JKT yatangaza majina ya vijana waliohitimu Kidato cha Sita 2020 wanaotakiwa kujiunga na JKT kwa Mujibu wa Sheria

JKT yatangaza majina ya vijana waliohitimu Kidato cha Sita 2020 wanaotakiwa kujiunga na JKT kwa Mujibu wa Sheria

Nikikujua wewe ni mzazi kisha unamruhusu mwanao wa kike aende JKT nitajitolea kukuchapa makofi.

Hata hivyo mimi mwenyewe sikwenda, nilifanya mradi wa serikali nikalipwa hela na kuijenga nchi. Wao wakajiviringisha kwenye matope na kuimba eti ndo uzalendo. Walirudi njaa kali na hawajafanyia chochote taifa.
 
Hope watafanya hivyo watu wasiwakatishe tamaa wadogo wetu kuna kitu watajifunza kwa muda mfupi wa mafunzo hao tusibeze
Saiv hamna Tena hivyo,lile fungu halipo Tena..
 
Nakumbuka kipindi chetu sie tulikuwa hatuendi hata na soksi maana zote tunapewa hukohoko hivyo vifungu 1-8 vyote vilikuwa vinagharamikiwa na serikali, achilia mbali na 50k ya posho kila mwezi serikali ilikuwa inamlipa mzabuni 8500 kwa siku na kwa kila mtu.

Hii bure kila kitu iliitia nchi umasikini sana na deni kubwa la Taifa wakati JKN ndio maana baadae ilifutwa na ilibidi ikawa RUKSA tu kila kitu wakati wa AHM, mwenye kupiga dili na apige, ustawi wa jamii ukapanda kwa mmoja mmoja, tena akaja BWM akasema piga dili lakini jifiche sio mambo hadharani.
Mara akaiingia JMK ikawa biashara huria, sasa tunarudi kwa mjukuu wa JKN aka JPM, lakini wakati ukuta.

Hitimisho: Upuuzi mtupu!!!!!£$%&@?
 
Vijana wenye mipngo ya jeshi tafuteni lonja mapem ya kujua kambi watakazopita hao jamaa kuchukua wale vijana wa kuunga mruke nazo otherwise mnaenda kujira tu
 
Hivyo vitu vya kwenda navyo tulikuaga tunavikuta huko, nashangaa kipindi hiki wanatakiwa waende navyo hadi nauli hivi kuna posho kweli siku hizi, What's happening with mama Tanzania???
Kuhusu nauli ukifika unaonesha tiketi unarejeshewa.

Wanachelea kuwatumia nauli 'watoro' wakafanya fursa!

Ila hili la bukta na shuka, ni suala jipya ama limekaa kipigaji, wataandaaje mafunzo bila kuandaa yote hayo ambayo ni ya msingi?

Sababu jeshi humvisha mtu kuanzia chupi ili asiwe na uchungu na nguo hizo wakati akigaragazwa mavumbini.
 
JKT ina faida gani wa FORM 6? , niya kufuta muda ukifika
 
Nasikia suala la kupigana miti kimasihala huko ni jambo la kawaida sana. Jamani kuna ukweli wowote hapo?
Kwa mtoto wa kike ukitamaniwa unaandamwa wewe tuu wewe tuu hadi unajihisi una mkosi mkubwa wa ajabu kuliko wenziyo!

Sasa njemba ikiona umechoka na sulba zile na umelainika vilivyo ndiyo mwishowe inajifanya kukuonea huruma na kukukingia kifua!

Mbinu hiyo sasa haina cha ukali, msimamo and the like, lazima kitu kisomwe na inakuwa ni siri yako lakini 'kibaka' akichekelea, na kusherehekea mbinu yake chafu na ya kishenz.

Maana yake ni kwamba hakuna mwanamke yeyote duniani asiyehitaji upendeleo wa ziada... hakuna mkate mgumu mbele ya chai.
 
Dah! nakumbuka kipindi naenda 832 kj nilitoka na begi dogo la mgongoni ndani likiwa na tracksuit moja na sweta lake(hii nilivaa siku za uzalendo peke ila baada ya intro sikuwahi ivaa tena [emoji23]), boxer 2 ,pamoja,raba pair moja vingine kama pitshort, green t-shirt,combat full(karanga) na boots zake tulipewa jeshini huko huko pamoja na posho ya 50,000/= kila tarehe 28 ya kila mwezi .Hapo ni 2016 op magufuli intake ya kwanza .
Maajabu baada ya hapo mambo yaka change , naona vijana wanaji nunulia kila kitu na posho sidhani kama wanaijua [emoji23][emoji23][emoji23].

Sent using Jamii Forums mobile app
Zamani sisi tulilipwa sh.50! Hiyo hiyo yenye kona kona, nusu ya mia unayoijua wewe.
 
Nchi imesambaratika hakuna mawasiliano kati ya kitengo/Idara moja ya serikalini na nyingine.
Hawa wanafunzi wanatakiwa kuanza kujaza maombi ya Loan Board mwisho wa July. Wakati huo huo waende JKT.
Matokeo yatoke August wakiwa Jeshini halafu waanze kuomba Vyuo Vikuu.

Awamu ya viroja hii.

Halafu wameanza kuwabebesha wazazi mizigo wa kununua vifaa. Wameomba kwenda huko? Kwa nini serikali isinunue?

Utashangaa wao wenyewe ndiyo wauzaji vifaa vinavyotakiwa.

Wazee wa Elimu bure hao.
 
Vijana wenye mipngo ya jeshi tafuteni lonja mapem ya kujua kambi watakazopita hao jamaa kuchukua wale vijana wa kuunga mruke nazo otherwise mnaenda kujira tu
Hivi ikitokea sijaenda hayo Mafunzo je nini kitatokea au watanichukulia hatua zipi ???
 
acha tu, mabinti wengi wanatoka huko na UKIMWI, ndoto zao zinaishia hapo, laiti wazazi wangejua kinachoendelea huko, wangesikitika sana
Du!
Unamaana Inabidi tuwapime kabla na baada ilituwe na lakusema
 
Nakumbuka kipindi chetu sie tulikuwa hatuendi hata na soksi maana zote tunapewa hukohoko hivyo vifungu 1-8 vyote vilikuwa vinagharamikiwa na serikali, achilia mbali na 50k ya posho kila mwezi serikali ilikuwa inamlipa mzabuni 8500 kwa siku na kwa kila mtu.
Na tulikua tunarudishiwa nauli tuliyotumia kwenda tunapewa nauli ya kurudi home na allawonce ya kujikimu njiani.
OP:MIAKA 50 YA MUUNGANO(2014)
 
Sio KWELI maana kuna waliobaki wakakaa hadi miaka mitano hakuna kitu wakarudi kitaa kuanza upya na umri umekwenda
 
Kama ukitaka kujitolea kwa sisi wengine watu wazima utaratibu ukoje?
 
Back
Top Bottom