JK Ampeleka Augustino Mrema kutibiwa India?

JK ni noma,yeye anasubiri ukiumwa tu anakununua.

Hapana Mponjoli si kihivyo, huyu ana huruma umesahau kubeneya? lakini wapo na wengine wengi ambao wamesaidiwa na yeye , wengine si wansiasa. Na inawezekana hata BWM alikuwa akisaidia watu , inategemeana tu na kwa jinsi gani umeeleza shida yako na yeye akaichukuliaje. Kuna mshikaji ambaye kwa sasa ni marehemu alikuwa anasumbuliwa na figo ,alihitaji kufanya transplanting, madaktari bongo walikuwa wanamletea zengwe, Alichofanya ni kumtext mzee , japo hamjui lakini alimsaidia kwenda nje na alifanya hiyo transplanting bahati mbaya na hiyo figo ilifail tena alifariki.
 
Huyo ndiyo Mzee wa kiraracha. Kwanza mapene mengine baadaye. Wacha apone aje aendelee kumpigia kampeni JK.
 
Wakuu,
Ugonjwa ni kitu ambacho kinaweza mpata mtu yeyote. Na inapokuja swala la tiba ni haki ya yeyote kupata tiba. Na ni kwa jinsi gani mtu atasaidiwa kupata tiba haijalishi ni nani anamsaidia. Mfano kwenye ile ajali ya waziri mbatia, tuliambiwa Zito alikuwa wa kwanza kutoa msaada maana alikuwa wa kwanza eneo la tukio. Sasa kwanye vitu kama hivi tafadhali tuondoe tofauti zetu za kisiasa. Hili ni swala la kijamii mtu yeyote akipatwa na matatizo ya namna hii nadhani sote tutajumika irrespective of mitazamo yetu ya kisiasa. Ndio maana hata akifariki mtu, waendao kwenye misiba si wa chama fulani tu au wenye mtazamo fulani tu ni sote tunapaswa kujumuika. So kuna mambo ambayo lazima yatuweke pamoja kama jamii.
 

Ni utu wema tu wa JK na anajua wametoka wapi wakiwa mawaziri, Pole ndugu Mrema Mungu akusaidie upone
 
Hakuna anayekataa Mrema asitibiwe na serikali,tunasema kama ili utibiwe lazima ujikombe na kuukana ukweli na kuwasaliti wananchi walio masikini basi msaada huo hauna maana na anayeupokea hana maana vilevile.
 
Kwa hili Mrema anastahili huduma hizo, tena kwa gharama za serikali na sio "JK's pocket money" kama kiongozi mstaafu tena mfia nji hii, ukizingatia alikuwa "naibu waziri mkuu"
 
Ni haki ya kila raia kugharamiwa nje matibabu ambayo hayapatikani hapa nchini. Najua wizara ya afya inao utaratibu kama huo wa rufaa za kwenda kutibiwa nje. Sioni cha ajabu wala siasa yoyote katika hili. Mbona watoto wadogo wasiojulikana katika siasa zozote zile wanapelekwa nje kutibiwa na serikali, sema tu ni kunakuwa na foleni kubwa ya kusubiria. Na hatujui huyo Mrema alipewa hii rufaa lini na kasubiri hii fursa toka lini.

Tupunguze tafsiri zisizo na maana nzuri kwenye kila kitu. Siku hizi hata mwanamke yoyote akipewa cheo kikubwa tu utasikia wakisema ni 'chakula ya JK'. Ujinga mtupu huu.
 
mimi sioni ubay wa mzee wa kiraracha kwenda kutibiwa. maana hata kubenea pia si alipelekwa kutibiwa? tatizo ni hapo atakaporudi. wanahabari pateni tarehe maalum ili pale uwanja wa ndege wa kimataifa mkasikie mambo. hakawii kutangaza kurudi ccm kwa madai kuwa ni chombo kinachowajali maskini.
 
Mungu amjalie afya njema Lyatonga Mrema, akiwa waziri kazi yake ilionekana, ilikuwa ni nzuri na ya mfano, kila nikiona Polisi post namkumbuka
 
kwani kuna ubaya gani akilipiwa na serikali?, nafikili aliyelipa ni serikali na sio JK
 
Mradi tu asijekurudi na kuanza kusema kuwa hata Jimbo la Vunjo anaenda kupitia tiketi ya CCM.

Hivi kuna aina ngapi za Rushwa?
 
So now whatever J.K. Does tends to annoy someone (if not everyone!)? Wait till your Paps falls sick and you can't afford that hard cash to Indian medical services (let alone Apollo Medical Centre 'as quoted'), there now you'll discover what's good and what's bad for you and for J.K.

let him be paid for and get well soon!
 

Mkuu tartiibu! Ukisoma vizuri sana hoja za wakulu katika suala hili utaona kwamba wanajaribu kutafuta fwakti, uhalali na mantiki ya huo msaada kwa Mh. mzee wa Kiraracha. Si suala rahisi la ama kutopendana ama kukosa uzalendo. Hayo ni majibu mepesi sana. Huwezi kusema msaada ukitolewa tushangilie tu bila kuuelewa. Mifano ya hujuma zilizoanza na misaada au ufadhili ni mingi tu. Great thinkers lazima waumize vichwa kidogo kwa mambo kama haya. Kumbuka all that glitters is not always gold. Halafu nani kakwambia kwamba hapa kuna watu "wadogowadogo".
 

Huu ni msaada binafsi wa JK tuseme kwa huruma yake kwa mzee wa Kiraracha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…