JKU ni JWTZ ya Zanzibar?

Sawa mkuu ila hata huyo cammissioner wa polisi zanzibar taarifa zake anazituma kwa IGP anafata chain of command, kuhusu maelekezo wote wanapokea maelekezo kutoka kwa amir jeshi mkuu ambae ni rais wa JMT
Nakuelewa na naelewa chain of command yote mkuu!...
Je unahisi ni kwanini Siku ya Mapinduzi Rais wa zanzibar ndo huwa amiri jeshi mkuu kwa muda?
Tuanze kwanza kwa kujibu hilo..
Mengine yatafuata
 
Mkuu endelea kujidanganya na kujipa Moyo na vipi kuhus Jeshi la mafunzo ya Kupambana na uhalifu lililo chini ya katiba ya zanzibar ibara ya 122..
 
JKU ni zanzibar peke yake na Commander in Chief wa JKU ni Rais wa zanzibar na sio Rais wa Tanzania..
Mkuu sijui unafahamu hicho?
Inahitaji kiasi fulani cha ukichaa kuweza kuamini kuwa Zanzibar si nchi. Kama Katiba ya nchi ya Zanzibar imetamka kuwa Zanzibar ni nchi, mtu awaye yote kusema vinginevyo atakuwa anabwabwaja tu.
 
Kwaiyo ni km kule sudan kuna jeshi la serikal na kuna jeshi la raisi ambayo saiv wanagombea madalaka

So jku ni jeshi la zanzibar na linapokea amri toka kwa raisi wa zanzibar

Tunaomba utueleweshe vzr zaidi
Changanya na zako.
Ila kwa ufupi Watanganyika ni wajinga kama si wapumbavu.
 
Kwani jukumu la Jeshi ni kupindua nchi?

Kati ya JKU na Jeshi lililomwingiza Karume madarakani lipi lina hadhi ya Jeshi?
 
Ufala fulani hivi ambao unavhafua na kuchefua Muungano, ipo siku atakuja mtu anaejielewa na mzalendo haswa atafuyilia mbali upuuzi huu
 
Kwenye wasomi wajinga ni asilimia 100 naunga mkono hoja
 
Kwani jukumu la Jeshi ni kumpindua nchi?

Kati ya JKU na Jeshi lililomwingiza Karume madarakani lipi lina hadhi ya Jeshi?
Nimecheka sana 🤣🤣
Ye ameona kazi ya Jeshi ni kupindua Nchi.
Hii mindset tuliyonayo wabongo.Dah
 
Mkoa unaotambulika kama Nchi?
Ok nimekuelewa hata wanaoapa huko wanaapa kwa.katiba ya Zanzibar ambayo inatambua kuwa zanzibar ni nchi wakati waapishwa wanatambua kwmba kama zanzibar ni mkoa.?
View attachment 2891649
Mimi siyo mwanasheria, msinishangae kwa maswali yangu!

Sijui inatamkwa ibara ya 4 au kifungu cha 4, lakini inasema kuwa kunapotokea kuna Sheria inayopingana na Katiba hii ya Zanzibar, basi ya Zanzibar ndiyo itakayokuwa na nguvu hivyo hiyo nyingine itahesabiwa ni batili.

Swali langu ni hili: Katiba ya Zanzibar inaweza kuwa na nguvu dhidi ya Katiba ya JMT? Ikitokea Katiba ya JMT inapingana na ya Zanzibar, ya JMT itabatilishwa?
 
Kwenye katiba tunaita Ibara na kwenye Sheria tunaita kifungu...

Hapo ndo kuna Mgogoro Mkubwa mkuu!
Maana katiba ndo sheria mama..
Na Katiba ya Tanzania na katiba Ya zanzibar zinapingana Sana..
Na hiyo Ibara ya 80 inasema hivi pia naweka picha hapa chini..

Unajua Spika Wa Tanzania hana Mamlaka juu ya Spika wa Zanzibar pia?

 
Ni sahihi mkuu!
Spika wa nchi mmoja atawezaje kuwa na mamlaka juu ya Spika wa nchi nyingine, tena nchi huru yenye mamlaka yake?
 
Ni sahihi mkuu!
Spika wa nchi mmoja atawezaje kuwa na mamlaka juu ya Spika wa nchi nyingine, tena nchi huru yenye mamlaka yake?
Tanzania ina Spika wawili..(Muhimili w kwanza)
Tanzania ina Majaji wakuu wawili (Muhimili wa pili)
Tanzania ina Marais wawili (Muhimili wa Tatu)

Watu sijui kwanni hawaelewi kwamba hakuna muungano?
 
kimsingi kabisa huu muungano una wanufaisha wazanzibar kuliko watanganyika.
hii jku huku bara hatuwezi iweka hata ktk hadhi ya mgambo,ndio sababu katika ulinzi na usalama kuna jwtz moja,polisi moja,tiss moja.

kikundi chochote kitakachoanzishwa nje ya kanuni hizo kinakosa nguvu na mamlaka moja kwa moja ndani ya bara.
 
Pumzisha dukuduku lako juu ya Zanzibar. Binaadamu huwezi beba matatizo yote ya dunia au ya Zanzibar
Kila wakati utavurumisha uzi wa kinafiki kuhusu muungano.
 
Acha ujuha jku inamiliki silaha zote unazo zijua,halaf unalinganisha na mgambo wako,jku ni jeshi kamil
 
Acha ujuha jku inamiliki silaha zote unazo zijua,halaf unalinganisha na mgambo wako,jku ni jeshi kamil
juha ni wewe uneyedhani jku ni jeshi.

hao ni migambo tu.silaha hata alshabaab wanazo.
 
Kwa hiyo mnajiona mmeshinda au sio
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…