JKT kurejeshwa, wazo zuri au limepitwa na wakati?


Kafara,

Sidhani kama kuna mtu hapa anatetea yote ya JKT. Kuna mambo mengi sana ambayo hayakuwa sawa na ndio maana ilikufa. Kwa uzalishaji ule, ilitakiwa kabisa JKT ijitegemee lakini wajanja wakaanza kuiba nk.

Nikiangalia faida na hasara zake, nakuta faida nyingi zaidi na ndio maana kama uchumi unaruhusu mimi ningependa JKT iendelee na nitakuwa tayari kuwaona watoto wangu wanaenda JKT.

Hizi institutions zote zinakuwa na matatizo yake na ndio maana neno CHANGE ni muhimu sana katika muda wote wa uhai wa mwanadamu.
 

Yaani hapa nilitamani huu mfumo wa "thanks" kwenye forum yetu ungeniwezesha kukupa thanks mara 5, maana umetoa muhtasari tosha kabisa.
 
..viongozi wa chama na serikali, pamoja na wakamanda wa jeshi letu, walikuwa wakipitapita kwenye makambi ya JKT kufanya mapenzi na watoto wa kike.

..ma-matron wa JKT wana siri kubwa mno za uchafu na ufisadi uliokuwa ukiendelea. ma-matron walitoa mchango mkubwa kufanikisha ufisadi huo.

..nilitegemea ktk thread hii, Watanzania tutaungana kulaani ufisadi na unyama ule.

..malengo ya JKT yalikuwa kuwaunganisha vijana, na kuwafunda kuhusu umoja na maadili ya taifa letu.

..baadhi yetu wamedai kina dada waliodhalilishwa walikuwa wapenda shushi. wengine wakadai hawakufunzwa makwao na wazazi wao.
..kama madai hayo yana ukweli, basi JKT ilipaswa kuwaweka ktk njia nzuri, na siyo kuwafanya misukule wa ngono.

NB:

..nimepitia JKT na kilichonivutia wakati ule kilikuwa ni mafunzo ya Kijeshi. natamani ningepewa mafunzo makali zaidi na ya muda mrefu zaidi ya miezi 3.

..waalimu, wa-technician, wauguzi, etc etc, wangelitumikia jeshi ktk proffesions zao na siyo kufanyishwa kazi zisizohitaji ujuzi.
 
JokaKuu,

Nchi ya Norway- kutokana na tuhuma hizi za ngono wanawake sii lazima kwenda JKT yao- je unaona ni vyema JKT iwe kwa ajili ya Waume tu Tanzania?

Sasa hizi tuhuma za ngono- zipo mashule ya sekondari, Vyuoni, taasisi za serikali n.k Na huku iweje?
 

Tuhuma za ngono huwezi kuziepuka kwa kuweka wanaume watupu. Kitakachofuata ni kuanza kukamuana wanaume kwa wanaume back to square one!
 
Tuhuma za ngono huwezi kuziepuka kwa kuweka wanaume watupu. Kitakachofuata ni kuanza kukamuana wanaume kwa wanaume back to square one!

Mbona pia kulikuwa na maafande wa kike waliokuwa wanawania vijana wa kiume?

Oljoro kulikuwa na mdada mmoja ulikuwa unapenda kweli vijana. Tatizo la vijana walikuwa hawalalamiki badala yake wanatamba.
 
Mbona pia kulikuwa na maafande wa kike waliokuwa wanawania vijana wa kiume?

Oljoro kulikuwa na mdada mmoja ulikuwa unapenda kweli vijana. Tatizo la vijana walikuwa hawalalamiki badala yake wanatamba.

Mtanzania,

Leo nimecheka mpaka basi! well huyu alikuwa na shetani lake tu la ngono- akina mama wa aina hiyo wapo na sii jeshini tu!

Ila hujafafanua- ina maana na hawa vijana walikuwa wanapenda vya mteremko?

Nadhani % ya wadada kama hao ilikuwa kidogo ukilinganisha na wanaume!
 
WAZO la JKT HALIWEZI KUPITA BILA KUUNGWA MKONO.....! WATANZANIA TUNAOITAKIA MEMA TANZANIA NA VIJANA WAKE, TUSHIRIKIANE HIKI KITU KIRUDI....!
 
JKT kwa mujibu wa sheria kurejeshwa mwaka 2010



My take

Bora irudi manufaa yake ni mengi kuliko matatizo. Bado nakumbuka ule wimbo wangu " Kure kure kwa tinova kure-kure kwa tinovaa, baabaa we na mama tunasonga mwana-KuZimbabweee
 
Afrikaaaaaa Na Towe...... Towe........ Songa Nako Zimbabwe.... Baba Naye Mama Tutasonga Nako-zimbabweeeee....!
je Watanzania Wenye Asili Ya Asia Sheria Hii Itawahusu...?
 
