JKT yakanusha suala la kunyanyasa vijana

JKT yakanusha suala la kunyanyasa vijana

Hii nchi imekuwa ya ajabu Sana , imefikia mahali wazazi wanaingilia Hadi program za mafumzo ya jkt. JKT ni jeshi sio shule za msingi au sekondari. JKT waambieni ukweli pale ni jeshi na wanapewa mafunzo ya ujasiri na ukakamavu wa kijeshi , kwa tafsiri nyepesi wanaandaliwa kuwa jeshi la akiba. Haya ndo madhara ya kupeleka watt shule za st. vitoto plus wazazi wanafikra za umayaimayai .

Uko sahihi kabisa kaka,
Ila Wangeweka Utaratibu kama Mtoto hasa wa Kike akifanyiwa Vitendo vya Udhalilishaji ikiwemo Kutaka Kinguvu ngono na Linasemwa s ana hili kuwa lipo, Uwepo utaratibu au namba ya simu ya Kutoa Malalamiko.
Hii litalifanya Jeshi liwe sehemu ya Nidhamu,Otherwise litaonekana tuu kama sehemu ya Wahuni.
Ni kweli kuna Baadhi ya Ndugu watoto wao wa kike wamefanyiwa mambo machafu jadi wengine kurudi na Ujauzito.
so Lazima waweke utaratibu wa wazi Kwa wanafunzi.
 
Mini nimepitia jktl ni k weli enzi zile wadada walikuwa wanalazimishwa ngono Usipotoa walikuwa wanapewa adhabu kali. Tuwe wakwelli

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app

Na Hili wanalificha kwa nguvu kubwa Mnooo.
Wanatakiwa waweke Utaratibu ikiwa Itatokea Vitendo au viashiria hivyo taarifa itolewa kwa Mkuu wa JKT au kamati kwa Simu no….
Jeshi Litakiwa na Nidhamu sanaaa,
 
kuna baadhi wanaitafsiri JKT Mujibu wa sheria sijui ni kama summer Camp hivi

Sasa unaenda jeshi kula kulala au.

Itasemekana mateso endapo anaefanyiwa ni raia ila ukiwa umeenda ukianzia Uzalendo kuipitia Kuruta kwenda ServiceMen/Girls ndio mafunzo ya kijeshi

2018 mujibu tumepiga na iko fresh tu miezi mitatu unarudi home umenyooka vizuri tu
 
Mkuu kama ni Sheria ni Vema mtoto akaenda Sema Cha Msingi,Mkuu wa JKT anatakiwa aseme wazi kuwa Vitendo vya Kudhalilisha haswa watoto wa kike ikitokea wapige simu fulani au watoe taarifa sehemu fulani,Hii itasaidia sanaa kuliheshimisha Jeshi na Kuondoa woga hasa kwa watoto wa Kike.
Wahindi na Waarabu wameshika uchumi wa nchi yetu, huwezi wakuta watoto wao huko.

Huo muda bora wanafunzi wangepelekwa hata VETA
 
Wazazi wengine wana vijana wawili hata watatu..hizo hela za maandalizi na nauli zinatoka wapi?
Ni nini thamani ya vijana kwa nchi yao? Kama vitu vidogo kwa serikali lazima wazazi wagharimie.
Mimi kinachonishangaza ni pale mtoto anapangiwa kureport kambi fulani ya jeshi eti aje na vitu kadha wa kadha ni kama mzazi unampeleka mtoto boarding school kwanini serikali isigharamie badala ya kuagiza hivyo vibukta ambavyo mnataka visiwe na zipu kama serikali inaona hayo mafunzo yana tija!
 
Wanawake kutumika kingono lipo afande akinyimwa basi madoso kombania nzima hadi muhusika,ili jambo wapo walioondoka na maradhi jkt na walienda salama hata vikosini walikuwa viongozi wa Kambi walikuwa wakiwasihi wadada kuripot maovu kama hayo na kusema mtaondoka na maradhi msipokuwa makini,hili jambo lipo, serikali Iliangalie Sana kwa umakini na vitisho kwa kujenga ni kuwatia hofu watoto

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu kama ni Sheria ni Vema mtoto akaenda Sema Cha Msingi,Mkuu wa JKT anatakiwa aseme wazi kuwa Vitendo vya Kudhalilisha haswa watoto wa kike ikitokea wapige simu fulani au watoe taarifa sehemu fulani,Hii itasaidia sanaa kuliheshimisha Jeshi na Kuondoa woga hasa kwa watoto wa Kike.
Hii kitu haitawezekana milele hapa Tanzania. Kuweka hizo taratibu za kuripoti ovyo taarifa chafu za wanajeshi wetu ni kulipaka matope jeshi letu lote na kuliua kabisa. Jeshi letu huwa halikosei na halikoselewi!!

Wewe fahamu tu, jeshi ni kichaka cha kila uovu kinachotunzwa na taifa ili kulinda maslahi ya watawala.
 
Ukitaka kujua jambo fulani ni salama au sio salama, wewe angalia kama watoto wa viongozi kama wanajishughulisha nalo.
Binti wa kiongozi gani wa juu wa serikali anakwenda JKT?
 
JKT raha sana enzi zetu tulipiga mwaka bila hivyo No higher education, No employment na watu walikuwa wanafuatiliwa hadi maofisini wale waliopaswa kwenda kwa mujibu wa sheria wakajongo.
Mwaka Gani huo?
 
Kijana mpeleke akavutishwe bangi
Binti mpeleke akawe chakula ya maafande

Kuvuta bangi ni chaguo la mtu binafsi bro ,madogo wanavuta bangi kuanzia nyumbani kila mahali. Jkt hawakufundishi hivyo vitu unless umetaka mwenyewe
 
Nachofurahi ni kua mnajifanya kutupa ushauri tusiotaka, si mpeleke watoto wenu, ebo! Kwani mnakosa nini watoto wetu wakiwa legelege????
 
Unapotosha
Naungana nae siwezi peleka mwanangu huko ni ujinga mkubwa , hakuna program tanzania iliyo wahi kutekelezwa kwa usahihi tanzania ni blah blah nyingi sana nchi hii mambo mengi ni risk tu.

Watu wametafuta uchochoro kwa kupitishiwa budget kubwa na kupitisha pesa chafu kupitia prigram hii

Uzalendo ungekuwepo kusinge kuwa na wizi wa mabilioni unao fanywa na hao hao wanapigia kampeni uwepo kwa mafunzo kwa mujibu.

NASEMA : HAKUNA UZALENDO WA KUFUNDISHWA UKUBWANI BALI NI MAIGIZO YA UZALENDO
 
Nchi ni yetu sote.

Hata ningekuja mimi, nisinge sema kweli kuna unyanyasaji wowote.

Muhimu ni jeshi letu lichunguze na kuchukua hatua.

Tulio pitia JKT humu tupo wengi.

Naunga mkono yale mafunzo ya JKT. Lakini mabinti walindwe, wazazi tusiwe na mashaka mashaka na hilo linawezekana.
 
JKT kama viongozi wasipokuwa makini vijana wataambukizwa sana HIV.
 
Hii nchi imejaa upumbavu kupitiliza. Ni mabinti wa maskini tu wanaolazimishwa kwenda kubakwa huko kwenye makambi ya kipuuzi ya JKT na maafande wavuta bangi na kuwaambukiza UKIMWI. Ingekuwa watoto wa Rais Samia na wanasiasa ŵengine nao wanakernda JKT, haya makambi ya ngono yangeishafutiliwa mbali.
 
Back
Top Bottom