Baada ya tafakari ya muda mrefu sana nimelazimika kuyaelewa maneno ya Spika Job Ndugai. Naungana nae.
Ni wazi kuwa maneno yake yamekuja wakati sahihi. Ameongea kama mwananchi wa kawaida kabisa... Na kwa vile yupo ndani ndani huko kuna mengi anayajua!
Cha ajabu sisi wananchi wa kawaida ndo wale wale tunaompiga vita na kumkashifu. Tulipaswa tuwe na harakati huru na endelevu za kutaka kujua matumizi ya fedha za mikopo na zile za tozo! Isije ikawa tunatumika kama dhamana ya mikopo ili wateule wachache wazidi kuneemeka.
Dalili za matumizi ya kufuru na anasa zipo wazi kabla hata ya SSH. Je, hatupaswi kwenda mbali zaidi kuhoji uhalali wa mikopo/tozo na matumizi yake?? Au tukishaambiwa na watawala basi tuufyate zaidi ya maandiko!