JK: CCM Tujiandae kisaikolojia muundo wa serikali tatu

JK: CCM Tujiandae kisaikolojia muundo wa serikali tatu

dosama

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2010
Posts
912
Reaction score
957
LICHA ya Chama cha Mapinduzi (CCM), kutangaza msimamo wa kukataa serikali tatu, Mwenyekiti wa chama hicho, Rais Jakaya Kikwete, amewataka wake wajiandae kisaikolojia kwa mabadiliko yoyote yatakayotokea kinyume na matakwa yao.

Kwa mujibu wa chanzo kimoja kutoka ndani ya kikao cha Baraza la Kikatiba la Halimashauri Kuu ya CCM ambalo linapitia vifungu vya rasimu ya Katiba Mpya, Rais Kikwete aliwataka makada wenzake kujiandaa kwa lolote kama ilivyotokea mwaka 1992.

Rais Kikwete alisema mwaka 1992 idadi kubwa ya wanachama wa CCM walikataa mfumo wa vyama vingi lakini mfumo huo ulipita.

Kiongozi huyo alisema katika kikao hicho cha mwaka 1992 ilikubalika kuwa ‘wengi wapewe wachache wasikilizwe’.

Katika kikao cha jana Kikwete aliwataka wana CCM wajiandae kisaikolojia kwa jambo lolote litakaloamriwa na wananchi watakaopiga kura juu ya rasimu ya Katiba mpya.

Kwa mujibu wa chanzo cha Tanzania Daima, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha Rose Migiro, aliwasilisha na kuchambua upungufu uliopo kwenye rasimu ya Katiba Mpya iliyotolewa hivi karibuni na Tume ya Mabadiliko ya Katiba.

Kutokana na upungufu huo hasa katika mfumo wa serikali idadi kubwa ya makada wa chama hicho ilikubaliana kuendelea na msimamo wao wa serikali mbili.

Mara baada ya Migiro kumaliza, walisimama wajumbe kadhaa na Kikwete kumpa nafasi mmoja wao ambaye alitaka wasiendelee na suala la Katiba mpya liahirishwe mpaka baada ya mwaka 2015.

Inaelezwa kuwa mjumbe huyo kutoka Zanzibar, alijenga hoja kuwa suala la Katiba mpya halikuwa kwenye ilani ya uchaguzi wa chama hicho ya mwaka 2010.

Mjumbe huyo alisema ilani ya chama hicho ilitoa ahadi za ujenzi wa madaraja, barabara, ununuaji wa meli na nyinginezo nyingi ambazo mpaka sasa bado.

Alisema ni busara CCM ikaachana na hoja hiyo mpaka baada ya uchaguzi wa mwaka 2015.

Hata hivyo baada ya mjumbe huyo kutoa hoja hiyo, Kikwete aliwataka wajumbe wajadili mantiki ya rasimu ya Katiba mpya badala ya kufoka au kubishana.

Rais Kikwete alisema mazingira ndiyo huamua jambo fulani hivyo hakuna sababu hoja hiyo ya Katiba kutojadiliwa hivi sasa.

Inaelezwa kuwa Rais alisema licha ya asilimia 80 ya Watanzania kutoukubali mfumo wa vyama vingi mwaka 1992 hoja hiyo ilipita kutokana na mazingira.

Alisema licha ya hofu ya Watanzania juu ya mfumo wa vyama vingi bado mfumo huo umendelea kuwepo mpaka hivi sasa na umeonyesha maendeleo.

Baada ya kauli hiyo wajumbe walianza kupitia kifungu kwa kifungu Rasimu ya Katiba mpya ambapo wengi walipinga muundo wa serikali tatu uliopendekezwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba.

Msimamo wa CCM

Chama hicho tawala tangu kutoka kwa Rasimu ya Katiba kimekuwa kikisisitiza msimamo wa kutambua serikali mbili na si tatu kama ilivyotolewa na Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji mstaafu Joseph Warioba.

Kamati Kuu (CC) iliyoketi Juni mwaka huu iliamua kuipeleka rasimu hiyo kwa wananchi wake kuanzia ngazi ya matawi na kutaka yaundwe mabaraza ya Katiba ya chama hicho.

Hata hivyo CCM ilishaweka wazi msimamo wake kuwa haitokubali muundo wa serikali tatu.

Akizungumza na Tanzania Daima, kabla ya kuingia katika kikao jana jioni, Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, alisema suala la Katiba limewachukua nafasi kubwa.

Alisema suala hilo limechukua muda mwingi kutokana na kupitia kifungu kwa kifungu na mpaka jana saa 10, walikuwa wamepitia vifungu 140.

“Tumeshindwa kuanza kikao cha Halmashauri Kuu (NEC) kama tulivyotarajia kutokana na majadiliano hayo lakini nina imani tutamaliza vizuri.”

Nape alisema suala la kuingizwa kwa uraia wa nchi mbili katika Katiba Mpya nalo liliteka zaidi mjadala.
 
Katika kikao cha jana Kikwete aliwataka wana CCM wajiandae kisaikolojia kwa jambo lolote litakaloamriwa na wananchi watakaopiga kura juu ya rasimu ya Katiba mpya.

