JK amteua Prof. Idriss Bilali Mshoro kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya TIRDO

JK amteua Prof. Idriss Bilali Mshoro kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya TIRDO

Kwani kosa liko wapi hapo ? kwani muisilamu hana haki ndani ya nchi hii ya Tanganyika ? kweli hapo ndio nakubaliana na mashekh wanaposema mfumo kristo ndio unatawala Tanganyika maana uteuzi wa mtu mwenye jina la kiisilamu tu munapiga kelele, mbona wakiristo muna roho ya husda kisi hicho ? hakuna mulilonalo ila ni kuwapiga vita waisilamu Tanganyika na duniani kote kwa ujumla kumbukeni yana mwisho hayo.
 
Haya ma upuuzi ya udini yanachosha kwakweli... aliyesema urafiki ndio kigezo kikubwa (amepatia sana) lakini kama uwezo ungekuwa unazingatiwa urafiki hau-matter kivile. Nyerere alimuweka shemeji yake Warioba kuwa Waziri Mkuu. Siasa za udini tuwaachie wanigeria huko, sisi nchi yetu ina nafasi zakutosha kukidhi ndoto za wengi tu we nye uwezo. Haiwezekani katika kurusha sarafu ukipata 'bichwa' basi wewe unajipendelea kwasababu nawewe unakichwa, ikipata 'mwenge' (tails) ni sawa kwasababu hamfanani ( the difference here of course being that selecting people for important posts is not like coin tossing but the 50/50 analogy is relevant as far as christianity/Islam is concerned). Muacheni Rais aweke watu anaowaamini, pale watakapo fanya makosa au ikionekana ni wadhaifu ndio wakosolewe na kuawjibishwa katika jamii, vyombo vya habari, kisiasa na ingekuwa vizuri zaidi kisheria. Udini ni upuuzi tuu kwakuwa mwishoe Chenge na Lowassa wangetetewa kama kusingekuwa na jina Aziz kwenye list ya magamba yaliyotolewa (mfano tuu..facts not withstanding).
 
Salaam wanajamvi,
Habari za uhakika zinasema kuwa Rais Kikwete amemteua Prof. Idrissa Bilali Mshoro kuwa Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya Shirika la Utafiti na maendeleo ya viwanda (TIRDO). Uteuzi huo umeanza tangu tarehe 01.04.2011 na utadumu kwa muda wa miaka mitatu.

Kabla ya hapo Prof. Mshoro alikuwa Makamu mkuu wa chuo cha Ardhi, uteuzi ambao pia ulifanywa na JK mwaka 2007.

Nawakilisha.

Well Well:

Idrisa Mshoro ni
- Kolegi Meti (Kama alivyo Mukandara)
- Ni Muislamu (Kama alivyo JK)
- Ni Mtu wa Kujirusha na Mabibi/Wanawake (Kama alivyo JK and Co.)
- Ni Kaka yake Kamishana wa Internal Audit hapo TRA
- E.t.c

Sioni jipya - Nepo-Politics @ work
 
Haya ma upuuzi ya udini yanachosha kwakweli... aliyesema urafiki ndio kigezo kikubwa (amepatia sana) lakini kama uwezo ungekuwa unazingatiwa urafiki hau-matter kivile. Nyerere alimuweka shemeji yake Warioba kuwa Waziri Mkuu. Siasa za udini tuwaachie wanigeria huko, sisi nchi yetu ina nafasi zakutosha kukidhi ndoto za wengi tu we nye uwezo. Haiwezekani katika kurusha sarafu ukipata 'bichwa' basi wewe unajipendelea kwasababu nawewe unakichwa, ikipata 'mwenge' (tails) ni sawa kwasababu hamfanani ( the difference here of course being that selecting people for important posts is not like coin tossing but the 50/50 analogy is relevant as far as christianity/Islam is concerned). Muacheni Rais aweke watu anaowaamini, pale watakapo fanya makosa au ikionekana ni wadhaifu ndio wakosolewe na kuawjibishwa katika jamii, vyombo vya habari, kisiasa na ingekuwa vizuri zaidi kisheria. Udini ni upuuzi tuu kwakuwa mwishoe Chenge na Lowassa wangetetewa kama kusingekuwa na jina Aziz kwenye list ya magamba yaliyotolewa (mfano tuu..facts not withstanding).

Warioba hajawahi kuwa Waziri mkuu wakati wa uongozi wa Nyerere. Ila alikuwa Mwanasheria mkuu wa serikali. Alikuwa Waziri mkuu chini ya Ali Hassan Mwinyi. Sasa ukabila unatoka wapi? Fanya utafiti kabla ya kuongea.
 
Kwani hamna vijana mpaka akaamua kuteua mzee? Nchi hii itaongozwa ma wazee mpaka lini? Tumechoka tunataka damu changa sasa.
Nawakilisha.
Salaam wanajamvi,
Habari za uhakika zinasema kuwa Rais Kikwete amemteua Prof. Idrissa Bilali Mshoro kuwa Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya Shirika la Utafiti na maendeleo ya viwanda (TIRDO). Uteuzi huo umeanza tangu tarehe 01.04.2011 na utadumu kwa muda wa miaka mitatu.

