JK: CCM Tujiandae kisaikolojia muundo wa serikali tatu

JK: CCM Tujiandae kisaikolojia muundo wa serikali tatu

Hivi hawa wajumbe kutoka Zanzibar, huwa wanachaguliwa kwa vigezo vipi? Au kuja kutuongezea nzi tu?
 
Bora KJ kakumbuka na ya 1992, siku atakapokumbuka na tulivyoikataa EAC ya kuingiza Rwanda na Burundi, basi najua CCM wote watakubali Serikali 3.
hata Nape aje akanushe, JK hawezi kukanusha au kufuata mkumbo kwani muda wake umeisha na anataka kuiacha nchi katika amani, anataka Kura zipigwe na Watanzania waamue
 
Katika hali isoyotarajiwa na wengi hasa wale wanaoamini kuwa ni wafia chama ndani ya ccm, mwenyekiti wao Rais Kikwete ametoa rai kwa wanaccm wenzake kujiandaa kisaikolojia kukubali mfumo wa serikali tatu.

My take; Mpaka sasa Ccm hawana uhakika wa kupitisha hoja zao kibabe kama walivyozoea hapo awali ilhali Nguvu ya Umma ikawaacha salama. Nimpongeze kikwete japo kidogo kwa mara ya kwanza kwa kuwa muwazi kwa wanaccm wenzake wasioamini kuwa Ccm inaelekea kuzikwa maana ndio inamalizia kukata roho.

Cc. Nape, Mwigulu, Shonza, Mwampamba, Ritz, Lizaboni, MwanaDiwani nk.

Source:Magazeti ya Leo
 
Last edited by a moderator:
Katika hali isoyotarajiwa na wengi hasa wale wanaoamini kuwa ni wafia chama ndani ya ccm, mwenyekiti wao Rais Kikwete ametoa rai kwa wanaccm wenzake kujiandaa kisaikolojia kukubali mfumo wa serikali tatu.

My take; Mpaka sasa Ccm hawana uhakika wa kupitisha hoja zao kibabe kama walivyozoea hapo awali ilhali Nguvu ya Umma ikawaacha salama. Nimpongeze kikwete japo kidogo kwa mara ya kwanza kwa kuwa muwazi kwa wanaccm wenzake wasioamini kuwa Ccm inaelekea kuzikwa maana ndio inamalizia kukata roho.

Acha kutapatapa wewe. JK hajatamka hivyo. hii tabia zenu za kuwawekea maneno yenu viongozi wa CCM ni ushamba uliokithiri.Maneno hayo limeandika gazeti la Tanzania Daima pekee
 
habari ya kutuletea toka tanzania daima usirudie tena hilo gazeti huandika tarifa za udaku na kibavicha kama tujuavyo habari za kibavicha huwa hazina maana daima,
 
Hawa jamaa ni wana amin akili yao na maamuzi yao ni sahihi zaidi kuzid wengine, kama ile tume ilikusanya maoni ya wananchi halaf wenyewe wanapinga ni watu waajabu sana
 
Acha kutapatapa wewe. JK hajatamka hivyo. hii tabia zenu za kuwawekea maneno yenu viongozi wa CCM ni ushamba uliokithiri.Maneno hayo limeandika gazeti la Tanzania Daima pekee

Kama ni uongo walicho andika CCM na hasa JK akanushe au waende mahakamani .Kwani kuna ubaya gani na serikali 3 ?
 
Hangaikeni tu lakini nawambia andaeni nguzo na pembasi za kuwalinda 2015 manake mtatikiswa sana mpaka mtachanganyikiwa sana.
 
Hawa jamaa ni wana amin akili yao na maamuzi yao ni sahihi zaidi kuzid wengine, kama ile tume ilikusanya maoni ya wananchi halaf wenyewe wanapinga ni watu waajabu sana
umebeba nazi halafu huitumii ipasavyo, kwani wao hawana haki ya kutoa maoni?? au wao ni wakenya
 
Kwa mujibu wa chanzo kimoja kutoka ndani ya kikao cha Baraza la Kikatiba la Halimashauri Kuu ya CCM ambalo linapitia vifungu vya rasimu ya Katiba Mpya, Rais Kikwete amewataka makada wenzake kujiandaa kwa lolote kama ilivyotokea mwaka 1992.

Rais Kikwete alitolea mfano wa ujio wa vyama vingi mwaka 1992 ambapo idadi kubwa ya wanachama wa CCM walikataa mfumo wa vyama vingi lakini mfumo huo ulipita.

Chanzo: TDaima.
 
Rais Kikwete alisema mazingira ndiyo huamua jambo fulani hivyo hakuna sababu hoja hiyo ya Katiba kutojadiliwa hivi sasa.

Inaelezwa kuwa Rais alisema licha ya asilimia 80 ya Watanzania kutoukubali mfumo wa vyama vingi mwaka 1992 hoja hiyo ilipita kutokana na mazingira.

Alisema licha ya hofu ya Watanzania juu ya mfumo wa vyama vingi bado mfumo huo umendelea kuwepo mpaka hivi sasa na umeonyesha maendeleo.

Baada ya kauli hiyo wajumbe walianza kupitia kifungu kwa kifungu Rasimu ya Katiba mpya ambapo wengi walipinga muundo wa serikali tatu uliopendekezwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba.

.

Inaonekana kuwa ile falsafa ya '...ni upepo tu utapita...' imegoma kufanya kazi kiasi kwamba 'mwenyekiti' anawahimiza wajumbe kukubali kucheza 'muziki' wasioupenda japo kuusikia.

Ni dhahiri kuwa mabadiliko hayaepukiki kwa mujibu wa kipimo maarufu cha wakati na muda
 
chanzo ni udaku wa tzchadema, hah ha ha ahaaaaaaaa, heri kusoma uwazi kuliko tz chadema/daima
 
hongera sana ccm kwa kusimamia katiba yenye maslahi kwa watz wote. serikali mbili ndio mpango mzima
 
jk na ccm kwa ujumla wako tayari kwa lolote kwa chochote hata kama itakuwa serikali saba ccm itashinda na kuendelea kuwatumikia watanzania ambao ndiyo nguzo ya ccm tofauti na chadema ambayo nguvu yake ni ya kikabila na ukanda.
 
Back
Top Bottom