Job Ndugai: Ipo haja ya kusimamisha mshahara wa Tundu Lissu kwa sababu hayupo jimboni, Bungeni na hospitalini na sijapewa taarifa ya Daktari

Job Ndugai: Ipo haja ya kusimamisha mshahara wa Tundu Lissu kwa sababu hayupo jimboni, Bungeni na hospitalini na sijapewa taarifa ya Daktari

Sasa arudi bungeni ili ashambuliwe tena? Kama mtu anadai gari lilimfuatilia tangu bungeni mpaka nyumbani kwake na bado hiyo gari haijajulikana ,hapo bungeni ni mahali salama kwake kama akirudi?
Kwaiyo ataishi ughaibuni tu na pesa zetu anajichotea?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nionavyo mimi kumnyanyasa kwa kumnyima mishahara na posho, kumnyima pesa za matibabu nk ni kumpa cha kusema huko nje hata kama serikali ina haki hiyo.

Kama serikali itafanya hivyo haitasaidia kabis azaidi ya kujibomoa, kwa maana sasa Tundu Lissu Hatategemea pesa kutoka serikalini atapata ma dola mamilioni kwa ajili ya kuichafua Tanzania.

Naishauri serkali kwamba kukaa kimya nalo ni Jibu.

Lakini kila anachosema serikali au Bunge au CCM tunahamaki kumjibu ni kujitaabisha tu hayo yote ni matokeo ya maamuzi ya kibaguzi ya Bunge.
 
tunaweza kuchanga kwavidole lakini nawahakikishia mchango huo hautafika miezi 3 kwa idadi ileile na wengine watarudi na malalamiko.
kinachohitajika sio zima moto wala fedha ila cha kujadili nini kifanyinge mapungufu yaliyojitokeza kwatukio zima lisiweze kutokea tena kwa wengine na njia gani inaweza kuwa muafaka kama fidia ya kudumu kwa changamoto alizopitia kikaweza kumliwaza aliyeumizwa nafsi na mwili wake.
 
Embu labda tupate msaada wa Anapomzunguumzia daktari amabe anatakiwa kumpa taarifa Spika anamzunguzmzia dokta yupi wa hosptal gan ambayo Kama Bunge lina mawasiliano nao?
Tunamzunguzmia daktari ambae ili amtibu mtu mgonjwa wako inabd alipwe na akimshamtibu alete mrejesho kwa mgonjwa na anamehudumia Mgonjwa so sjajua kama Bunge limemlipa daktar yupi ili kupata hayo majibu ya Mgonjwa Lissu.
Mwenye majibu naomba..............
Lissu ni mtoro ila Ndugai anachukulia poa tu. Alitoroka kuanzia siku viongozi wa cdm walivyomtoroshea Kenya hadi Ubeligiji.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa sababu amejiaminisha kwamba wazungu ndo wataweza kumsaidia shida zake, basi ni vema awaombe waanze kumlipa mshahara na hata kumpa hifadhi
 
Ni kweli jamaa anachukua malipo bila kufanya kazi..

Akiambiwa arudi kazini anadai anaumwa ila yupo busy kufuata Interview za TV miji Mbali Mbali duniani akialikwa Australia ataenda ila kwenda kufanya kazi bungeni hataki.

Wewe mpaka mauaji ya Itigi unasupport kwahiyo nakuonea huruma maana najua una stroke ya ubongo
 
Kama kweli mshahara wa Tundu Lisu utazuiliwa baada ya mbunge huyo kumaliza tu mahojiano luningani yaliyomshirikisha pia mwakilishi wa Rais balozi Masilingi, basi bungeni labda kuna mambo hayako sawa.

Siamini kama Katibu wa bunge anaona huu ni wakati muafaka wa kusimamisha mshahara wa Lisu kwa sababu hii inampa uwanja mkubwa Tundu kwa kumuongezea vitu vipya vya kuongea.

Lakini sioni sababu za msingi za kuutangazia umma pale mshahara wa mnunge au mtumishi unaposimamishwa kwa sababu yoyote ile.

Zitto aliwahi kufukuzwa bungeni wakati wa Buzwagi na ndio akazidi kuwa maarufu.

Tusifanye maamuzi kwa jazba na kisiasa
Maendeleo hayana vyama!
Nikisemaga Tanzania ina mang'ombe huwa niko sahihi 1

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wasitishe wataona nguvu ya umma jamaa hatakufa njaa wanaweza kumchangia vile vile milioni kumi na tatu siyo kitu $5600 hiyo anaweza kupewa kama allowance hata na wapinzani wa serikali ndani ya CCM endelee kupiga kelele akiwa huko nje ya nchi...kuna mambo yanaleta aibu sana yanayofanya na bwana Job...kukaa kimya kuna kuna nafuu, unless otherwise kama nao wanachokoza hoja hii saga iendelee na hatimaye wahusika watiwe mbaroni
Thubutu eti nguvu ya umma!!

Hiyo unayoita nguvu ya umma tungeona kwa Mwenyekiti hadi leo yupo Segedansi.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mpaka Muda huu ilitakiwa Katibu Mkuu wa Bunge ajiuzulu Kama aliendelea kumlipa Mtu Mshahara wakati hayupo eneo la Kazi Na Hakuna taarifa yoyote ya kimaandishi ya kutokuwepo kazini Na Sasa hivi anaonekana anazurura Kwenye Channel Za Kimataifa anachafua Nchi
Unaongea kijingajiiinga utadhani unaongelea mshahara wa Hamifirei Tarapole
 
Lissu kwasasa hana cha kupoteza, Mshahara kwake si kitu....

Yeye Ndugai kama Spika anapaswa kujua hali ya Lissu bila hata Lissu kumtaarifu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndugai na MKUU wake ni wabaguzi ..

Mbna yy alipoenda kutibiwa hakusimamishiwa mshahara?

Yaani ndugai anatumia ushauri wa msukuma? Kweli darasa LA 7 waondolewe bungeni

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom