Job Ndugai: Ipo haja ya kusimamisha mshahara wa Tundu Lissu kwa sababu hayupo jimboni, Bungeni na hospitalini na sijapewa taarifa ya Daktari

Job Ndugai: Ipo haja ya kusimamisha mshahara wa Tundu Lissu kwa sababu hayupo jimboni, Bungeni na hospitalini na sijapewa taarifa ya Daktari

Viongozi wa CDM, wajadili na kupiga mahesabu ya Mshahara na Marupu rupu ya Mh.Lissu, ambayo Spika Job Ndugai na wana hira wenzie, wanataka kuuzuia kisha watutangazie sisi wenyewe wa Tanzania tutamchangia Mh.Lissu kwa kufidia Mshahara utakao kuwa umepokonywa na Bunge uchwara!

Ni vema waandae Akaunt maalum ya Bank kwa mchango huu.
Ninaunga mkono wazo hili kwa asilimia 100%.
Kama kuna viongozi wa CHADEMA wanatembelea jukwaa hili, tafadhali lifanyie kazi.
 
Mtu mzima unapoambiwa au amrishwa ufanye jambo fulani then ukajitokeza ukafanya kama ni utashi wako kumbe ni kuambiwa tukuiteje?
1. Njaa kichwani
2. Njaa tumboni
3. Kufikiri kwa kutumia vidole
4.....
 
Ukiangalia video vema,utabaini kua mhe msukuma alikua katumwa kuuliza swali hilo mapema kabisa,maana kabla ya kipindi cha maswali na majibu siku ya alhamis,uanza maswali kwa waziri mkuu,na kabla ya waziri mkuu Mhe msukuma alisimama na kuomba mwongozo,wakati mwongozo kwa mujibu wa kanuni uombwa wakati kuna jambo lilikua linaendelea kabla.lakini mhe spika akajibu na kukubaliana na msukuma,ule ulikua ni mpango maalumu kabisa,alipomaliza kuutolea maelekezo ndo akaitwa mhe waziri mkuu kuendelea na maswali ya papo kwa papo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mm nina mawazo sawa na Spika pia.. Ni hivi, ingekuwa Mh. Lissu bado yuko hospitalini, au karudi nchini kwa wananchi waliomchagua anapaswa kulipwa mshahara na stahiki zake zote kama kawaida, ila sababu ni muda sasa katoka hospitali na yuko huko nje ya nchi anaitwa kila kituo cha TV duniani na kupata kusema anachojisikia, na ku attack bunge na serikali, mm nadhani hastahili kulipwa mshahara hadi arudi nchini na kama hajapona kwanini anatembea nchi zote hizo ktk media mbalimbali na kuchafua nchi yake..? Hatuungi mkono kabisa na tunalaani kwa vikali kitendo cha kushambuliwa kwa risasi alichofanyiwa Mh. Lissu hilo lieleweke wazi, that is our position, ila mgonjwa gani anazunguka duniani ktk TV mbali mbali na kuichafua nchi yake? Mgonjwa hawi hivyo hata kidogo..!!
"That is our position" kwake jiyo unawasemea kundi la watu.

Hivi mtu mgonjwa alipewa likizo ya kapumzike na Dr. Hatakiwi hata kuwatembelea ndugu zake? Hapaswi hata kuongea na ndugu Jamaal na marafiki waliomsaidia?

Serikali haikutani, Bunge halikumtibu, Je Lissu anapata wapo pesa za matibabu?

Kama hujui Basi huko anakoenda Ni kutoa shukrani Lea waliomtibia.

Hivi hamuoni anatembelea magogo? Kama mnaona kwa Nini mnauliza?
 
bora waukate kabisaaaa,heri kufa maskini kuliko kuishi maisha ya fahari na risasi mwilini
 
Hili suala Tundu Lissu sasa limegeuka kuwa TAMTHILIA.Ni tamthilia kali ambayo imetuonyesha washiriki hata tusiowatarajia;hata hivyo wameonyesha umahiri mkubwa was kuvaa 'uhusika'.Na kwa sasa tupo 'season 3' kwenye 'episode 2'.Tamthilia inaendelea.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hili suala wala halihitaji kutatuliwa sijui kwa sheria, hata Biblia inasema: Asiyefanya kazi, asile! Mimi sijui wale waliomchagulia akawawakilishe wapo kwenye hali gani, maana ni ajabu kuona mgonjwa anaongea sana, labda ugonjwa umeamia mdomoni.
 
Ndugai kila akiamka anakuja na tamko hili au tamko lile, hatujui kesho atapokea maagizo gani kutokea "juu"!
 
The government of some people,by some people for some people.according to tshaka
 
Back
Top Bottom