Haya ma upuuzi ya udini yanachosha kwakweli... aliyesema urafiki ndio kigezo kikubwa (amepatia sana) lakini kama uwezo ungekuwa unazingatiwa urafiki hau-matter kivile. Nyerere alimuweka shemeji yake Warioba kuwa Waziri Mkuu. Siasa za udini tuwaachie wanigeria huko, sisi nchi yetu ina nafasi zakutosha kukidhi ndoto za wengi tu we nye uwezo. Haiwezekani katika kurusha sarafu ukipata 'bichwa' basi wewe unajipendelea kwasababu nawewe unakichwa, ikipata 'mwenge' (tails) ni sawa kwasababu hamfanani ( the difference here of course being that selecting people for important posts is not like coin tossing but the 50/50 analogy is relevant as far as christianity/Islam is concerned). Muacheni Rais aweke watu anaowaamini, pale watakapo fanya makosa au ikionekana ni wadhaifu ndio wakosolewe na kuawjibishwa katika jamii, vyombo vya habari, kisiasa na ingekuwa vizuri zaidi kisheria. Udini ni upuuzi tuu kwakuwa mwishoe Chenge na Lowassa wangetetewa kama kusingekuwa na jina Aziz kwenye list ya magamba yaliyotolewa (mfano tuu..facts not withstanding).