Kuna anaejua kama kuna mtu katika safu ya JK ambayo anayapitia maswali yatakayo ulizwa na kuyapatia majibu toka kwa wahusika katika serekali? Maanake majibu aliyotoa JK kidogo yanaonyesha hayakutafutiwa majibu fasaha.
Kwa mfano alipoongelea zao la pamba... duu mbona kachemsha sana?
Na swali la binafsi aliloshitukiziwa juu ya vita vya wenyewe kwa wenyewe barani Africa... jibu alilotoa makes me wonder if Africans are serious na matatizo yanayotukumba... kazi yetu sisi ni ku blame our problems on other people....
Shame on our leaders....
Skasuku,naomba nitofautiane na wewe kwenye hili.
Kuhusu jibu la zao la pamba kwa maoni yangu lilikuwa jibu sahihi ila hakuwa constructive na kutoa maelezo ya kina,alijibu swali hilo kirahisi,hata hivyo kwenye hilo nampa pongezi licha ya kwamba hakutoa maelezo enye uzito zaidi kama hadhi yake ya urais inavyotaka. Alichosema kuhusu mfano wa pamba ni pale aliposema kuwa wanunuzi wa pamba walikopa benki kulingana na bei ya mauzo ya wakati huo kabla ya hii credit crunch....Kwamba baada ya hapo,bei zilishuka,na kama bei ikishuka ina maana umeshaingia hasara kwani anticipation yako ilikuwa ni kuuza kwa bei ya juu zaidi,kwa hiyo waliokwisha nunua pamba waliingia hasara kwani hawawezi kuuza kwa bei ya juu ili kupata faida hence incurring loss while still liableto debt repayment....Same thing kwa wakulima kwani bei za vitu kama mbolea nk lazima zilikuwa based on the higher price on the product,kwa mantiki hiyo unakuwa unalipa deni la mkopo kwa hasara ama pengine hata kushindwa kulipa.
Kuhusu kwenye swali la vita ya wenyewe kwa wenyewe,nadhani ni kweli alishtukizwa,hata hivyo he did his best ukilinganisha na vile tunavyomchukulia.
Lilikuwa ni swali la kimtego,na lilikuwa la kumsaidia na ndio maana naamini interview hiyo iliandiwa kwa ajili yake na watu flani wenye manufaa kwa namna moja ama nyingine na yanayoendelea Tanzania...Kwasababu swali aliloulizwa ni kwamba kama mapigano hayo ya wenyewe kwa wenyewe huko Afrika yangekuwa ni ulaya je yangeruhusiwa? Yeye alichotakiwa kujibu kama alitaka kuwa sarcastic kama alivyo intend to be,angemwuliza huyo dada kuwa ni nani hasa huyo anayemaanisha kuwa "Angeruhusu mapigano Europe?" Je alimaanisha wananchi wenyewe wa ulaya ama international insititutions such as UN?
Ukweli ni kwamba ni majukumu ya wenye kupigana pamoja na jumuiya za kimataifa kusuluhisha mapigano ya wenywe kwa wenyewe,ni wazi dada huyo kama ilivyo kwa wengi wenye kutoa maoni yao kuhusu mapigano ya wenyewe kwa wenyewe wana maoni yao tofauti,wengine wanaamini ni udikteta,tamaa za madaraka,ukosekananji wa demokrasia,ufisadi nk. Hayo ndio mambo makuu yenye kuendeleza mapigano ya wenyewe kwa wenyewe Afrika,na katika mapigano hayo kuna matabaka,kwa nchi nyingine ni ya kikabala na nyingine ya kidini nk. alamuradi tu sababu ni zile zile.
Tanzania ni Taifa lililojaribu kuepuka hayo,lakini ni mambo ambayo JK mwenyewe anayaona yakishamiri chini ya utawala wake na yeye kazi yake ni kwenda huko nje ya nchi na kujifanya mzalendo na kudai kuwa na serikali ya Afrika moja,kama huwezi kumake one Tanzania then dream yako ni sawa na day dreaming.....Nimemtizama Mh Rais na nimeshangazwa kweli kweli,yani kuna unafiki wa hali ya juu viongozi wetu wanapokuwa nje ya nchi na wanapokuwa nyumbani unasiktisha.
Kwa kifupi kuhusu hilo swali la mapigano ni kwamba labda angesema kuwa mpigano ya sehemu kama Europe yangeweza kupewa kipaumbele zaidi ya inavyofanyika kuhusu mapigano ya Afrika,mfano halisi ambao hata wazungu hawa wanalimana wenyewe kwa wenyewe ni jinsi walivyo ignore Rwanda genocide na pia Darfur.
Lakini sasa sijui ni kwamba hakulielewa swali ama aliamua kuwa mwoga wa kusema ukweli na kubakia na unafiki kama alivyoundeleza yeye na Bush.
Majibu mazuri kuhusu hayo ya vita ni mawili kwa maoni yangu,either jumuiya ya kimataifa ingeyashughulika mapigano hayo ya ulaya kwa haraka zaidi kuliko inavyofanya kuhusu mapigano ya Afrika,ama sisi kama Afrika tungejitahidi zaidi ya inavyofanywa kwa mataifa mengine duniani kujaribu kutatua tofauti za hao wazungu zenye kupelekea kuleta mapigano ya wenyewe kwa wenyewe,JK alitakiwa aelewe wazi kuwa ni sawa na kuambiwa kama umshindwa kusimamisha mapigano hayo,na bado kuna kuna lawama kuhusiana na hilo,je yeye angefanya nini kama ni ulaya wanapigana?...Na ukweli wa swali hilo ni kwamba dada yule ni kama alimwuliza JK swali kama Afrika ndo ingekuwa Europe na Europe Afrika,je sisi kama Waafrika ngozi nyeusi na utajiri tungewasaidia vipi masikini hao weupe wanaopigana wenyewe kwa wenyewe,yeye alimjibu yule dada kama ifuatavyo "What would you do?"
Hapo inaonyesha kuwa kila mtu ana namna ya kujibu,hata hivyo he should have done better kwasababu jibu lake hilo lime imply kuwa Mh Rais hana clue ya namna ya kuyamaliza matatizo ya mapigano ya wenyewe kwa wenyewe Afrika,ama hata wazo la namna ya kuweza kuepeukana nayo...Ama ata least vyanzo na namna ya kuepukana na such consequences...Ndio maana nadhani wazungu hawashangazwi kwani hakuna kutumia akili yako,ni kuomba tuu! N wao wana assume kama hao viongozi wetu ndio the best material basi sisi sijui ni nini?
Labda alitakiwa aseme ukweli tu,tungeomba na kundendelea kuomba,no solutions but bakuli.