Job Ndugai: Ipo siku Tanzania itapigwa mnada, Watu tukishakopa tunapiga makofi kujipongeza. Deni la Taifa ni 70 Trilioni

Job Ndugai: Ipo siku Tanzania itapigwa mnada, Watu tukishakopa tunapiga makofi kujipongeza. Deni la Taifa ni 70 Trilioni

Mkuu humu kuna watoto sasa hivi mpaka shule zifunguliwe, sijui wanachokidai hata kama walikuwepo miaka hiyo kuona kama ilikuwa inafanyika hivyo, mkataba unawekwa wazi kwa wananchi,
Nimekuelewa Chief,ahsante kwa kunifumbua.But wanatumia a/c za wazazi wao huku jukwaani?
 
Huyo mwamba ana hoja na ajibiwe kwa hoja.

Ni kwanini kweli pesa ya mkopo inaenda kujenga madarasa yaleyale ambayo km Nchi tumejibana kwenye tozo kufanya kwalo?

Kwa nini hiyo pesa isingeelekezwa kwingineko ili ifanye mambo mengine?

Mbona hatupewi mrejesho wa pesa za tozo ni wapi na kipi zinafanya?

Job ameuliza mambo ya msingi sana na ajibiwe kwa hoja.
 
Kwani Ndugai aloyongea yote ni ujinga?

Anahoja ya msingi kwa baadhi take

Tuliambiwa Tozo inaenda maliza uhaba wa madarasa na vifaa vyake vypte

Matokeo yake fedha ya mikopo nayo iko hukohuko
 
Watuambie basi pesa za COVID zimefanya nini!???maana yale madarasa tunaambiwa ni ya COVID....
 
FATHER MICHONGO UMEMSIKILIZA GAVANA WA BENKI KUU


UNAPOKOPA KUFANYA MRADI UHIMILIVU WAKO WA DENI UNAENDELEA KUWA MZURI .

"Unapokopa mkopo hukopi kwa ajili ya kula unakopa kwa ajili ya kufanya project ambazo zitaendelea kuzalisha na kwasababu unaendelea kuzalisha uhimilivu wako wa deni unaendelea kuwa mzuri sio kwamba deni linapanda" Gavana Benki Kuu Tanzania, Profesa Florens Luoga

NCHI HAIWEKI REHANI WATU WALA RASILIMALI ZAKE -GAVANA BENKI KUU

"Katika kamati mnaangalia madeni yenu yasiuze nchi ndio maana nchi haiwezi ikaweka rehani watu au rasilimali zake na itahakikisha inazitumia ili kuhakikisha Serikali inaendelea kupata kipato" Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Florens Luoga

#PowerBreakfast #CloudsFm

View attachment 2061491
Kazi apigwe tu mnada, maana ameshazoea minada ya ng'ombe, sasa na yeye anatamani kuwa moooo
 
Je tunaendelea kuzalisha ?

Au ndio tunakopa sijui tungue bandari ya wapi, kesho tunaachana na hio bandari tunakopa tuanzishe kitakachoachwa na awamu ijayo....

Mwisho wa siku ni watu kula 10% zao na wananchi kubaki na zigo la madeni.....
 
Hivi huyu Luoga katuambia huo mkopo “utaendelea kuzalisha kitu gani”

Jaribuni kuelewa perspective ya Mr. Job Ndugai. Kwa sasa asibezwe eti mbona alikaa kimya wakati wa Jiwe. Two wrongs never make a right
 
Back
Top Bottom