Job Ndugai: Ipo haja ya kusimamisha mshahara wa Tundu Lissu kwa sababu hayupo jimboni, Bungeni na hospitalini na sijapewa taarifa ya Daktari

Job Ndugai: Ipo haja ya kusimamisha mshahara wa Tundu Lissu kwa sababu hayupo jimboni, Bungeni na hospitalini na sijapewa taarifa ya Daktari

Binadamu unakua na Roho ya kikatili mpaka shetani mwenyewe anakushangaa ujue...unakua huna hata chembe ya kumuogopa Mungu kisa uwafurahishe binadamu wenzio wanaokutuma kinachotokea ni karma mbaya sana unayoipanda kwenye familia yako Ubaya unarudi Mkuu jifunze...
 
Uamuzi huu utakuwa ni moja ya kosa kubwa sana na Lissu ataendelea kupata support kubwa sana!

Hawa watu Mungu kawanyima akili na maarifa.
 
asimpe mshahara wake, lissu atalipwa na wananchi, nguvu ya umma ikiamua hakuna wa kuweka uzio. Watu wamechanga pesa ya lissu kwenda kutibiwa nje tena VIP Hospitals, sembuse mshahara?
 
Basi shetani akaja akamwuliza Yesu, ikiwa wewe ndio mwana wa Mungu, badili haya mawe yawe mkate. Yesu akamjibu akisema, Mtu hataishi kwa mkate tu bali bali kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu.

Inanifikirisha sana maeneo makuu mawili
a. Badili mawe yawe mkate = Sema uongo/ miujiza hewa
b. Mtu ataishi kwa mkate tu = mshahara
 
Hayo ni mawazo yako tu kuwa ameponzwa

Lissu uhai wake kwanza kuliko fedha, Lissu hatishiki na kauli za lofa adunje ambaye anatimiza matakwa ya aliyemtuma

Lissu hana shida kama mnavyoamini kuwa mnaweza kumkomoa

Lissu anaweza kupata pesa ndefu sana kuliko hiyo anayolipwa na bunge

Jiulize gharama ya matibabu ya mh Lissu ni kiasi gani? Na hizo pesa alipata wapi?

Lissu yuko hai leo kwa sababu ya watu wema wanaojali utu bila kujali itikadi za kisiasa

Lissu hammuwezi mtaishia kuaibika tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kambale anazidi kumeza ndoano. Hiyo kitu ilishakuwa calculated na ilishajulikana kuwa hizo ndizo zitakuwa only last kicks left of the dying horse.
Sema hesabu zimekataa kidogo maana matarajio ni muuchukue kabisa huo ubunge wenyewe.
Kosa vyote usikose akili, hekima na busara. Mumemnyima pesa ya matibabu na kila kitu, mkawakamatavwaliokuwa wanamuombea, pamija na yote kazawadiqa uhai na ujasiri to 'Tell the Tale' , halafu eti mnarudia kimnyima hela ambazo wakati anazihitaji ili kuokoa uhai mulimnyima leo hii yupo hai na akiwa ameandika historia, na sasa akiwa katika world class platforms eti mnataka awapigie magoti kwa ajili ya heza hela ambazo ninyi wenyewe haziwasaidii zaidi kuwaharibuni akili na kuwaongezeeni madhambi tu.
 
Utaona unamsimamishia mshahara wake lakini pigo utakalolipata maishani mwako hayatakuacha salama. Huyo ni mtu wa kumhurumia.
 
kwani akupe taarifa ya maendeleo ya afya yake kwan kuna taarifa uliwahi kupewa ya kuumwa kwake??

wakubwa mmechanganyikiwa sasa badala ya kutafuta namna ya kupooza hii sintofaham ndoo kwanza mnazid kuiwasha!! athali ya haya maumivu yanachanganywa na kutolipowa matibabu aisee mtajuta kumuumiza Lissu
 
Back
Top Bottom