Kutokana na upungufu huo hasa katika mfumo wa serikali idadi kubwa ya makada wa chama hicho ilikubaliana kuendelea na msimamo wao wa serikali mbili.

Kikwete ampa nafasi mmoja wa wajumbe toka zanzibar ambaye alitaka wasiendelee na suala la Katiba mpya liahirishwe mpaka baada ya mwaka 2015.

Inaelezwa kuwa mjumbe huyo kutoka Zanzibar, alijenga hoja kuwa suala la Katiba mpya halikuwa kwenye ilani ya uchaguzi wa chama hicho ya mwaka 2010.

Mjumbe huyo alisema ilani ya chama hicho ilitoa ahadi za ujenzi wa madaraja, barabara, ununuaji wa meli na nyinginezo nyingi ambazo mpaka sasa bado.

Baada ya kauli hiyo wajumbe walianza kupitia kifungu kwa kifungu Rasimu ya Katiba mpya ambapo wengi walipinga muundo wa serikali tatu uliopendekezwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba.

My Take:
Wanajua kuwa hawajatekeleza ahadi zao za 2010 na pia msimamo wao wa serikali mbili ndio wanataka uwekwe katika rasimu ya katiba mpya na sasa inafuta ngazi ya chini ambayo huwa haina say wala kutafiti mambo-wao ni kuswagwa tu.
 
safi sana jk kwa kuwashauri wenzako kuwa mabadiliko uwezi yapinga hata kidogo cha msingi hapa ni wana ccm kujianda kuipokea serikali tatu ambayo itabidi iwepo kulingana na mazingira ambayo umeona.....safi sana raisi kikwete kwa kuona mbali na hii inakuwa kama ww ndo umefunuliwa ila wenzako bado wabishi sana
 
Katika hili naamini Mh. Kikkwete hatakubali kurudishwa nyuma na makada wenzake ambao hawaitakii mema nchi hii. Kiukweli katiba nzuri ikipatikana, Mh. Kikwete pamoja na mapungufu yake kama walivyo binadamu wengine, atakumbukwa kama baba wa katiba mpya Tanzania, ikiwa kinyume chake historia itamhukumu.
 
The President has spoken boldly. We support him. Ila kusema atakumbukwa kama Baba wa Katiba Mpya ni kukosa kumbukumbu. Rais alipinga mwanzoni. Ni shinikizo la wananchi wakiongozwa na CHADEMA lilimfanya akona mwanga.

Nampongeza kwamba inapobidi kukubali hukubali. When he can't beat them he joins them. That is as it should be. Ni watu tu kama Njugulu Nchembe ndio hawatambui hilo.
 
Cc Nape bwatubwatu,halafu serikali 3 kiukweli ndo ambazo ziko sasa hivi,Zanzibar raisi wao ni Amiri jeshi mkuu wa vikosi vya zanzibar

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Sarikali tatu ni kama mfuriko, ni muhimu kujiandaa kisaikolojia.
 
Bila ccm nchi itayumba, hekima za nyerere hizo

Ccm ndio dira na mwelekeo wa nchi na maisha ya watanzania, litakalokubaliwa na ccm ndio lenye maslahi mapana kwa watz wote
 
Bila ccm nchi itayumba, hekima za nyerere hizo

Ccm ndio dira na mwelekeo wa nchi na maisha ya watanzania, litakalokubaliwa na ccm ndio lenye maslahi mapana kwa watz wote
"Watanzania wanataka mabadiliko ,wasipoyaona ndani ya ccm watayatafuta nje ya ccm" ,mwl.nyerere hakuishia hapo pia alisemaa!!!! baba.jpg
 
wameshagundua kuwa Warioba anaungwa mkono na CDM kuhusu serikali tatu,na ukigusa CDM umegusa umma,hivyo keshasoma upepo mapema kuwa sio rahisi kwa CCM kuwashawishi wananchi kukataa mfumo wa serikali tatu.
 
The President has spoken boldly. We support him. Ila kusema atakumbukwa kama Baba wa Katiba Mpya ni kukosa kumbukumbu. Rais alipinga mwanzoni. Ni shinikizo la wananchi wakiongozwa na CHADEMA lilimfanya akona mwanga.

Nampongeza kwamba inapobidi kukubali hukubali. When he can't beat them he joins them. That is as it should be. Ni watu tu kama Njugulu Nchembe ndio hawatambui hilo.
Augustine Moshi

Hapana humtendei haki bila yeye huuu mchakato usingekuwepo, yeye hakuwahi kuongea na wala kupinga na alipokuja kuongea alisema mchakato uanze.
walio kuw awanapinga ni VIBARAKA wakina WEREMA na yule mama wa Sheria sijuhi nani.
 
Last edited by a moderator:
Jk.anawasisitiza wanaccm wajiandae kisakilojia,wajiandae kisaikolojia kama hawataki kujiandaa ngoja aje awaachie manyoya!!!!!!!!!!!!! Katika hili lazima awamwage kaamua kusimama upande wa watanzania.
 
Kwa jambo ilo sina budi kumpongeza Kikwete,ila huyu mjumbe toka Zanzibar sidhani kama anaelewa kinachojadiliwa,eti haikuwemo katika ilani ya C.c.m,hivi anadhani nchi hii ni ya C.c.m peke yake?
 
Back
Top Bottom