JKT yatangaza majina ya vijana waliohitimu Kidato cha Sita 2020 wanaotakiwa kujiunga na JKT kwa Mujibu wa Sheria

JKT yatangaza majina ya vijana waliohitimu Kidato cha Sita 2020 wanaotakiwa kujiunga na JKT kwa Mujibu wa Sheria

Hivi kama wahitimu wa kidato cha sita walikuwa ni wengi zaidi ya hao wachache waliochaguliwa kujiunga na JKT kwa mujibu wa sheria wale ambao hawajachaguliwa wanakuwa wamepata bahati ya kutojiunga kabisa? Na ni vigezo gani utumika kuwachagua hao wachache? Na kama kuna aliyechaguliwa kujiunga na akaamua kutokwenda na kukaa nyumbani kama wale ambao hawakuchaguliwa uwa kuna adhabu yoyote atakayopata huko mbele ya safari?
 
JKT linawataka vijana hao kuripoti wakiwa na vifaa vifuatavyo.

1. Bukta ya rangi ya ‘Dark Blue’ yenye mpira kiunoni (lastic), iliyo na mfuko mmoja nyuma, urefu unaoishia magotini, isiyo na zipu.

2. T-shirt ya rangi ya kijani (Green Vest)

3. Raba za michezo zenye rangi kijani au blue.

4. Shuka mbili za kulalia zenye rangi ya blue bahari.

5. Soksi ndefu za rangi nyeusi.

6. Nguo za kuzuia baridi kwa waliopangiwa mikoa yenye baridi.

7. Track suit ya rangi ya kijani au blue

8. Nauli ya kwenda makambini na kurudi nyumbani.

Be, jesi lisisile - Wanaenda na vifaa vyao hata supi sa jesi serikali imesindwa?
 
Hivyo vtu si huwa vnatolewa kulekule au serekal haina pesa? Aah ila Kurutu ni mdudu acha ajinunulie tu
 
Enzi zetu tulirudishiwa nauli na kupewa ya kuondokea na kila kitu
Hope watafanya hivyo watu wasiwakatishe tamaa wadogo wetu kuna kitu watajifunza kwa muda mfupi wa mafunzo hao tusibeze
 
pumbav kabisa yani mimi nisote miaka yote hiyo alaf bado na wao wanisoteshe tena kwa vitu visivyokuwa na faida yoyote ile....huko ni kupoteza muda na kukatisha ndoto za watu...miafrika ndivyo ilivyo..
 
Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), limechagua vijana waliohitimu elimu ya sekondari kidato cha sita kwa mwaka 2020, kutoka shule zote za Tanzania Bara kuhudhuria mafunzo ya JKT kwa mujibu wa Sheria.

Sanjari na uchaguzi huo, JKT limewapangia makambi watakayo kwenda kupatiwa mafunzo na wanatakiwa kuripoti makambini kuanzia tarehe 24 hadi 27 Julai 2020. Aidha, mafunzo hayo yatafunguliwa kuanzia 01 Agosti 2020.

Vijana waliochaguliwa wamepangiwa katika kambi za JKT Rwamkoma - Mara, JKT Msange - Tabora, JKT Ruvu - Pwani, JKT Mpwapwa Dodoma, JKT Mafinga - Iringa, JKT Mlale - Ruvuma, JKT Mgambo na JKT Maramba -Tanga, JKT Makuyuni - Arusha, JKT Bulombora, JKT Kanembwa, na JKT Mtabila - Kigoma, JKT Itaka - Songwe, JKT Luwa na JKT Milundikwa - Rukwa, JKT Nachingwea - Lindi na JKT Kibiti- Pwani na Oljoro JKT- Arusha.

Wahitimu wenye ulemavu wa kuonekana kwa macho (physical disabilities) waripoti katika kambi ya JKT Ruvu iliyopo Mlandizi mkoani Pwani ambayo ina miundombinu ya kuhudumia watu wa jamii hiyo.

Aidha, kutokana na ugonjwa wa Homa kali ya Mapafu (COVID-19) Nchini, Tahadhari za kuzuia maambukizi ya ugonjwa huo zitachukuliwa kipindi chote vijana watakapokuwa makambini.

JKT linawataka vijana hao kuripoti wakiwa na vifaa vifuatavyo.

1. Bukta ya rangi ya ‘Dark Blue’ yenye mpira kiunoni (lastic), iliyo na mfuko mmoja nyuma, urefu unaoishia magotini, isiyo na zipu.

2. T-shirt ya rangi ya kijani (Green Vest)

3. Raba za michezo zenye rangi kijani au blue.

4. Shuka mbili za kulalia zenye rangi ya blue bahari.

5. Soksi ndefu za rangi nyeusi.

6. Nguo za kuzuia baridi kwa waliopangiwa mikoa yenye baridi.

7. Track suit ya rangi ya kijani au blue

8. Nauli ya kwenda makambini na kurudi nyumbani.

Mkuu wa JKT anawakaribisha vijana wote waliochaguliwa ili waweze kujiunga na vijana wenzao katika kujifunza uzalendo, umoja wa kitaifa, stadi za kazi, stadi za maisha na utayari wa kulijenga na kulitumikia Taifa letu.

Kuona orodha kamili ya majina ya vijana waliochaguliwa na maeneo ya makambi ya JKT waliyopangiwa bofya kwenye jina la kambi hapo chini.

BOFYA JINA LA KIKOSI HAPO CHINI KUANGALIA MAJINA JA VIJANA WA MUJIBU WA SHERIA 2020

Tafadhali bonyeza jina la kikosi kutafuta jina lako

Nakumbuka kipindi chetu sie tulikuwa hatuendi hata na soksi maana zote tunapewa hukohoko hivyo vifungu 1-8 vyote vilikuwa vinagharamikiwa na serikali, achilia mbali na 50k ya posho kila mwezi serikali ilikuwa inamlipa mzabuni 8500 kwa siku na kwa kila mtu.
 
Nawaonea huruma watoto wa kike daaahhhh
Huruma kwa lipi,kama kubanduliwa,wameishabanduliwa,na matango ya kila saizi,kuna ambao nilisafiri nao kutoka Mwanza kwenda Arusha na Isamilo bus,njia nzima wanasimuliana walivyokunywa pombe,na jinsi maticha wao walivyokuwa wanawamendea.
 
Vijana waende tu kijifunza Uzalendo! Nina kijana wangu hapa yeye atariport Jkt Ruvu - pwani
 
Back
Top Bottom