JK amteua Prof. Idriss Bilali Mshoro kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya TIRDO

JK amteua Prof. Idriss Bilali Mshoro kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya TIRDO

Mkeshaji

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2011
Posts
4,258
Reaction score
1,416
Salaam wanajamvi,

Habari za uhakika zinasema kuwa Rais Kikwete amemteua Prof. Idrissa Bilali Mshoro kuwa Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya Shirika la Utafiti na maendeleo ya viwanda (TIRDO). Uteuzi huo umeanza tangu tarehe 01.04.2011 na utadumu kwa muda wa miaka mitatu.

Kabla ya hapo Prof. Mshoro alikuwa Makamu mkuu wa chuo cha Ardhi, uteuzi ambao pia ulifanywa na JK mwaka 2007.

Nawakilisha.

=============

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Prof. Idrissa Bilali Mshoro kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda (TIRDO) kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia tarehe 01 aprili, 2011.

Kwa mujibu wa taarifa ya katibu mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Bi.Joyce Mapunjo, Prof. Mshoro alikuwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ardhi tangu mwezi Septemba, 2007 akitokea Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kama Mhadhiri.

Taarifa hiyo imefafanua kuwa Prof. Mshoro alihitimu Falsafa ya Udaktari wa Uhandisi Mitambo (Mechanical Engineering) katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Peterborough cha Uingereza mwaka 1996.

Wakati huo huo, Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Cyril Chami amewateua wajumbe mbalimbali wa bodi hiyo. Walioteuliwa ni Dkt. Hassan Mshinda, mkurugenzi mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Dkt. Roshan abdalla -Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti ya Viuatilifu (TPRI), Bwana Geofrey Msella- Msajili wa Hazina, Wizara ya Fedha na Prof. Brigedia Generali Yadon Kohi- Chief Medical Services Defence wa makao makuu Dar es Salaam.

Wajumbe wengine walioteuliwa ni Bwana Bernard Mchomvu- Afisa Mtendaji Mkuu wa Millennium Challenge Account, Tanzania, Bwana Ali Rajab Mohamed -Mkurugenzi, Wizara ya Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia, Bibi Suzy Lazier- Mkurugenzi, Tanzania Food Processors Association, Bibi Eline Sikazwe- Mkurugenzi, Idara ya Maendeleo ya Viwanda pamoja na Dkt Asifa Nanyaro-Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania.
 
Salaam wanajamvi,
Habari za uhakika zinasema kuwa Rais Kikwete amemteua Prof. Idrissa Bilali Mshoro kuwa Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya Shirika la Utafiti na maendeleo ya viwanda (TIRDO). Uteuzi huo umeanza tangu tarehe 01.04.2011 na utadumu kwa muda wa miaka mitatu.

Kabla ya hapo Prof. Mshoro alikuwa Makamu mkuu wa chuo cha Ardhi, uteuzi ambao pia ulifanywa na JK mwaka 2007.

Nawakilisha.

Upande ule ule wa JK
 
Vijana wa kiislam Tanzania wanahitaji kuthaminiwa na kuona matunda ya miaka 50 ya uhuru wa nchi yao.

Napendeka wanafunzi wote wa vyuo (waislam na wakristu) wafanye maandamano nchi nzima ya kumpongeza Mh Rais Dr JK kwa uteuzi huu.
 
Ukiitwa Idrisa ni Muislam? Kati ya wewe unaelalamika na mh rais nani mdini? Jiangalie mwenyewe

Nyani haoni...
 
Mngejua yanayotokea kwenye level ya utendaji ndio mngekoma, teuzi ni hizohizo
 
JF kufilia mbali. Inajadiliwa dini na si hoja! Hebu wekeni na bodi memba tuwaone. Ndio maana watu wanaamini JF imekuwa kijiwe cha chuki na majungu.
 
Chadema bwana! Yaani nchi hii mnataka iongozwe na wakristo tuu? Mbona hapa ofisni kwangu wakristo ni 95%? Waislamu wakilalamika; mnasema hawakusoma! Wakisoma wakipewa madaraka --oooh udini!

Haya ngoja Rais awe Padri Slaa mfurahi!
 
Back
Top Bottom