Job Ndugai: Ipo siku Tanzania itapigwa mnada, Watu tukishakopa tunapiga makofi kujipongeza. Deni la Taifa ni 70 Trilioni

"Wapinzani walituchelewesha sana." Alisikika yule shujaa.
Mkuu kumbe huko ng'ambo ya pili hali siyo shwari kabisa. Mimi nilikuwa naona tetesi hapa nikadharu lakini hili jiwe lililotupwa na Ndugai linaonekana kumlenga mtu kabisa. There should be something behind the scene! Kuna kitu Ndugai amenusa. Asingeweza kujilipua namna hii bila kunyaka mipango kabambe against him.
 
Hela ipo ila usimamizi sio mzuri! Tatizo linalotukwamisha ni usimamiz wa rasilimali zetu tumewapa madaraka watu wa hovyo!
Mkuu Extrovert,

Magufuli alisimamia nidhamu ya matumizi alipigwa vita hadi leo hii ambapo hayupo nasi na wengine wanasema afukuliwe azikwe upya kilomita 1 chini ya ardhi (kaburi ambalo litakuwa limevunja rekodi ya dunia) ili asije kuleta hata ndoto. Leo hii Zenji inakuwa Dubai kwa gharama za JMT na SMZ wakati Magufuli alipojenga ushoroba wa Kaskazini (Northern Economic Corridor) aliambiwa anapoteza ela kupendelea Chato, si bora Chato iko Tanganyika. Nawaambia in 10 yrs time now on... Zanzibar itakuwa Dubai ya Afrika, ndipo majuto yatakuwa mjukuu kwa Watanganyika.

Introvert.
 
Wafu wanazikana wenyewe.
 
Bado unajisifia kenya 67% kwa yetu 35% siyo? Walio jikoni wameona Kuna tatizo. Wewe unaona sana. Una mzazi au ndugu mpiga makofi mle bungeni hata spika aki ja---mba?.
 
Anaoneka kama anauchungu sana na taifa ila sasa.....
Labda ameona Bandari ya Bagamoyo imepotezewa wakati aliishakarimiwa kupitia Sino-Africa Blackmail, mimi nafikiri tupunguze matumizi ya Mhimili wa Bunge ili tulipie mikopo hiyo. Mbona Raila alimbana Kibaki hadi wabunge wakapunguziwa maslahi na serikali ikapumua.
 
Wacha tuendelee kusubiria
 
Inafikirisha sana nchi iliyojaariwa utajiri mkubwa inahoji kipi bora kati ya kuongeza tozo kwa wananchi wake ama kukopa pesa zitakazolipwa na wananchi wake.
Kazi kwelikweli.
 
Inafikirisha sana nchi iliyojaariwa utajiri mkubwa inahoji kipi bora kati ya kuongeza tozo kwa wananchi wake ama kukopa pesa zitakazolipwa na wananchi wake.
Kazi kwelikweli.
Yani eti wanaona tuna option mbili japokuwa tuna kila aina ya rasilimali. Yani kwao option ni either tukope au tozo
 
Tafsiri ya malalamiko ya Spika ni kwamba Mhimili wa Bunge umeshindwa kufanya kazi yake ya kuisimamia serikali (inakopa hovyo hovyo). Hivyo basi, Mhe. Ndugai kwa kauli yake anathibitisha kuingia rasmi kwenye kundi la akina Polepole, Gwajima na Silaa.
Na kama Bunge limeshindwa kuisimamia serikali bora basi livunjwe twende kwenye uchaguzi, ili tupate pia Bunge ambalo silo la Magufuli labda.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…