Habari za kulazimishana ni mambo ya totalitarianism, kama watu wana mitkas ya mingo JKT itakuwa kupotezeana muda na maafande tu.

Kama wanataka wafanye kwa hiyari halafu jeshi lijiendeshe kiuchumi, sio kwa handouts za walipa kodi.
 
.... JKT ikirudishwa 2010 kama habari zinavyosema, itabidi waziwezeshe kambi zote kwa mawasiliano ya kisasa, maana kwa jinsi vile vijana walivyozoea mambo ya mitandao hivi sasa, itawawia vigumu sana kuishi bila mitandao ya internet, haswa wanaotoka mjini.

.... kuwawezesha vijana kuwa na mawasiliano kutasaidia pia mtandao wa habari kwa manufaa ya wote, kuhusiana na shughuli na matukio mbalimbali kutoka kwenye maeneo ya kambi.
 
mimi naona Haya mambo ya JKT ni kupotezeana mda tu hakuna lolote huko mlilojifunza huko.

Maana mafisadi yote na majamaa ambayo hayataki maendeleo ya nchi yetu yote yamepita JKT wamejifunza nyimbo tu huko yani aleselema aleja.

Nchi kama Tz kua masikini ni kwasababu ya mijamaa hii inapenda tuwe masikini ,Hata ukiachana na madini Bado Tanzania inauwezo wa kutajirika ndani ya mda mfupi mno.

Ukiangalia jeografia ya TZ yawezekana ni nchi bora wenda duniani kwa kujaliwa maji imezungukwa na maji pande zote ardhi ya kutosha na yenye rutuba.
Na ukiamua kabisa hizo kodi za madini ukanunua ma trekta na vitendea kazi vya kutosha na ukayatumia maji na ukawa dikiteta mstaarabu ndani ya miaka miwili Tanzania inakua nyingine.

Hawa jamaa wamepita JKT na wanatuzuga walikua wanalima na wamejifunza mengi mimi sioni hata moja walilojifunza maana wameshindwa kabisa kugeuza vitu Mungu alivyotujalia ili viwasaidie wana wa Mungu.

Nyie mliopita JKT tuambieni nini mlijifunza huko na mmekitumia kwa manufaa ili kujikwamua na huu umasikini.
Nothing
Badala ya kufikilia kutupa elimu bure mnafikilia JKT kwangu ni NONSENSE
 
Habari za kulazimishana ni mambo ya totalitarianism, kama watu wana mitkas ya mingo JKT itakuwa kupotezeana muda na maafande tu.

Kama wanataka wafanye kwa hiyari halafu jeshi lijiendeshe kiuchumi, sio kwa handouts za walipa kodi.

Absolutely!! Ni udikteta kulazimisha watu kwenda kusurubika pasipo na sababu yoyote.
 
JKT kwa mujibu wa sheria kurejeshwa mwaka 2010




My take

Bora irudi manufaa yake ni mengi kuliko matatizo. Bado nakumbuka ule wimbo wangu " Kure kure kwa tinova kure-kure kwa tinovaa, baabaa we na mama tunasonga mwana-KuZimbabweee

Unfortunately katika mazingira ya siku hizi mimi sikubali vijana wakanyanyaswe kwa lazima tena bila ujira wowote wakati nchi imeshageuka kuwa ya kibepari. Kurudisha JKT ni lazima nchi ikubali kurudisha ujamaa tena. wakati ule JKT ilikuwa inatumika kama namna ya kuilipa serikali kwa fadhila za kuwasomesha vijana wale bure, leo hii mambo si hayo.

Tena katika mazingira ya siku hizi ya ukimwi, nina wasiwasi sana kuwa kuwaweka vijana wetu JKT itakuwa kama kuandika death warrants kwa wengi wao. Nadhani kuwa vijana wengi wanamaliza form 6 siku hizi huwa ni wadogo sana kuliko enzi zile ambapo wengi wao walikuwa wakianza shule na umri wa miaka 8 mpaka 10 na zaidi.
 
Yaani wasichana watakuwa wanapata minmba za maafande! Vijana mtahenyeshwa! Jamani, sijui nisemeje kuhusu hii suala. Tanzania imebadilika. JKT haitufai tena.
 


I truly regret missing it.
 

Kudadeki walahi!! Yaani unalipishwa fadhila kwa kuteswa na kunyanyaswa? Hii kiboko.
 
...hawana idea hao na mawazo yao ya ukomunisti wa 17 century...JKT my azz!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…