Jiwe la dhahabu lilokamatwa Kenya na kurudishwa nchini kipindi cha JPM umma ulitangaziwa

Jiwe la dhahabu lilokamatwa Kenya na kurudishwa nchini kipindi cha JPM umma ulitangaziwa

Trable

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2023
Posts
1,781
Reaction score
3,288
Hivi mnajua nyinyi maccm na vibaraka wa kumchafua mpigania haki na rasilimali za Tanzania kujaribu kumchafua JPM ni sawa na mtu kuweka mguu wake kwenye pango la siafu?

Mtu aliyekuwa mkweli kutoka moyoni mwake, sote tunakumbuka ile skendo ya Madini yetu ambayo yalidakwa Kenya na kisha kurudishwa nchini, JPM kama angekuwa mwizi si angejichukulia hayo na kuamua kukaa zake kimya?

Eti kirahisi tu mje kuzusha aliiba siju wapi kule,

JPM kaondoka. Lakini matendo yake matukufu kwa nchi hii yanaishi mioyoni mwa watanzania mamilioni kulikoni hata mlio hai
 
Mitano tena kwake
629BCAFB-805E-439B-A437-72F51951B354.jpeg
 
Zile zilikua sanaa tu, code zakishamba sana, jamaa alikua mpori pori one

Yalikamatwa Kenya na vyombo vya kenya pia viliandika kwa hiyo siri haikuwepo.

Hakunaga malaika humu duniani na pia makosa yanayozungumziwa mengi yametendwa na wateule wake yeye anahusishwa kwakuwa ndiye aliyewateua.

Kila serikali ina madudu yake acha yasemwe tu maana hayakusema enzi zake kwa hofu sasa watayasema sasa.

Ana mengi mazuri yatakumbukwa na mabaya yapo yatasemwa.
 
Yalikamatwa kenya na vyombo vya kenya pia viliandika kwa hiyo siri haikuwep...
Mbele ya Maraisi wa nchi? Mbona kufutwa hizo Habari na kutoandikwa kabisa uwezekano huo ni mkubwa sana mkuu kama wameamua lao?

Kaburi la aliyekuwa Gavana wetu enzi hizo aliyetorokea Ughaibuni unalijua lilipo?
 
Kutokujua kabuli la gavana lilipo hakufuti kuwa na yeye Magufuli anaweza kukosea. Hakuwa malaika yule na alikuwa na wateule wengi sana kama bwana bisalo ambao wangeweza kukosea na kama kawaida lawama zitarudi kwa aliyewateua

Two wrongs don't make uo a right.
 
Hivi mnajua nyinyi maccm na vibaraka wa kumchafua mpigania haki na rasilimali za Tanzania kujaribu kumchafua JPM ni sawa na mtu kuweka mguu wake kwenye pango la siafu...
Eti kaiba, kapeleka wapi pumbafu hawa.

Wanachotaka kusema wao hawajidai hawaibi kama yeye ila wanaiba. Aliwaambia kila mtu ale kwa urefu wa kamba yake ya mbuzi
 
Hivi mnajua nyinyi maccm na vibaraka wa kumchafua mpigania haki na rasilimali za Tanzania kujaribu kumchafua JPM ni sawa na mtu kuweka mguu wake kwenye pango la siafu...
Kwa hiyo mtu akitangaza jiwe la dhahabu hawezi kuiba pia?

Logical non sequitar.

Hujasikia majambazi yanaiba na kusafisha jina kwa kutoa sadaka na misaada kwa jamii?
 
Mtu aliyekuwa mkweli kutoka moyoni
Kama kuna dhambi inayomuunguza huko jehanamu huyu jkwe basi ni ile ya kusema uwongo.

Mwanaizaya huyu alikuwa muongo haijapata kutokea.

Mfano.
1. Alisema tunajenga kwa fedha zetu za ndani kumbe anakopa hatari.

2. Alisema nchi yetu umeingia uchumi wa kati kumbe anatupiga fix mithili ya shetani

ACHA AENDELEE KUUNGUA
 
hakuna aliye mkamilifu chini ya jua tatizo la magufuli alikuwa anapenda sifa ili aonekane ni mwema ila nyuma ya pazia alikuwa mkatili sana tutamkumbuka kwa mabaya na wema wake pia
Mie nilimpenda sana kwa sababu alikuwa hawapendi watu wajingawajinga kama wewe,
 
Alishirikiana na Uhuru Kenyata kutengeneza lile Igizo?

Maana waliongea kwa simu, mbele ya Camera. Mpaka mwamba akaomba yule Waziri wa Kenya (Pisi kali) abakie Tz[emoji851]
Mbona hilo dogo umesahau patatu ya makinikia mpaka akaja yule mzungu wa acacia wakafanya press release ikulu baada ya jamaa kufa kabudi anatuambia walikosea? Mzee yule jamaa alikua zaidi ya unavomfahamu .
 
Hivi mnajua nyinyi maccm na vibaraka wa kumchafua mpigania haki na rasilimali za Tanzania kujaribu kumchafua JPM ni sawa na mtu kuweka mguu wake kwenye pango la siafu?

Mtu aliyekuwa mkweli kutoka moyoni mwake, sote tunakumbuka ile skendo ya Madini yetu ambayo yalidakwa Kenya na kisha kurudishwa nchini, JPM kama angekuwa mwizi si angejichukulia hayo na kuamua kukaa zake kimya?

Eti kirahisi tu mje kuzusha aliiba siju wapi kule,

JPM kaondoka. Lakini matendo yake matukufu kwa nchi hii yanaishi mioyoni mwa watanzania mamilioni kulikoni hata mlio hai
Sinema za hovyo ile kutokea Duniani. TZ ilionekana nchi ya wajinga awamu ile. Ati jiwe inakamatwa Kenya, hakuna alikamatwa na kushitakiwa. Uhusiano wa kidiplomasia ukabaki vilevile Na wanaendelea kupeana Tausi wetu. Inawezekanaje?

Wakaona haikutosha wakaja kuokota vichwa vya treni mchana kweupeeee hapo Dar. Aiseee?!
Bado haikutosha, akatokea mtu anaitwa Laizer, yeye ni kuokoaga mawe makubwa Mererani, hakunaga mwingine wa kuokota zaidi yake. Kama siyo ujuha ni nini?! Siku hizi hatuji hata alipo huyo Laizer. Sijui mawe yameishaga Mererani?
 
Back
Top Bottom