JJ Mnyika na Esther Bulaya Live: Star TV

JJ Mnyika na Esther Bulaya Live: Star TV

Asenga wa Pakaya

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2012
Posts
260
Reaction score
60
Ukimtazama usoni utakubaliana nami kuwa huyu sio mnyika yule,Amechoka Uso na masharabu yake yanathibitisha uzee umefika.

Kila alieangalia kipindi cha startv tuongee asbh leo Atakubaliana nami kuwa Bi Esta Bulaya amemuacha mbali sana Mnyika ktk hoja yake ya waraka wa siri wa CCM.

Kiasi Mnyika amechanganyikiwa hadi kukiri wazi kuwa yeye si mtu mwenye msimamo.

"Msimamo wangu wa wazi na msimamo wa haki ni kura ya wazi, lakini baada ya kujua CCM wanaunga mkono kura ya wazi, nmebadili msimamo sasa naunga mkono kura ya siri". Mnyika naona unazeeka sasa

Anataka tuamini kuwa waraka anaodai ni wasiri toka CCM ni wa kweli eti kwa sababu ule waraka wa Mtikila Tarime CHADEMA haijawahi kukaa kikao kuuandaa so hauwezi kukaa kikao kuandaa wa CCM.

Sasa Mnyika kwa uzee wako unadhani mikakati yenu yote huwa mnakaaa vikao vya chama au wenye chama (3) ndio huwa wanaamua??

Nakushauri Mnyika kuanza kuweka akiba kwa kasi kwenye mashirika ya umma Ili yakusaidie uzeeni.

Uzee mwema.
 

Attachments

  • 1393633209559.jpg
    1393633209559.jpg
    78.6 KB · Views: 269
angalao kwa hili nimeanza kumheshimu ingawa itabidi afanye kazi ya ziada ili nimuamini zaidi maana ccm mimi nawaona wamejipanga kuvuruga katiba mpya. wanang'ang'ania kura ya wazi ili waweze kuwadhibiti wale wote waliowateua na wabunge wake, jambo ambalo sio sahihi maana katiba ni ya watanzania wote. toka lini ccm wakataka uwazi?, eti sasa kwenye katiba mpya ndiyo wanataka uwazi, hiki ni kichekesho lakini pamoja na sarakasi zote wanazofanya lakini wajue siku zao za kuwa madarakani ni chache sana.
 
Ester Bulaya ni miongoni mwa wabunge wachache sana wa CCM wanaofanya kazi kwa mashali ya uma,
Ester I love you too..
 
Huwa anaongea kutoka moyoni. Natamani nimuone live huyu dada ili nimpe hongera yake
 
Ester namtabiria kuja upinzani kwanza ni best Yake sana na halima mdee na dada yupo vizuri tena nasikia anamtisha sana wasira anataka gombea Jimbo lake huyu bora hâta awe rais tujue moja kuliko jk
 
Mmmmmh!!!!

Sio hongera tena????

Tatizo lako sijui ni ufahamu mdogo wa lugha ya kiingereza au basi tu nawe uonekane umepost kwenye thread husika..!? Kusema "I love you" haimaanishi kumpenda mtu kimapenzi pekee bali pia upendo uliopitiliza kutokana na mambo anayofanya au aliyofanya. Vile vile hutumika kuelezea upendo kwa watu wako wa karibu kama Baba, Mama, Dada, Kaka na Mtoto.
 
Tatizo lako sijui ni ufahamu mdogo wa lugha ya kiingereza au basi tu nawe uonekane umepost kwenye thread husika..!? Kusema "I love you" haimaanishi kumpenda mtu kimapenzi pekee bali pia upendo uliopitiliza kutokana na mambo anayofanya au aliyofanya. Vile vile hutumika kuelezea upendo kwa watu wako wa karibu kama Baba, Mama, Dada, Kaka na Mtoto.

asante Osambi ze Great kwa kutoa elimu juu ya lugha yetu adhimu ya kiingereza
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom