Jk aongoza maziko ya shekh yahya hussein

Jk aongoza maziko ya shekh yahya hussein

Tulijua atakwenda kwenye huko kwani Arusha na Tarime aliowapiga risasi si aliatabiriwa na huyo huyo Shehe Yahya. Congratulations and big up to kikwete for doing good job.

Contribution ya Shehe Yahya ktk Taifa la Tanzania, uchawi na ushirikina tunaomba michango mingine kama wananchi mnayo. Tunakumbuka maneno ya kishetani ya Shehe Yahya kuhusu Dr Slaa alipokuwa mgombe wa uraisi kwamba atakufa? jk aliishia kuanguka kikwanjani, seem thats jk na ushirikina go hand to hand. Watanzania asilimia kubwa hatutaki kuhusishwa na hawa washirikina na hasa mtu anayejiita kiongozi wa Taifa, ushetani uishie huko huko kwenu na familia zenu na muache kutuunganisha kitaifa.

"Shehe Yahya Hakutabiri kifo chake? au alikuwa amelala na akaondoka haraka haraka? Hii sign kwamba ccm wamezika chama chao leo"

God protect us from such sins and cover us from devil's hand from North to South and West to East
 
Alikuwa wa kwanza kupanda ndege kurudi bongo awah mazishi ya yahya.
 
Katika biblia kuna mfalme fulani alimwendea mwanamke mchawi wa Endori ili amchawie, kwani Mungu alikuwa amemwacha, hakumjibu kwa urim thumim,*manabii wala kumpa ndoto.
Mnamaanisha Jk nae......?
.
 
Tuko pamoja nao ndugu wa marehemu pia 2natoa pole kwa wafiwa wote.M/mungu ilaze roho yake mahala pema pepon.amin
 
Katika biblia kuna mfalme fulani alimwendea mwanamke mchawi wa Endori ili amchawie, kwani Mungu alikuwa amemwacha, hakumjibu kwa urim thumim,*manabii wala kumpa ndoto.
Mnamaanisha Jk nae......?
.

Avatar yako inafanana na ya mdogo wangu.
Gundi ya kubandikia magamba imeondoka, sasa tutarajie magamba kuanza kudondoka yenyewe!
 
mahusiano kati ya jk na shehe yhya ni yapi? na ni nini kilichomtoa huko na kuja huku tofauti na huyu jini mkuu...
 
R.I.P Sheikh Yahya Hussein,Pole Jakaya Mrisho,Poleni Ccm,najua mnaumia sana Mioyoni mwenu Mama Salma Kikwete kwani wewe na watoto wako mlimwamini sana huyu Mchawi.SALMA,RIDHIWAN NA JAKAYA Mliweka sana mbele.
 
Hakuna awezaye kutabiri kifo cha mtu mwingine, hilo ndo funzo kwa kilichotea.
 
Naona huko Namibia alikuwa anaota mazishi ya Shekh Yahaya tuuuu!!!! IMANI HIZI JAMANI!!!!!! MWISHOWE UNAACHA KUFANYA MAMBO YA MAANA AMBAYO KWAYO WATANZANIA WALIKUCHAGUA......KILA SIKU MISIBANI TUUUU!!!!!!
ndege mlimnunulia ya nini?
 
Habari JF members...!
Kama mtaalaam wa Occult Science.
Kifo cha Babu yangu...Marhuum Shaykh Yahya Hasan...imekua huzuni kwa wataalam wa utabiri(Astrology) nchini kwetu na kote Duniani alikojulikana.
Kwa kawaida mtu hufurahiwa kwa mazuri alioyatenda....wengine huchukiwa kwa mabaya alioyatenda.
Nimejifunza mengi kupitia yeye japo sikuwahi kufika nikawa nae ana kwa ana ispokua mwaka 1995/1996 nlifika ofisini kwake magomeni kwa ajili ya kuuliza maswali magumu yalioniingia kichwani mwangu...japo hakunijibu kama nlivyotarajia...ila alinipa mkono wake na kunishauri niende kuwaona wazee katikati ya jiji la dsm...sikufanya hivyo.
Baada ya hapo nliondoka nikiwa na maswali mengi kwanini hakunijibu maswali yangu! Nae ndie nlitaraji angenijibu...lakini sikua na kinyongo moyoni...mwaka mwaka 1999 nlienda clouds nikaongea kuhusu ukweli wa viumbe waitwao Majini nikiwa nae Master T (Taji Liundi) kwenye kipindi chake alicho kiita Appex. Wasikilizaji walipenda mada yangu hiyo. Mwaka 2000 nlienda kuutabiri mwaka kwa kila nyota na matukio yake pia walifurahia wasikilizaji wa Clouds Fm..nlikua nae mtangazaji Fina Mango.
Mwaka huo huo nlianzisha kipindi changu cha (live) unauliza maswali yanayohusu elim ya nyota ...nikawa nawajibu wasikilizaji wa Radio Uhuru nikiwa nae Mtangazaji Masoud Masoud...hadi Radio ikapata umaarufu wa hali ya juu...ikiwa ni pamoja na kuwapata wadhamini wakubwa wawili.1-Tritel
2-Azam Fast Ferry.
Hapo ndipo Marhum Shaykh Yahya alipotaka kunifaham mimi ni nani?
Nilipewa ujumbe nyingi kutoka kwake Marhum Sh Yahya...
Nae alianza kuleta matangazo yake hapo ya kua anasomesha darsa la nyota...magomeni.
Niliotaka kumkumbuka Sh Yahya tangu hapo sikuwahi kumsikia akiongea kwa mafumbo kuhusu mimi...au wataalam wengine. Zaidi alikua akionesha ujasiri wa kile alichokua anakijua/kukifaham yeye.
Pia hakua anajikatia tamaa au kujirudisha nyuma iwapo atakosea yale aliyo amini alitabiri yeye...hali hii inanizidisha upendo niwakumbuke baadhi ya wazee mashuhuri nliowahi kukaa nao pamoja na wakinipa usiya wao kuhusu faida za ilmu na majaribu mbali mbali ambayo mtu/mjuzi unayo weza kukutana nayo...mmoja wa wazee hao ni marhuum Khamis Akida...pia wapo wazee wengi mashuhuri kwa ilmu ni Marhuum shaykh wangu Said bin Aliy bin Umar...ni wengi ....hadi sasa namshukuru Mungu nafuata wasiya zao.
Tumezoea kusubiri mazuri kuanzia mwanzo hadi mwisho...hilo jambo hua muhali kutokea...ni vizuri kuangalia mazuri zaidi na mbaya kuyawacha.Mungu ailaze Roho ya Shaikh Yahya Hasan Mahala pa wema Peponi.Aamiin.
((*Mtabiri Maalim Abalhasan.*)).
 
