JK: CCM Tujiandae kisaikolojia muundo wa serikali tatu

JK: CCM Tujiandae kisaikolojia muundo wa serikali tatu

Bado nijambo lisilo wazi kwanini ccm wana ogopa sana serikali tatu.Huu nignge penda kuuweka kama mjadala wazi ili kwa michango ya wana jamvi tupate kitu fulani na labda kitakacho wasaidia wale wenye bahati ya kwenda kwenye bunge maalumu la katiba.Wengine nilio pata kuongea nao wanasema wanaogopa TANU isije ikarudi.Wanadhani itakuwa vigumu ccm kuwa moja bara na visiwani.Kimsingi kwa sasa chama kilicho na nguvu bara na visiwani ni ccm.vyama vingine vime fanikiwa kujikita upande mmoja tu.Cuf kwamfano kina nguvu visiwani ilihali bara hakina nguvu sana isipo kuwa maeneo machache.
Chadema kwaupande wake kina nguvu kubwa ya kukubalika bara lakini visiwani hamna kitu kabisa.Hivyo ccm inge penda hali hii alau inge endelea hivihivi ili kiwe na nguvu kote kote chenyewe tu peke yake na hivyo kufanya mwananchi mwenye fikra za kawaida kujengewa taswira kuwa hakuna kama ccm.Pia iko hofu kuwa sasa muungano unafikia mwisho wake kulingana na hamu ya Wazanzibari wengi.Hivyo historia ya Tanu na ccm kuonekana waliasisi kitu kilicho prove failure na kuonekana haya kuwa maono sahihi.Yote hiyo itazidi kuonyesha dira ya ccm ama ya muda mfupi ama mrefu haina mafanikio yoyote na hata kuto aminika mbele ya macho ya Watanzania.Wangependa hata walazimishe hivyo hivyo ilmuradi tu muungano uendelee kuwepo.
Kumbukeni wakati sheri hii ya mchakato wa katiba mpya wakati ina anza walitangulia kusema swala la muungano lisiguswe kabisa.Ili kuwa ni hofu hii hii na sasa yametokea.
Kwa sasa watakalo jaribisha kufanya nikutumia bunge la katiba kuondoa hicho kipengele cha serikali tatu kwa gharama yoyote.Lakini tatizo litakalo wakumba ni ufafanuzi alio utoa Mzee Warioba ulikuwa wandani muno kiasi unaye kuja na sababu zingine kuonekano huna hoja zenye mstakabali wa kitaifa.Alisema Wazanzibari wana ona Tanzania bara au Tanganyika imevaa koti la muungano peke yake huku ikifanya Zanzibar nje ya koti hilo inahangaika na kaserikali ambako haka sikilizwi kimataifa.Mzanzibar mmoja anaye chukua Masters UDOM alisema Zanzibar hakuna shughuli za maana za kiuchumi haata bajeti nzima ya serikali ya mapinduzi ya zanzibar ni Billion 600 wakati huku bara bajeti moja kama Tamisemi ni zaidi ya trion 3.
Hali hiyo wanaiona Wazanzibar ni shauri ya muunganao.Aliongeza msomi huyo wa shahada ya pili ya uongozi wa uma kuwa Zanzibar walikuwa wa kwanza kuwa na Television yao katika afrika mashariki lakini hawanauwezo hata wa kuifanya isikike hata Dar tu.Kama tuliweza maratu baada ya uhuru ina kuwaje baada ya muungano uwezo wote umepotea kabisa.Ni mjadala mpana wana jamvi tuu angalie.
 
CCM hawaogopi serikali tatu.

Umeutrafsiri vibaya ujumbe wa CCM.

CCM inataka serikali mbili. Kutaka serikali mbili sio kuogopa serikali tatu.

Ukitaka shati jeusi sio kwamba unaogopa shati jeupe, la hasha.

CCM inajua how serikali mbili works na kutokana na uzoefu ilio nao wa kusimamia dola inaona serikali mbili ndio njia sahihi itakayowezesha nchi kuendelea kuwa stable.

Hata hivyo swala hili haliko ndani ya mamlaka ya CCM. CCM ni mdau tu, kama walivyo wadau wengine ingawa CCM ni mdau mwenye nafasi ya kipekee ya kujua zaidi hali halisi ya nchi na changamoto za usimamizi wa serikali. Ila CCM imeweka bayana msimamo wake na ushauri wake, iwapo ushauri huo hautafuatwa basi CCM haitaweza kulaumiwa kwa consequences zitakazotokea.
 
Mambo ya kufoji foji huwa yanamwisho kama hivi, sasa serikali tatu haikwepeki, kama ambavyo kifo cha CCM kisivyokwepeka. Matafoji kura hadi mtaachia tu
 
Yanaumbuka haya, si hata vyama Vingi walipinga?tuendelee kuungana tuwatoe hawa wareno.
 
Siasa za Umangimeza na Ukiritimba zimepitwa na wakati. CCM haina Hati miliki ya nchi hii maana imezaliwa mwaka 1977 tu kwahivyo ni Mchanga sana kwenye siasa naomba wafunge midomo yao
 
CCM hawaogopi serikali tatu.

