JK: CCM Tujiandae kisaikolojia muundo wa serikali tatu

...Big up JK, jenga ushujaa kwa kuwatosa hao "makasuku wa serikali mbili" kama ulivyowatosa kwenye kuruhusu mchakato wa katiba mpya, jenga legacy yako kwenye hili...
 
Bila ccm nchi itayumba, hekima za nyerere hizo

Ccm ndio dira na mwelekeo wa nchi na maisha ya watanzania, litakalokubaliwa na ccm ndio lenye maslahi mapana kwa watz wote

Ni kweli hiyo ni Nukuu ya Baba wa Taifa, Mwal. J.K Nyerere, lakini alimaanisha C.C.M ipi ? CCM imara au legelege ambayo inapingana yenyewe kwa yenyewe.
 
Augustine Moshi

Hapana humtendei haki bila yeye huuu mchakato usingekuwepo, yeye hakuwahi kuongea na wala kupinga na alipokuja kuongea alisema mchakato uanze.
walio kuw awanapinga ni VIBARAKA wakina WEREMA na yule mama wa Sheria sijuhi nani.

Kwenye jambo kubwa kama la kutoa bungeni msimamo wa serikali kuhusu madai ya kuandika katiba mpya, Waziri wa Sheria na Katiba (Mama Kombani) na pia Mwanasheria Mkuu wa Serikali (Jaji Werema) hawangethubutu kusema bila kupata msimamo wa Rais kwanza.

Mchakato ulianza, not because of him but inspite of him.

I sincerely congratulate him for knowing when to yield.
 
Last edited by a moderator:
Source Radio Deuch well.Katibu wa itikadi na uenezi wa ccm Nape Nauye akizungumza na mwandishi wa habari amesema ccm kama taasisi wamekaa kamati kuu yao mkoani Dodoma na kupitia maoni ya wanachama wao kwa mujibu wa Nape anadai wanachama wao zaidi ya milion mbili(2)wamependekeza muundo huu wa sasa wa serikali mbili kuwa ndio muafaka wa muungano bila hata kuonyesha maudhui ya hicho anachokingangania kuwa ndio muafaka,hata hivyo alipoulizwa swali lingine kuwa haoni kuwa ccm inapingana na maoni ya tume ya katiba ya muundo wa serikali tatu ambayo ndio mawazo ya wengi, amejibu hata wananchi wote waliotoa maoni kwenye tume hawafikii idadi ya wanaccm milioni mbili. Hii ni kwangu mie nadhani ni hatari sana kwa taifa letu kama kweli wajumbe wa ccm zaidi ya 400 waliokutana huko Dodoma wemeona hoja ya muungano wanaweze kuibeba kama alivyowajibia Nape hapo juu basi hii nchi ina ombwe la uongozi kwa sababu tafiti nyingi zilizofanya na majaji wazoefu na waadilifu tangu mwaka 1990 kuanzia kwa tume ya Mh jaji Nyarali imeonyesha mawazo ya watanzania walio wengi wanataka kuwepo na muundo wa serikali tatu,lakini ccm wao wamejikita kwenye hoja dhaifu ya gharama bila kuonyesha uchambuzi wa gharama hizo.
 
Safi JK kwani ndani ya ccm kuna wanafiki wanaoogopa kivuli cha na cha mwal. Wanasema tofauti na wamnavyoamini
 
JK naona amesoma alama za nyakati, katika CCM tupo wengi tunaoona muda wa kuibeba beba Zanzibar umepitwa na wakati.
Kila mundu ave na kwao, kila Taifa libebe jamvi lake.
 
Wana JF;
Ili kuondoa manung'uniko na kero za Muungano uliopo kwa nini CCM isikubali Muundo wa serikali tatu? Wazanzibari wanataka Zanzibar huru yenye mamlaka kamili, Tanzania bara wanataka Tanganyika yao maana Zanzibar angalau wana bunge lao japo bado kuna kero kadhaa za Muungano. Kwani kuna siri gani kwa CCM kung'ang'ania serikali mbili huku wanaona hali si shwari malalamiko hayaishi na ni ya muda mrefu? Mi nadhani jibu la kero zote hizi ni serikali tatu.
Wadau mnaonaje katika hili?
 
Mkuu hata mimi naona hapa serikali tatu yatosha. Maana hata migongano inayotokea bungeni ni kwa ajili ya mtazamo tofauti ya muundo wa muungano. CCM ijiandae kisaikolojia kupata serikali tatu maana ndo mapendekezo ya raia walio wengi mpaka tume ikakubali kuyachukua ili yafanyiwe kazi. Kwa hiyo isione tabu hata kama haikuwa ajenda yao kulikubali hilo.
 

Serikali moja au tatu ndiyo muungano usikuwa na mashaka
 
Hatuwezi kuwa na serikali Moja wakati zimeungana nchi 2 dawa ni tatu hawataki weka mkataba lamuhimu ccm waende ktk tv wazijibu hoja za Zanzibar wanakwepa nini?
 
bora uwaambie wanaweza wakakuelewa ila kwa sasa hawana ujanja serikali tatu inakuja mkuu tena kwa amani bila kumuangosi mtu yeyote
 
Ni kweli kabisa mkuu. Kama serkali tatu ni ngumu au ni gharama kama wanavyodai CCM basi tuwe na serikali moja tu.

Sidhani kama CCM inaogopa gharama tu kuwa na serikali tatu ni lazima wana jambo lingine kubwa zaidi hapo lenye maslahi ya chama zaidi kuliko maslahi ya raia. Mwenye tetesi juu ya ajenda yao nyuma ya hili atupie hapa.
 
Hebu jaribuni kujiuliza ikiwa CCM haitaki serikali tatu na Rasimu ya Katiba ikaja kama ilivyo kura za maoni zitakapo pigwa Zanzibar watapata 2/3 na Je Tanzania bara watapata 2/3.Mimi naamini tusipokuwa makini na kung'ang'ania serikali tatu za CUF na Chadema hatupata Katiba mpya mwisho wa siku tutairudia ile ile ya mwanzo kwani haitapita kabisa.Tuache siasa za kufuata wana siasa wanaowaza ikulu bila muungano.
 
Kama tunataka tuendelee kuwa na nchi iitwayo tanzania, muundo ni wa serikali 3 au moja, vinginevyo tugawane mbao!
 
Hakuna maoni ya ccm wala chadema katiba ni ya watu wote tatizo ya chadema ni kujiona kuwa katiba ni ya kwao.
 
Tuache utoto wa kuwashabikia akina slaa wenye malengo kama ya kagame kwenye nchi hii watanzani ndiyo wenye maamuzi ya katiba yao wala siyo chadema kama wanavyodhani.
 
Tuache utoto wa kuwashabikia akina slaa wenye malengo kama ya kagame kwenye nchi hii watanzani ndiyo wenye maamuzi ya katiba yao wala siyo chadema kama wanavyodhani.

Topic iliyoko mbele yetu umeielewa kweli?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…