Mkeshaji, sio kabla ya hapo alikuwa as if kuwa board chair ni full time job, Prof. Mshoro bado ni Makamo Mkuu wa Chuo cha Ardhi. Ila pia kabla ya uteuzi huu kwenda TIRDO, Prof. Mshoro alikuwa ndie Mwenyekiti wa bodi ya VETA mpaka mwezi huu wa April alipomaliza miaka yake 4.
Angalizo!, wana JF tuache kuishabikia hii sumu ya udini kwenye kila teuzi za JK, tufike mahali tuwakubali wateuliwa hawa kwa sifa walizo nazo na sio kwa dini zao. Na kama kuna ukweli dini fulani iliwahi kupendelewa kushika nyadhifa zote za juu kipindi fulani nyuma, then affimative action to redress situation hiyo ni halali kabisa mbele ya wapenda hahi wote!.
Mimi ni Mkristo, tena Mkatoliki, lakini najiamini ni mpenda haki, kama Waislamu wanataka mahakama ya kadhi, wapewe!, si yao na ni ya mambo yao?!, mbona huko nyuma ilikuwepo na hakukuwa na matatizo yoyote?.
Kama wanataka OIC kwa ajili ya maendeleo, tujiunge tuu, mbona Kenya na Uganda zimejiunga na hawana matatizo ya udini?.
Tuwe na upendo wa dhati mioyoni mwetu kwa watu wasio wa dini zetu, tuwatendee haki!.
Pasco.