Job Ndugai: Ipo haja ya kusimamisha mshahara wa Tundu Lissu kwa sababu hayupo jimboni, Bungeni na hospitalini na sijapewa taarifa ya Daktari

Job Ndugai: Ipo haja ya kusimamisha mshahara wa Tundu Lissu kwa sababu hayupo jimboni, Bungeni na hospitalini na sijapewa taarifa ya Daktari

Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema kuna haja ya kusimamisha mshahara wa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu kwa sababu hayupo bungeni, jimboni kwake wala hospitalini, na hajapewa taarifa zozote na daktari. #GlobalHabariUpdates.
View attachment 1015718
Sawa kabisa.Hawezi kuendelea kuidhalilishi nchi na serikali halafu serikali hiyo hiyo anayoidhalilisha na kuisaliti imlipe mshahara.Ale jeuri yake.
 
Hahaha hivi unaamini kabisa Lissu kwa jinsi anavyopendwa na Watanzania anaweza kupata tabu ya hela?!

Sent using Jamii Forums mobile app

Hakuna mahali niliposema napenda apate tabu tayari ameshapata tabu na anaendelea kupata tabu hivyo mimi siwezi wala kupunguza kupata kwake tabu, ila hakuna maana kuendelea kumlipa mtu mshahara ambaye hafiki kazini, mimi nisiporipoti kazini kwa ugonjwa halafu nikaonekana napiga selfie mitandaoni nitafukuzwa pia.
 
Ukiona mshahara mesitishwa ujue ndio mwanzo wa Lissu ku-bid bye bye Bungeni. Pengine atasubiri kugombea urais ambao nao ni mawili kwa kuwa kuna mashaka iwapo atatimiza lengo hili maana E. N Lowasa, mwansiasa mwenye ushawishi mkubwa ndani na nje ya Chadema amekuwa kwenye maandalizi hayo hayo tangu 2015. Who knows, it could be such an unceremonious end of punch politics of Tundu Antipasi Magwai Lissu.
Mbona wewe na Barbarosa mnabadili badili posti zenu mimi natunza kumbukumbu
 
Ni kweli jamaa anachukua malipo bila kufanya kazi..

Akiambiwa arudi kazini anadai anaumwa ila yupo busy kufuata Interview za TV miji Mbali Mbali duniani akialikwa Australia ataenda ila kwenda kufanya kazi bungeni hataki.
Unataka aje wammalizie???

Akija ujue ndio mwisho wa hizo jinga mbili jiwe na andunje

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wameshindwa kumuua sasa wanatamani kusitisha mshahara wake lakini wameshindwa kujua ya kwamba malipo ni hapa hapa duniani
 
Hakuna mahali niliposema napenda apate tabu tayari ameshapata tabu na anaendelea kupata tabu hivyo mimi siwezi wala kupunguza kupata kwake tabu, ila hakuna maana kuendelea kumlipa mtu mshahara ambaye hafiki kazini, mimi nisiporipoti kazini kwa ugonjwa halafu nikaonekana napiga selfie mitandaoni nitafukuzwa pia.
Mimi nakuuliza kama unaamini anaweza kupata tabu ya kukosa pesa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bunge la Tanzania kabla ya kusitisha mshahara wa Lissu ni sharti lijiulize yafuatayo:-
1 -Je -Waliompiga Lissu risasi wameshapatikaka?

2 -CCTV ulishawai kuhoji nani amezitoa?

3 -Lissu alipigwa risasi akiwa Jimboni au kazini Hapo Dodoma?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahaha hivi unaamini kabisa Lissu kwa jinsi anavyopendwa na Watanzania anaweza kupata tabu ya hela?!

Sent using Jamii Forums mobile app
😂😂😂 Mbona mabeberu walikacha kwenye mhadhara chuoni jana?
Dyr6Dt5X0AAz74P.jpeg
 
Back
Top Bottom