JKT waliorudishwa nyumbani watakiwa makambini

JKT waliorudishwa nyumbani watakiwa makambini

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
49,390
Reaction score
152,301
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Meja Jenerali Charles Mbuge, amewataka vijana waliochaguliwa kujiunga na mafunzo ya JKT kwa kujitolea kwa mwaka 2020/2021 na kurejeshwa nyumbani mwezi Februari mwaka huu kurejea makambini.

Kaimu mkuu wa utawala wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Kanali Hassan Mabena, amewaambia wanahabari kuwa vijana hao wanatakiwa kuripoti kwenye makambi waliyopangiwa awali.

Aidha Kanali Mabena amesema kuwa JKT wameingia makubaliano na Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) kwa ajili ya vijana kupata elimu ya vitalu.

Mwezi Februari mwaka huu, Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) alitangaza kuwarejesha nyumbani zaidi ya vijana 12,000, hadi ambapo wangetangaziwa tena.
 
Dah ningeumia Sana Kama Kuruti wenzangu wangesalitiwa mazima
 
Usikute ndo vibaka wa muda huu. Maana matukio ya ukwapuaji yameongeza Dar. Juzi rafiki yangu kapigwa roba na kuchukuliwa simu.
Bora warudishe huko. Pia, next time CDF afanye upembuzi kabla ya kufikia maamuzi.
 
Hamna maelezo zaidi ya hayo isipokuwa kuna link tu ambayo kuiweka hapa ni makosa kwa taratibu za JF.
Sawa mkuu nilidhani na wewe umekuwa kama yule babu Johnthebaptist, yule mzee huwa anakimbilia kuweko vitu hapa hata ambavyo havina maana
 
Sawa mkuu nilidhani na wewe umekuwa kama yule babu Johnthebaptist, yule mzee huwa anakimbilia kuweko vitu hapa hata ambavyo havina maana
Nimefungua link na kuweka habari kamili.
 
Back
Top Bottom