JKT yatangaza majina ya vijana waliohitimu Kidato cha Sita 2020 wanaotakiwa kujiunga na JKT kwa Mujibu wa Sheria

JKT yatangaza majina ya vijana waliohitimu Kidato cha Sita 2020 wanaotakiwa kujiunga na JKT kwa Mujibu wa Sheria

Ushauri wa bure kwa madogo ni kwamba wakienda huko wabaki huko wasije kuomba vyuo. Yaani utasoma chuo kisha utasota weeeeeeeeee mpaka ujute. Jamaa zangu waliobaki washamaliza kozi monduli na vyeo juu. Naishia kuwaona kwenye status wakisafiri kupiga kozi huko nje ya nchi. Na mimi niliyejikuta msomi nipo hapa naandika comment kwa jf freebasics.😂😂.

NB: MTOTO WA KIKE ASIENDE.
 
Hivyo vitu vya kwenda navyo tulikuaga tunavikuta huko, nashangaa kipindi hiki wanatakiwa waende navyo hadi nauli hivi kuna posho kweli siku hizi, What's happening with mama Tanzania???
 
Hivi huwa wanaenda pamoja na wale wa kujitolea kwa intake moja lakini Hawa wanakuwa kwa miezi mitatu tu...au Hawa wanakuwa group special linalohusu waliomaliza six tu?
 
JKT ni kuwapotezea muda vijana.

Mafunzo ya JKT hayajawahi kua na maana yoyote.

Kwenda kufundishwa kukesha usiku kucha, sijui kugalagala kwenye matope eti ndio uzalendo sijui ukakamavu.

JKT kuwapotezea muda vijana, muda amvao wangeweza kuzalisha au kufanya mambo ya maana kwenye maisha yao.

JKT badala ya kufundisha watu ujuzi wanaenda kufundisha watu kukesha, kumwagilia bustani, sijui kufanya ujinga gani mwingine eti ndio uzalendo.

Una point
 
jeshi ni amri tu, malalamiko utayapeleka wapi?

Wangekua na mfumo nje ya kambi, basi angalau wafanyie kazi tuhuma hizi hata kama hazijafikishwa rasmi. Maana ipo siku hii habari itakuja kuibuka na kulichafua sana jeshi letu
 
JKT ni kuwapotezea muda vijana.

Mafunzo ya JKT hayajawahi kua na maana yoyote.

Kwenda kufundishwa kukesha usiku kucha, sijui kugalagala kwenye matope eti ndio uzalendo sijui ukakamavu.

JKT kuwapotezea muda vijana, muda amvao wangeweza kuzalisha au kufanya mambo ya maana kwenye maisha yao.

JKT badala ya kufundisha watu ujuzi wanaenda kufundisha watu kukesha, kumwagilia bustani, sijui kufanya ujinga gani mwingine eti ndio uzalendo.
Kuna vijana kibao wapo mitaani na wanapoteza muda kuliko hata hao wanaokwenda jkt.

Sent from my SM-A5100 using JamiiForums mobile app
 
Hivi huwa wanaenda pamoja na wale wa kujitolea kwa intake moja lakini Hawa wanakuwa kwa miezi mitatu tu...au Hawa wanakuwa group special linalohusu waliomaliza six tu?
Hapana kila mtu kivyake..na Kama unataka kwenda sikushauri ufanye hivyo
 
Hivyo vitu vya kwenda navyo tulikuaga tunavikuta huko, nashangaa kipindi hiki wanatakiwa waende navyo hadi nauli hivi kuna posho kweli siku hizi, What's happening with mama Tanzania???
Usishangae..zile hela zilizokuwa zinatolewa kwa ajili ya hayo yote alivoingia jamaa akazipiga stop,zikawa allocated kununua bombardier na kujenga flyover
 
Nasikia suala la kupigana miti kimasihala huko ni jambo la kawaida sana. Jamani kuna ukweli wowote hapo?
 
Dah! nakumbuka kipindi naenda 832 kj nilitoka na begi dogo la mgongoni ndani likiwa na tracksuit moja na sweta lake(hii nilivaa siku za uzalendo peke ila baada ya intro sikuwahi ivaa tena [emoji23]), boxer 2 ,pamoja,raba pair moja vingine kama pitshort, green t-shirt,combat full(karanga) na boots zake tulipewa jeshini huko huko pamoja na posho ya 50,000/= kila tarehe 28 ya kila mwezi .Hapo ni 2016 op magufuli intake ya kwanza .
Maajabu baada ya hapo mambo yaka change , naona vijana wanaji nunulia kila kitu na posho sidhani kama wanaijua [emoji23][emoji23][emoji23].

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom