Nape Nnauye jiandae kisaikolojia.
Katika hali isoyotarajiwa na wengi hasa wale wanaoamini kuwa ni wafia chama ndani ya ccm, mwenyekiti wao Rais Kikwete ametoa rai kwa wanaccm wenzake kujiandaa kisaikolojia kukubali mfumo wa serikali tatu.
My take; Mpaka sasa Ccm hawana uhakika wa kupitisha hoja zao kibabe kama walivyozoea hapo awali ilhali Nguvu ya Umma ikawaacha salama. Nimpongeze kikwete japo kidogo kwa mara ya kwanza kwa kuwa muwazi kwa wanaccm wenzake wasioamini kuwa Ccm inaelekea kuzikwa maana ndio inamalizia kukata roho.
Watakubali tu,chezea nguvu ya umma weye
Acha kutapatapa wewe. JK hajatamka hivyo. hii tabia zenu za kuwawekea maneno yenu viongozi wa CCM ni ushamba uliokithiri.Maneno hayo limeandika gazeti la Tanzania Daima pekee
umebeba nazi halafu huitumii ipasavyo, kwani wao hawana haki ya kutoa maoni?? au wao ni wakenyaHawa jamaa ni wana amin akili yao na maamuzi yao ni sahihi zaidi kuzid wengine, kama ile tume ilikusanya maoni ya wananchi halaf wenyewe wanapinga ni watu waajabu sana
nguvu ya umma ipo ccm mana ndio yenye wabunge 251 huku machadema yana viwabunge 23 tu, hongera ccm kwa kuwa ndio nguvu ya umma halisiWatakubali tu,chezea nguvu ya umma weye
Rais Kikwete alisema mazingira ndiyo huamua jambo fulani hivyo hakuna sababu hoja hiyo ya Katiba kutojadiliwa hivi sasa.
Inaelezwa kuwa Rais alisema licha ya asilimia 80 ya Watanzania kutoukubali mfumo wa vyama vingi mwaka 1992 hoja hiyo ilipita kutokana na mazingira.
Alisema licha ya hofu ya Watanzania juu ya mfumo wa vyama vingi bado mfumo huo umendelea kuwepo mpaka hivi sasa na umeonyesha maendeleo.
Baada ya kauli hiyo wajumbe walianza kupitia kifungu kwa kifungu Rasimu ya Katiba mpya ambapo wengi walipinga muundo wa serikali tatu uliopendekezwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba.
.