JKCI: Mwanaume anatakiwa kunywa Bia 2 na mwanamke Bia 1 tu kwa siku

JKCI: Mwanaume anatakiwa kunywa Bia 2 na mwanamke Bia 1 tu kwa siku

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
MWANAUME anatakiwa kunywa uniti mbili za bia sawa na chupa mbili wakati mwanamke anapawa kunywa unit moja ambayo ni sawa na chupa moja ili kuepuka magonjwa yasiyo ambukiza ikiwemo Moyo.

Hayo yamesemwa na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Tatizo Waane ikiwa ni maadhimisho ya siku ya Moyo Duniani. Dokta Waane amesema unywaji pombe kupita kiasi ni miongoni mwa sababu kubwa inayosababisha magonjwa ya moyo.

Sababu zingine zilizotajiwa ni mtindo mbaya wa maisha ikiwemo ulaji na kutokufanya mazoezi. Amesema Pombe inafanya misuli ya moyo kulainika na inapolainika inakosa nguvu na moyo unashindwa kufanya kazi kama inavyotakiwa.

“Lakini unapokuwa na matumizi ya pombe kupita kiasi inachangia tabia nyingine kama mtindo wa maisha utakuwa unakula na ndizi, nyama choma, tumbaku sigara kwa hiyo vitu hiyo ni hatari,’ amesisitiza.
Aidha, amewashauri kwa wale ambao hawanyi pombe wasinywe na kwa wale ambao wanatumia wapunguze matumizi au kuacha kabisa. Dk Waane ambaye pia ni Mkurugenzi wa tiba JKCI amesema wagonjwa wamoyo wanaongezeka ambapo awali walikuwa wanapoke wagonjwa 50 hadi 60 kwa siku na hivi karibuni wagonjwa wamefika 300 hadi 500 kwa siku.
 
Madaktari tunapiga nao mtungi mpaka nane usiku.

Kuna dogo langu ni daktari bingwa kabisa wa figo kwenye gari yake huko si mzinga wa whisky na bia.

Hebu watuache tupoteze mawazo ya tozo hizi.
 
Tatizo binadamu wa siku hizi ni wabishi sana...
 
Niulizie kwa bwana daktari je nikiacha kunywa kwa wiki mbili kisha nikanywa bia 28 kwa siku (Hiyo siku nayoamua kunywa) kuna ubaya? Si amesema bia 2 kwa siku?
 
Back
Top Bottom