Umeutrafsiri vibaya ujumbe wa CCM.

CCM inataka serikali mbili. Kutaka serikali mbili sio kuogopa serikali tatu.

Ukitaka shati jeusi sio kwamba unaogopa shati jeupe, la hasha.

CCM inajua how serikali mbili works na kutokana na uzoefu ilio nao wa kusimamia dola inaona serikali mbili ndio njia sahihi itakayowezesha nchi kuendelea kuwa stable.

Hata hivyo swala hili haliko ndani ya mamlaka ya CCM. CCM ni mdau tu, kama walivyo wadau wengine ingawa CCM ni mdau mwenye nafasi ya kipekee ya kujua zaidi hali halisi ya nchi na changamoto za usimamizi wa serikali. Ila CCM imeweka bayana msimamo wake na ushauri wake, iwapo ushauri huo hautafuatwa basi CCM haitaweza kulaumiwa kwa consequences zitakazotokea.
mkuu huo ustable wa serikali mbili ni upi? Mbona wananchi kama wenye nchi hawauoni?
 
Tatizo la ccm ni uchama dola, ccm inadhani iko juu ya umma wa watanganyika na wazanzibar! Haiwezekani umma upendekeze serikali tatu halafu kundi la watu (ccm) ling'ang'anie serikali mbili, huu ni usaliti dhidi ya umma! Nina wasiwasi na bunge maalumu la katiba, ccm inaweza kupenyeza wajumbe wakwenda kuchakachua maoni ya wananchi! Watanzania wazalendo na wapenda taifa lao inabidi wawe macho sana katika kipindi hiki! Ccm kwao ni maslahi binafsi kwanza, maslahi ya taifa baadae!
 
Kamuulize Nape ndo anamajibu sahihi, magamba washaambiwa wajiandae kufa na kuzikwa kisaikologia 2015.
 
CCM hawaogopi serikali tatu.

Umeutrafsiri vibaya ujumbe wa CCM.

CCM inataka serikali mbili. Kutaka serikali mbili sio kuogopa serikali tatu.

Ukitaka shati jeusi sio kwamba unaogopa shati jeupe, la hasha.

CCM inajua how serikali mbili works na kutokana na uzoefu ilio nao wa kusimamia dola inaona serikali mbili ndio njia sahihi itakayowezesha nchi kuendelea kuwa stable.

Hata hivyo swala hili haliko ndani ya mamlaka ya CCM. CCM ni mdau tu, kama walivyo wadau wengine ingawa CCM ni mdau mwenye nafasi ya kipekee ya kujua zaidi hali halisi ya nchi na changamoto za usimamizi wa serikali. Ila CCM imeweka bayana msimamo wake na ushauri wake, iwapo ushauri huo hautafuatwa basi CCM haitaweza kulaumiwa kwa consequences zitakazotokea.

Hili la political stability limekuwa sababu ya kimbilio kwa CCM, ndio maana haishangazi kuona historia inatumbia ati serikali ya TANU (alias CCM) ilifuta vyama vingi miaka ile kweusi kulinda political stability, baadaye ikashadadia ati 80% ya Watanzania hawataki vyama vingi kwa vile vitasababisha political unrest. Lakini baada ya kuanzishwa upya kwa demokrasia ya vyama vingi imebainika ya kuwa ni CCM ndio inayoibua chokochoko za migogoro ya kisiasa, kikabila na hata kidini.

Kwenye hili la kung'ang'ania serikali mbili kwa kigezo cha political stability pasina shaka CCM itaafeli pia, maana haihitaji usomi wa kupindukia kuona ya kwamba political stability ya CCM haijasaidia social wala economic development ya Watanzania, badala yake political stability hiyo imeongeza sio tu pengo la wenye nacho dhidi ya wasio nacho, bali pia [political stability hii] imepanua wigo wa tatizo la ajira hasa hasa kwa vijana pamoja na umasikini wa kutupwa kwa Watanzania.

Ni vema Washauri wa CCM watazame upya namna wanavyokishauri chama hiki, maana ushauri wanaokipatia chama sio tu unachochea political instability, bali unatishia usalama wa taifa na kuharibu kabisa maadili ya Kitanzania,kwa mfano imeanza kuwa kawaida kwa vijana kuona fahari ya kukamatwa na mzigo wa 'sembe' huko Mashariki ya Mbali, inaanza kuwa fahari kujihusisha na uhalifu wa kuharibu nyara za taifa wakiwamo tembo. Yapo mengi yaliyozamishwa na turufu hii ya CCM ya political stability. Sasa kama political stability ya CCM ndio inatufikisha hapa, kuna haja gani ya kukumbatia model hii ya utawala?
 
Ni watu wachache sana ndani ya CCM... wenye njaa kali na uchu wa mdaraka na tamaa ya vyeo vya kupewa ndio wanahofia serikali tatu... na kusahau kabisa kuwa CCM na wanachama wake hawazidi milion 7 kama sio 6. Na kwamba kuna watanzania zaidi ya milioni 34 hivi ambao wana mtazamo tofauti.
 
Back
Top Bottom