wachafu sana chooni awe amesoma au hajasoma hawapendi kuflash akimaliza kunya yaan mtu haoni aibu kuacha mavi yake chooni na umekuta choo kisafi mda mwingine unakuta mtu anaenda choon na ka kopo ka nusu kilo ka blueband unajiuliza hv huto tumaji ndo ajitawaze na then aflash inawezekana kweli? Kuna dini moja wafuasi wake ndo wana hizi tabia haijalishi amesoma au hajasoma
 
Mimi nilipe kodi ya pango na mikodi mingine kibao wewe uje unye utoke bila kununua hata maji?Hata mimi sikuelewi
 
JIUNGE NAMI KUSEMA HAPANA KWA UDHALILISHAJI NA UBAGUZI ANAOUFANYA MMLIKI WA CLOCK TOWER CAFÉ IRINGA.

#SAYNOTOCLOCKTOWERCAFEIRINGAMISTREATMENTOFCLIENTS#
Nimekuwa mteja wa mgahawa wa Clock Tower Café uliopo barabara ya Dodoma/Uhuru Avenue katika Manispaa ya Iringa tangu uanzishwe mwaka jana. Nimekuwa nikipata huduma ya chakula katika Mgahawa wa Clock Tower nikiwa ama peke yangu au nikiwa na wageni au wateja wangu kwa kuwa ofisi yangu ya Uwakili ipo jirani tu na mgahawa huu. Hata hivyo jana tarehe 9 mwezi Mei mwaka 2019 limetokea tukio ambalo limenisononesha na kunifanya nisiwe tena na hamu ya kupata huduma ya chakula katika mgahawa wa Clock Tower Café wa hapa Iringa.

Jana ilikuwa ni siku ya tatu/ya nne ya mwezi wa Ramadhan. Nami nilikuwa katika saumu lakinijana wakati natoka mahakamani wakati napita Clock Tower Café nilijisikia haja nikaona niinge ili nijisaidie. Mnamo saan 4.00 asubuhi hivi niliingia Clock Tower Café. Nilipoingia nilimkuta Mmiliki wa Clock Tower Café, Iringa akiwa na mfanyakazi wake wa muda mrefu tangu enzi eneo hilo lilipokuwa Iringanet ikitoa huduma za mtandao wa internet. Kama ilivyo desturi niliwasalimia na kuingia ndani nikapita chooni.

Wakati nataka kutoka Clock Tower Café, niliwakuta Mmiliki na mfanyakazi wake wakiwa eneo lile lile na Mmiliki alinikabili kwa ujeuri na katika hali ya udhalilishaji na kashfa kwangu. Mbele ya wateja na wafanyakazi wa Clock Tower Café Iringa alinionyesha kwa sauti ya ukali kama vile mimi ni motto mdogo sana poster yenye maneno “Management reserves the right to refuse admission” iliyobandikwa ukutani. Maneno hayo ya Kiingereza yanamanisha: “Utawala unayo haki ya kumkataza mtu yoyote kuingia”. Na kisha kwa maneno makali akaniambia eti mimi ni mteja mbaya na kamwe hataki kuniona nikiingia au kununua chochote katika mgahawa wake wa Clock Tower Café Iringa na kwamba choo chake sio choo cha umma.

Kwa kweli nilifedheheka sana na kuvunjiwa heshima yangu katika jamii kwa tukio hili na sikuamini kinachotokea. Nimekuwa ninamfahamu Mmiliki huyo wa Clock Tower Café Iringa kwa miaka mingi sana name nimekuwa nikimchukulia kwamba ni jamaa yangu na yeye ananifahamu kwa kina na kazi ninazofanya hapa Iringa na hata baba yake namfahamu na tuna mahusiano mazuri tu kwa miaka mingi. Nimemfahamu Mmiliki huyu wa Clock Tower Cafe Iringa tangu mwaka 2015 nilipokuwa nafanya kazi Iringa na nikiwa mteja wa Iringanet tangu ilipokuwa jingo la Ghorofa pale Mshindo hadi anahamia hapa Barabara ya Dodoma. Kwa upole, nilimsihi na kumkumbusha kwamba tuko ndani ya mwezi wa Ramadhani na si vizuri kunifanyia kitendo cha udhalilishaji lakini alibaki na msimamo wake kuwa hanihitaji mimi wakla wananihusu kuwa wateja wa Clock Tower Café na kwamba niondoke na kamwe nisiingie tena Clock Tower Café Iringa. Ilibidi niondoke kwa aibu kimya kimya kwa unyonge mithili ya mbwa aliyemwagia maji akiogopa hata kubwekawa. Na jambo hili lilinishangaza sana kwa sababu sehemu ya biashara ni sehemu ya umma ambapo kila mtu anaweza kuingia na kutoka.

Kwa kweli tukio hili lininsononesha, kunidhalilisha na kunikumbisha si tukio lilimtokea mmoja wa wagombe Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye alipoingia katika Hotel moja Mjini Dar es Salaam, Uongozi wa Hotel ulikataa hata kumhudumia maji ya kunywa na pia unakumbusha madhila ya siku za ukoloni ambapo watu waafrika licha ya kuwa ndiyo wenyeji wa nchi hii walikuwa wanabaguliwa kwa rangi na hadhi yao na kukatazwa kuingia katika mahoteli au migahawa ya watu weupe. Pale jijini Tanga ilikuwa rahisi mbwa kuingia Planters Hotel lakini si Mwaafrika. Na marehemu Mzee Erasto Mang’enya katika kitabu chake kimoja anaeleza madhila haya ya ubaguzi kwa waafrika pamoja na elimu yake na kuwa mjumbe wa Mamlaka ya Mji alikuwa haruhusiwi kuingia katika Hotel za watu weupe kwa kuwa tu alikuwa ni Mwaafrika.