Kabla ya hapo Prof. Mshoro alikuwa Makamu mkuu wa chuo cha Ardhi, uteuzi ambao pia ulifanywa na JK mwaka 2007.
K
 
hahahaha.... yaani kwasababu anajina la kiislam basi hafai!! .. au tatizo ameteuliwa na JK ambaye ni muislam.. hebu amkeni huu udini utawafikisha pabaya na mafisadi ndivyo wanavyotaka, mnabishana kuhusu mambo ya dini wao wanawapa mgongo wanaendelea kula maisha.

hongera Prof.
 
zumbemkuu :

mkuu kabla yake alikuwa prof. IDRISSA KIKULA ambae sasa yupo UDOM, huyu nae ni mzanzibar na anashutumiwa kwa kuweka wanzanzibar wengi kwenye admistration, kuanzia alivyokuwa ardhi hadi asaiv UDOM. kaaaaaz kwel kwel

Kuna watu wanafikia mabo ya udini tu katika kila kitu. Huku ni kuonyesha jinsi walivyofilisika kimawazo. Mwenye post ya hapo juu anadai Prof. idris Kikula ni Mzanzinbari! Huyu ndugu anatoka Makambako kule Njombe na kabila lake ni Mbena. Huo Uzanzibari alipatia wapi?
 
Udini huu utawafikisha pabaya. Ningependa kuuliza Je Prof Idrissa Mshoro hafai kuwa chairman wa TIRDO kwa taaluma yake au dini yake?

Nakupongeza Prof

Mimi namfahamu Prof. Mshoro. Siamini kabisa kuwa ameteuliwa kwenye nafasi hii kwa kigezo cha udini. Kwani kama Mwislamu anazo sifa asiteuliwe tu kwa sababu ni Mwislamu??
 
Is Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi a full time job? Kwa maelezo hayo chini inaonyesha Mshoro anahama kuotoka Ardhi University kwenda TIRDO!

Salaam wanajamvi,
Habari za uhakika zinasema kuwa Rais Kikwete amemteua Prof. Idrissa Bilali Mshoro kuwa Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya Shirika la Utafiti na maendeleo ya viwanda (TIRDO). Uteuzi huo umeanza tangu tarehe 01.04.2011 na utadumu kwa muda wa miaka mitatu.

Kabla ya hapo Prof. Mshoro alikuwa Makamu mkuu wa chuo cha Ardhi, uteuzi ambao pia ulifanywa na JK mwaka 2007.

Nawakilisha.
 
Salaam wanajamvi,
Habari za uhakika zinasema kuwa Rais Kikwete amemteua Prof. Idrissa Bilali Mshoro kuwa Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya Shirika la Utafiti na maendeleo ya viwanda (TIRDO). Uteuzi huo umeanza tangu tarehe 01.04.2011 na utadumu kwa muda wa miaka mitatu.

Kabla ya hapo Prof. Mshoro alikuwa Makamu mkuu wa chuo cha Ardhi, uteuzi ambao pia ulifanywa na JK mwaka 2007.

Nawakilisha.

Wana Jamii forums tuwe tunatoa hoja na kufanya utafiti wa kina kwa habari tunazorusha hapa;mambo ya tabia za kiswahili tuyapunguze.Mada hii tuiache maana sioni umuhimu wake .Watu wazima mnaanza kujadili upuuzi.Naamini nyote ni wasomi mtakuwa mmenielewa.Sihitaji kuchangia katika hili kwani uelewa umekuwa tofauti kati ya waliochangia mada.
 
Kama tutaendelea hivi na maswala ya udini basi ni kansa ya aina yake. Nilidhani kitaalauma Prof. Idrissa Bilali Mshoro amekuwa ni chaguo sahihi, sasa kurukia udini ni jambo la kushangaza. JF msiwe jamvi la poor thinking, na simple minds.

Anaendelea kuwa Makamu mkuu wa chuo cha Ardhi; uenyekiti wa Bodi sio full time position.

Nawakilisha.
 
Tuna vichwa vizuri na wataalamu wengi nchi hii sasa. Kwa nini tunaendelea kulundikiana vyeo na majukumu haya kwa watu walewale?
 
Cha msingi hapa ni taifa kuwa na taratibu za kueleweka ambazo ni competitive ili kuwapata watu wa kuongoza nyadhifa mbalimbali zile zisizohusika na siasa..taifa ambalo linataka ku-evolve kwene right direction linatakiwa lijitoe kwene hizi aina za subjectivities na uswahili wa kuteuana..kwanini nafasi zisiwe competitive watu wakatuma maombi ya kazi na kusimamiwa na ikiwezekana kuwajibishwa wanaposhindwa kukidhi matarajio ya watz? unless kama tunakumbatia mediocrity basi tuendelee na uswahili huuhuu wa 'kuteuana'.
 
Hata Mbuyu ulianza kama mchicha.

masikini Tanganyika wee na Udini. Angalieni msije kuwa kama Nigeria
 
Back
Top Bottom