Job Ndugai: Anayesema vijana wa Bodaboda wamelaaniwa labda amelaaniwa yeye

Job Ndugai: Anayesema vijana wa Bodaboda wamelaaniwa labda amelaaniwa yeye

Tatizo vijana wengi wa bodaboda ni walevi wa pombe bangi ugolo nk bofaboda ni ajira nzuri sana kama ikizingatiwa kanuni na sheria za barabarani
Ajira ambayo unaumia kwa jua, mvua, upepo, baridi, vumbi.
Ajira ambayo huna uhakika wa matibabu?
Ajira nzuri ambayo ukiugua huna uhakika wa kula?
Ajira ambayo mkono au mguu ukivinjika ndo mwisho wako?

Hebu tufikirie njia zingine na sio huu upumbavu

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Hakuna mahali alisema vijana wa bodaboda wamelaaniwa bali alisema kazi ya bodaboda ni laana,mana haina matumaini na nikazi inayoumiza vijana wengi,job aache unafiki akae kutulia mana ametengeneza taifa la hovyo.
Huyu mzee bichwa lilisha vuligika kabisa! muda wote anafikiria kire kiti chake ndiomaana hata kwa hili kakulupuka
 

Spika Mstaafu wa Bunge, Job Ndugai amewataka Watanzania kuacha tabia kutothamini mafanikio au juhudi za watu mbalimbali wanazozionesha katika taifa hasa katika sekta ya biashara, akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mgahawa wa Chakula katika Taarafa ya Pandambili Iliyopo njia Kuu ya Kutoka Dodoma Owenya Morogoro.

Amesema "Kijana anza kufanya biashara halali, kazi ni kazi, achaneni na yule anayesema watu wamelaaniwa labda amelaaniwa yeye, yule anayesema vijana wa Bodaboda wamelaaniwa, sasa ule si wenzawazimu tu."

Chanzo: GlobalTV
Mimi anayehangaika na matamshi ya yule kijana alikuwa kule ugaibuni ambapo ule mchicha mkali wao unaliwa hadharani, kwakweli anapoteza mdaa.
 
Kama wafanya kazi mazingira magumu kwa afya yako, kazi ambayo hauna uhakika wa kurudi nyumbani, kazi ambayo huna uhakika wa matibabu na wanasiasa wako upande wako, jua kabisa wewe ni daraja

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
Maisha ni mchezo wa kufa na kupona.

Hakuna kitu salama hapa duniani.

Kimsingi maisha yako hayana usalama hata kidogo
Hisia zako tu ndo zinakudanganya uko salama.

Kama ingekuwa ni hivyo basi kusingekuwa na bodaboda sababu hakuna anayependa kufa.
 
Back
Top Bottom