Tulijua atakwenda kwenye huko kwani Arusha na Tarime aliowapiga risasi si aliatabiriwa na huyo huyo Shehe Yahya. Congratulations and big up to kikwete for doing good job.

Contribution ya Shehe Yahya ktk Taifa la Tanzania, uchawi na ushirikina tunaomba michango mingine kama wananchi mnayo. Tunakumbuka maneno ya kishetani ya Shehe Yahya kuhusu Dr Slaa alipokuwa mgombe wa uraisi kwamba atakufa? jk aliishia kuanguka kikwanjani, seem thats jk na ushirikina go hand to hand. Watanzania asilimia kubwa hatutaki kuhusishwa na hawa washirikina na hasa mtu anayejiita kiongozi wa Taifa, ushetani uishie huko huko kwenu na familia zenu na muache kutuunganisha kitaifa.

"Shehe Yahya Hakutabiri kifo chake? au alikuwa amelala na akaondoka haraka haraka? Hii sign kwamba ccm wamezika chama chao leo"

God protect us from such sins and cover us from devil's hand from North to South and West to East

kufa kila mtu atakufa, na si vyema kumhukumu aliyetangulia. Kwani uzima ni wa Mungu na kifo ni kazi yake. Kuhusu kuanguka kwa jk cdhani ni vyema kuhusisha na ushirikina, kwani hata Dr Slaa alianguka, na akavunjika na mkono, na hiyo tuiteje?, sihani kama tutakuwa tunaendeshwa na hisia na kuropoka itatufikisha kwenye ukombozi na ushawishi tunaoutaka. Wafaham kama mbowe alikuwepo kwenye msiba? Jiulize Sheikh yahya nani asiyemfaham ? Siasa ni watu. Usitoe maneno ya kuwafanya baadhi ya watu watilie shaka mtazamo wako.
 
mbona waislamu wenzio wanasema kutabiri ni sawa na kupiga ramli na hairuhusiwi katika uislamu..wewe kwa nini unafanya hayo?:dance::dance:
 
Maalim kweli hata mimi nakukubali ndigu yangu. Ukweli utabaki ni ukweli na uongo utajitenga na ukweli.
Poleni watabiri kwa kuondokewa na Mnajimu mwenzenu tena mkongwe.
Mungu ailaze roho yake mahala pema peponi. Aamiin.
 
mbona waislamu wenzio wanasema kutabiri ni sawa na kupiga ramli na hairuhusiwi katika uislamu..wewe kwa nini unafanya hayo?:dance::dance:
Ingekua hairuhusiwi ningeacha.
Usiwe unaongea hivyo tena bila kuweka ushahidi uliopewa wa kukataza. Yawezekana uelewa ukawa tafauti.
 
Maalim kweli hata mimi nakukubali ndigu yangu. Ukweli utabaki ni ukweli na uongo utajitenga na ukweli.
Poleni watabiri kwa kuondokewa na Mnajimu mwenzenu tena mkongwe.
Mungu ailaze roho yake mahala pema peponi. Aamiin.
Sote ni waja kwake...na wote tutarejea kwake.
 
Pole Maalim Jumar.

"Al-Ladhīna 'Idhā 'Aşābat' hum Muşībatun Qālū 'Innā Lillāhi Wa 'Innā 'Ilayhi Rāji`ūna".
Wale ambao ukiwasibu msiba husema: Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye hakika tutarejea.

Baqarah: 156
 
Back
Top Bottom