Na ni jambo la kusikitisha zaidi kuona kuwa baada ya zaidi ya nusu karne ya nchi yetu ya Tanzania na pia Visiwa vya Unguja na Pemba kuwa nchi huru, bado wapo watu kama Mmiliki wa Clock Tower Café Iringa ambao wanaona wanayo haki ya kumnyanyasa Mtanzania na kwamba Mwaafrika kwao ni mtu dhalili asiye na hadhi au haki ya kupata huduma katika biashara zao. Jambo hili halivumiliki hata kidogo na kamwe siwezi kukaa kimya katika hili kuona mtu kwa sababu yeye ni Mwaarabu au Mweupe anayo haki ya kumnyanyasa mtu mweusi katika ardhi ya mababu zake. Je mtu mwenye rangi nyeupe akiingia Clock Tower Café kwenda choo kujisaidia na kasha kutoka bila ya kupata huduma yoyote, je Mmiliki huyu angemsemesha katika kama alivyonisemesha mie kijeuri?

Kama Mtanzania na Mwaafrika naona fahari kuwa nimepata bahati ya kutembelea au kuishi katika nchi zingine za Afrika Mashariki, Ulaya (Norway) na Marekani (USA) lakini katika kutembea kwangu kote huko sijawahi kukatazwa kupata huduma hata ya kujisaidia chooni katika mgahawa au Hotel yoyote kokote kule duniani isipokuwa hapa Iringa katika mgahawa huu wa Clock Tower Café. Kote nilipopata huduma hotelini au mgahawani nimekuwa nikipata heshaima ya utu wangu kwa usawa bila ya kujali hali yangu, rangi yangu au Utaifa wangu hata kama nilikuwa Mwaafrika pekee mahali hapo. Kamwe sijawahi kutokewa na tukio la kubaguliwa na kuonekana dhalili na nisiye na hadhi yoyote isipokuwa jana mbele ya Mmiliki, wafanyakazi na wateja wa Clock Tower Café Iringa ndani ya Mji na nchi yangu. Jambo hili halivumiliki na ni lazima kwa vitendo tulikemee.

Msimamo wangu ni kwamba tukio lililonitokea jana kamwe lisimtokee mkazi au mtu yoyote anayetembelea Iringa. Rai yangu ni kuwa wakazi na watu wote wanaotembelea Iringa kamwe tusiingie kupata huduma Clock Tower Café Iringa kwani Mmili hatuhitaji sisi anao wateja wake wenye hadhi ya kupata huduma ya chakula chake na sio sisi wakazi na watu wanaotembelea Iringa. Tusimmudhi tuwache Mmiliki huyu awahudumie wateja wake anaowataka kwa raha zake.

Tuungane pamoja kusema hapana kwa udhahlilishaji na ubaguzi anaoufanya Mmiliki wa Clock Tower Café katika nchi yetu na mji wetu!

Tafadhali mhabarishe na mwingine!

ZUBERI HAMISI NGODA
Iringa, Tanzania
Simu: +255 655 200 200
E-Mail: advocate.ngoda@gmail.com
May 10 , 2019

#SAYNOTOCLOCKTOWERCAFEIRINGAMISTREATMENTOFCLIENTS#
Weee Siyo wa Kutulalamikia Hapa

Unakuwaje M/sheria
Una Ofisi Nzuri ila Huna Choo?
Usichukulie Poa Nyumba/Ofisi ni Choo
 
Nimesoma maelezo yako yote na sijaona ni wapi umebaguliwa kutokana na rangi yako. Umekataliwa kutumia choo kama si mteja. Hoja ya ubaguzi wa rangi imekujaje?
 
Nimesoma maelezo yako yote na sijaona ni wapi umebaguliwa kutokana na rangi yako. Umekataliwa kutumia choo kama si mteja. Hoja ya ubaguzi wa rangi imekujaje?
Hata Mimi namshangaa huyu wakili Ana tatizo Sio Siri na hafai kuwa mteja wa hiyo cafe yenye hadhi kubwa.Huyo mumiliki ana haki ya kumpiga marufuku kukanyaga hapo
 
Umeshakariri sababu maisha yako yameshafunikwa na ego na roho chafu. Hakika kama ungetambua kama simba mla nyama siku akizidiwa hula majani, basi hilo suala lisingekuchanganya. Hivyo vyoo vya kulipia haviko kila hatua mbili, na haja ya mtu haina macho kusema ikuhurumie mahali penye vyoo visivyo public. Kinachofuata pale ni ubinadamu ndio hutawala sio biashara. Si sawa mtu kwenda kujisaidia kwenye vyoo vya biashara ila ikitokea dharula ya kibinadamu hekima hutumika mzee. Hilo nalo linahitaji shule?
Eti vyoo havipo kila baada ya hatua mbili...kwa hiyo kuzidiwa kunatokeaga ghafla tu ndani ya sekunde???...na ukijifanya msamaria mwema kwa kila anayezidiwa sehemu kama kariakoo na mzunguko kama ule utafanya usamaria wema kwa watu wangapi mwisho si choo chako cha biashara kitageuka public toilet....hekima gani unataka nitumie wakati hekima ya wewe kuomba kwanza kabda ya kuingia huna...aya umeingia bila kuomba unatoka unashindwa hata kuzuga ujifanye unanunua vimaji vidogo badala yake unajibu eti mimi nanunuaga chakula hapa...jifunze kuheshimu biashara za watu pale sio kwako kama kuna huduma unaiomba omba kwanza utapewa but si unatumia bila kuomba alafu ukiulizwa unaleta ujinga...ukitaka watu wakufanyie ustaarabu na ubinadamu kuwa kwanza mstaarabu wewe
 
Back
Top Bottom